Baba Mtakatifu Leo wa XIV amemteuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo la Nkayi François Halyday Mbouangui kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nkayi, nchini Congo. Baba Mtakatifu Leo wa XIV amemteuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo la Nkayi François Halyday Mbouangui kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nkayi, nchini Congo. 

Askofu François Halyday Mbouangui Jimbo Katoliki la Nkayi Congo

Askofu François Halyday Mbouangui alizaliwa tarehe 4 Oktoba 1977 huko Mindouuli, Jimbo kuu la Brazzaville. Tarehe 14 Julai 2007 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 1 Desemba 2025 akamteuwa kuwa ni Askofu na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa ni Askofu tarehe 15 Februari 2026. Tarehe 1 Juni 2026 akatangazwa kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nkayi. Askofu Daniel Mizonzo ameng'atuka kutoka madarakani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe Mosi Juni 2026 ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Daniel Mizonzo wa Jimbo Katoliki Nkayi, Jamhuri ya Congo la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu mstaafu Daniel Mizonzo alizaliwa tarehe 29 Septemba 1953. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 12 Julai 1981. Akawekwa wakfu tarehe 6 Januari 2002 kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nkayi, Jamhuri ya Congo na kung’atuka rasmi tarehe 1 Juni 2026. Amelitumikia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 44.88 na kama Askofu kwa kuwafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kwa muda wa miaka 24.40.

Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Congo, Brazzaville
Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Congo, Brazzaville   (Le père spiritain Jean Marie Grivaz, immortalisé au Congo-Brazzaville, le 17 août 2024.)

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Leo wa XIV amemteuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo la Nkayi François Halyday Mbouangui kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nkayi. Itakumbukwa kwamba, Askofu François Halyday Mbouangui alizaliwa tarehe 4 Oktoba 1977 huko Mindouuli, Jimbo kuu la Brazzaville. Tarehe 14 Julai 2007 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 1 Desemba 2025 akamteuwa kuwa ni Askofu na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa ni Askofu tarehe 15 Februari 2026. Tarehe 1 Juni 2026 akatangazwa kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nkayi.

Askofu Congo
02 Juni 2026, 16:15