2026.06.27 Mkutano Mkuu wa makardinali mjini Vatican. 2026.06.27 Mkutano Mkuu wa makardinali mjini Vatican.  (@Vatican Media)

Kard.Brislin.Tujenge sinodi,kupitia uwepo,kusikiliza na uwajibikaji pamoja!

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Johannesburg,Afrika Kusini alifungua kikao cha tatu cha Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali akitafakari utangulizi na hitimisho la waraka wa Magnifica Humanitas.Nguvu ya teknolojia lazima ielekezwe kwenye mahusiano ya haki zaidi,taasisi zinazomjali zaidi mtu na mustakabali wa pamoja wa kweli.Kanisa liishi wakati uliopo kwa kujiamini na uwazi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Stephen Brislin, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la  Johannesburg nchini Afrika Kusini wakati wa ufunguzi wa  kikao cha tatu cha siku ya pili na ya mwisho ya Mkutano Mkuu maalum wa Makardinali  asubuhi ya  Jumamosi, tarehe 27 Juni 2026  katika Ukumbi wa Paulo VI alibainisha kuwa “Kukaa katika maeneo ya ujenzi wa historia kwa umbo tofauti, sinodi katika mbinu, yenye mizizi katika fadhila za kitaalimungu, na inayolenga huduma ya mtu ni jukumu sahihi lililokabidhiwa Kanisa na Waraka wa Papa Leo XIV wa Magnifica Humanitas.

Swali kugusu maendeleo ya kiteknolijia

Kardinali wa Afrika Kusini aliwapatia Makardinali hao tafakari kuhusu sehemu ya kwanza na ya mwisho ya waraka huo, ambao unategemea swali muhimu: kama maendeleo ya kiteknolojia yanaambatana na ongezeko la uwajibikaji au kama yanaweka ubinadamu katika aina mpya za kutengwa na kupunguzwa kwa uwajibikaji. Kardinali Brislin alibainisha swali hilo, kuwa linahamisha umakini kutoka kwa nguvu ya njia za kiufundi" hadi jinsi zinavyoweza kubadilisha uhalisia, kukuza au kuzuia "mahusiano ya haki zaidi, taasisi zinazozingatia zaidi binadamu, na mustakabali wa pamoja wa kweli. Tofauti hiyo, ni sawa na ile inayopatikana katika kujenga Babeli au Yerusalemu: katika ile ya kwanza, akili ya binadamu ni "kitendo cha kujitosheleza," na umoja, unaotafutwa "bila Mungu," husababisha kuvunjika,"alisema Askofu Mkuu wa Johannesburg.

Kujenga mji Mtakatifu ni uwezo wa bindamu kwa ajili ya utumishi wa Mungu

Kwa upande mwingine, kujenga Mji Mtakatifu kunamaanisha uwezo wa binadamu "uliowekwa kwa ajili ya utumishi wa Mungu na kitendo kinachoweza kukuza na kuwezesha heshima ya kila mtu. Lakini eneo la ujenzi wa Yerusalemu, Kardinali Brislin alisisitiza zaidi, pia ni ishara ya ujenzi wa sinodi ambao hauungi mkono maendeleo ya kiteknolojia kama mwisho wenyewe, bali hufanya kama ngome dhidi ya athari zake zinazovunjika. Mtindo halisi wa uwepo, kusikiliza, na uwajibikaji wa pamojs," sinodi inatoa mfano wa sarufi ya ujenzi iliyoelezwa katika vipengele vinne. La kwanza ni tamaa ya kibinadamu ya furaha, ambayo lazima ihifadhiwe katika ukweli wake. Teknolojia mpya, kiukweli, zinaahidi maisha ya starehe zaidi, yasiyoathiriwa sana na mateso, lakini kweli hupunguza furaha kuwa utendaji au udhibiti, na kumfanya mtu kuwa maskini.

Kard Brislin

Maisha ni zawadi tunayoipokea

Kipengele cha pili ni kikomo, ambacho kinatukumbusha kwamba maisha ni zawadi tunayopokea na yanahitaji kulindwa. Kwa hivyo, kupata tena hisia ya kikomo hutusaidia kuepuka "udanganyifu wa kujitosheleza." Hii inaleta kipengele cha tatu, yaani "uwajibikaji wa pamoja wa ujasiri," kwa sababu manufaa ya wote hukua "wakati kila mtu anaweza kuchangia sehemu yake na kuungwa mkono katika kuitimiza." Kwa hivyo, uungwana unakuwa "aina ya ushiriki uliopangwa." Hatimaye, kama kipengele cha nne, Kardinali Brislin alionesha vigezo vya utambuzi vinavyotolewa na Mafundisho Jamii ya Kanisa. Hizi zinaturuhusu kutafsiri michakato ya kihistoria, kutathmini ahadi za teknolojia, na kutofautisha kinachomtumikia mtu na kile kinachomfunua kwa aina mpya za utegemezi au kutengwa. Sarufi ya ujenzi iliyoelezwa mwanzoni mwa Waraka, inatimizwa katika kurasa za mwisho, ambapo inaelekeza nyuma kwenye fadhila za kitaalimungu: imani, upendo, na matumaini, Kardinali Brislin alielezea.

Kardinali  Brislin alisema, kwanza,  inaelimisha mtazamo, inafungua njia ya kutafakari mpango wa huruma unaoenea katika historia, na inatambua kwamba safari ya mwanadamu inaendelezwa na mantiki ya zawadi, inayozingatia fumbo la Umwilisho. Sadaka, kwa upande wake, hutoa ushirika na hupata chanzo chake cha kisakramenti katika Ekaristi, hivyo kuunda njia ya Kikristo ya kuishi katika historia, yaani, kwa kutufundisha kuwatambua wengine kama kaka na dada, kubeba mizigo yao, na kushiriki nao jukumu la kazi ya pamoja.

Tumaini uendeleza ujenzi wa ustaarabu wa upendo 

Hatimaye, tumaini huendeleza ujenzi wa ustaarabu wa upendo kwa kushirikiana na Kristo. Katika nuru hii uwezekano wa kiufundi "unakaribishwa ndani ya njia ya hekima, inayolenga heshima ya mtu, utunzaji wa nyumba na mahusiano yetu ya pamoja, pamoja na muungano kati ya sala na kujitolea kikamilifu. Haya yote, Kardinali Brislin alihitimisha, kuwa hayawezi kutenganishwa na sala, ili Kanisa liweze kujumuisha "ibada ya kikanisa inayoweza kuishi wakati huu kwa uaminifu na uwazi."

KARD BRISLIN

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

27 Juni 2026, 16:16