Uokoaji baharini Uokoaji baharini  (Mediterranea Saving Humans)

Ask.Mkuu Balestrero:Hatari ya 'utumwa wa mtandaoni'katika mipango ya ulaghai

Mitandao ya uhalifu mara nyingi hutumia majukwaa ya mtandaoni na njia zisizojulikana kuajiri,kudhibiti na kusafirisha waathiriwa wao,ambao mara nyingi ni watoto wadogo.Haya yalisemwa katika hotuba na Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa wakati wa Kikako cha 62 cha Baraza la haki za binadamu,Juni 22 huko Geneva Uswiss.Mada ilihusu biashara haramu ya watoto katika muktadha utaif, uhamiaji na uhamisho wa kulazimishwa.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Kuunganishwa kwa watoto na familia hasa wasiosindikizwa ni muhimu ili kutojikuta katika mikono ya wahalifu. Na kuna umuhimu wa kuzuia, kulinda, kukomboa, na kurekebisha tabia. Zaidi ya hayo, kuanzisha njia salama na za kawaida za uhamiaji husaidia kuzuia shughuli za wafanyabiashara haramu.  Haya yalisemwa na Askofu Mkuu Ettore Balestrero Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa mataifa na Mashirika ya Kimaifa katika hotuba yake,  wakati wa Kikao cha Kawaida cha 62 cha Baraza la Haki za Binadamu tarehe 22 Juni 2026 huko Geneva, Uswiss. Ujumbe wa Vatican ulizingatia juu ya Ripoti ya Mwandishi Maalum kuhusu "biashara haramu ya watoto katika muktadha wa kutokuwa na utaifa, uhamiaji na uhamisho wa kulazimishwa." Biashara haramu ya binadamu ni aina ya utumwa wa kisasa na ukiukaji mkubwa wa utu wa binadamu uliotolewa na Mungu alieleza 

Vitendo vinavyotokana na unyonyaji uliodumu

Mtoto aliyesafirishwa kwanza kabisa ni mwathiriwa, anayestahili ulinzi, huruma, na utunzaji, pamoja na fursa ya kurekebisha tabia, badala ya adhabu kwa vitendo vinavyotokana na unyonyaji uliodumu, alisisitiza Mwakilishi wa Vatican. "Uhalifu huo uko kwa wasafirishaji haramu, si mtoto. Udhaifu wa watoto wanaohama unazidishwa na mifumo ya kidijitali ambayo inaweza kuwezesha biashara haramu zaidi. Katika suala hili, kuongezeka kwa kile kinachoitwa 'utumwa wa mtandaoni', ambapo watu hushawishiwa katika mipango ya ulaghai na shughuli za uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni na ulaghai wa dawa za kulevya, ni jambo la kusumbua sana."

Kuunganisha watoto na familia kwa watoto wasiosindikizwa

Vatican ilibanisha kwamba "Mitandao ya uhalifu mara nyingi hutumia majukwaa ya mtandaoni na njia zisizojulikana kuajiri, kudhibiti, na kusafirisha waathiriwa wao, ambao mara nyingi ni watoto wadogo."  Kwa njia hiyo, Askofu Balestreo alisema kwamba ujumbe wake unasisitiza  “umuhimu wa kuzuia, kulinda, kukomboa, na kurekebisha tabia. Zaidi ya hayo, kuanzisha njia salama na za kawaida za uhamiaji husaidia kuzuia shughuli za wafanyabiashara haramu. Katika muktadha huu, jukumu la familia ni muhimu, hasa kupitia kuungana tena kwa familia na malezi kwa watoto wasio na wazazi. Katikati ya vita, ugaidi, biashara haramu ya binadamu na uchokozi ulioenea, ni muhimu sana kwamba watoto wapate utamaduni wa maisha, mazungumzo na kuheshimiana.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

 

23 Juni 2026, 10:57