2026.06.28 Askofu Mkuu Richard Gallagher huko Kaunas (Lithuania) 2026.06.28 Askofu Mkuu Richard Gallagher huko Kaunas (Lithuania) 

Ask.Mkuu Gallagher:"Tunaomba amani isiyo na silaha"

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa aliongoza Misa jioni tarehe 27 Juni 2026 katika Kanisa Kuu la Kaunas,Lithuania,katika hafla ya kuadhimisha miaka mia moja ya jimbo la kwanza la Kanisa lililoungana nchini humo.Askofu Mkuu aliwakabidhi watu waliokumbwa na vita chini ya maombezi ya Mama wa Mungu,katika enzi hii "waliojeruhiwa na mzozo mkali katika Ukraine iliyoteswa."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kama vile watu wa Lithuania wakati wa mateso makali ya Kisovieti walivyotembea njia ya kuuawa shahidi, wakijikabidhi kwa Bikira Maria, wakiheshimiwa katika madhabahu yake mengi, vivyo hivyo Kanisa zima liweze kutafuta kimbilio na mwongozo chini ya vazi lake kwa ufahamu ulioongezeka, katika nyakati hizi za mikasa  mikubwa, iliyojeruhi na mzozo mkali katika Ukraine iliyoteswa. Kwa Mama wa Mungu, tunawakabidhi watu walioathiriwa na mzozo huo, tukimwomba maombezi yake ya kimama kwa zawadi ya amani isiyo na silaha na inayopokonya silaha.

Misa nchini Lithuania iliyoongozwa na Askofu Mkuu Gallagher
Misa nchini Lithuania iliyoongozwa na Askofu Mkuu Gallagher

Kwa sala hiyo, Askofu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ya Vatican, alihitimisha mahubiri yake katika Misa aliyoiongoza jioni ya Jumamosi tarehe 27 Juni 2026, katika Kanisa Kuu la Kaunas, Nchini Lithuania, katika hafla ya maadhimisho ya miaka mia moja ya Lituanorum Gente, yaani ya katiba ya kitume ambayo Papa Pio XI alianzisha jimbo la kwanza la Kanisa la Lithuania lililoungana.

Mapadre na watawa wa kike na kiume wangapi ni mashuhuda

Mjumbe maalum wa Papa Leo XIV, aliyeongozwa na masomo ya Dominika ya XIII ya Kipindi cha Kawaida cha Kanisa, alisisitiza umuhimu wa ushuhuda wa watakatifu, wenye uwezo wa kufanya nafasi katika roho zao, kukukuza ndani ya mioyo yao, kuwaweka huru kutokana na maslahi binafsi, wasiwasi, unaokandamiza Neno. Lithuania ilitoa mifano mingi ya mashahidi hawa na mifano ya utakatifu katika karne iliyopita, wakivumilia mateso ya utawala wa kidikteta ambao ulishindwa kuharibu Kanisa. Ni mapadre  wangapi, wanaume na wanawake watawa, pamoja na makumi ya maelfu ya waaminifu, Askofu Mkuu alisema wakati wa mahubiri yake, kuwa walifukuzwa hadi gulags za Siberia! Ni ukurasa mtukufu ulioandikwa na wote katika 'Mambo ya Nyakati ya Kanisa Katoliki nchini Lithuania'!

Askofu Mkuu Gallgher akihutubia Lithuania
Askofu Mkuu Gallgher akihutubia Lithuania

Mateso makali 

Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka historia ya kugusa moyo ya uaminifu kwa Kristo ya Kilima cha Misalaba, kilima ambacho makumi ya maelfu ya misalaba imesimamishwa kwa miaka mingi: kwanza kwa kumbukumbu ya wale waliokufa katika maasi ya Kilithuania ya karne ya 19 dhidi ya Milki ya Urusi, kisha, wakati wa utawala wa Kisovieti, ya mashahidi wa utawala huo. Papa John Paul II, Askofu mkuu alisisitiza, wakati wa ziara yake ya 1993, alipokiita kilima hicho kuwa , "kilichoharibiwa mara kwa mara na matingatinga" ya udikteta wa kikomunisti, na ambayao ni kama  "Kolosseum ya kisasa.” Mwanadiplomasia huyo aliongeza kuwa, “katika miongo kadhaa ya mateso makali." Neno la Mungu halijabaki kuwa nadharia kwa watu wa Lithuania, bali limekuwa mwili katika mwili wa mashahidi wenu!" Akinukuu msemo wa Tertullian kwamba, "damu ya mashahidi ni mbegu ya Wakristo wapya, katika historia ya karne nyingi ya Wakristo wa jumuiya hii uthibitisho unaong'aa zaidi wa ukweli huu wa kihistoria na wa kiroho," Askofu Mkuu Gallagher alibainisha.

Askofu Mkuu Gallagher alipokutana na Mamlaka ya Lithuania
Askofu Mkuu Gallagher alipokutana na Mamlaka ya Lithuania

Shukrani kwa Bwana kwa Kazi kubwa

Historia iliyohifadhiwa na wachungaji wake, kwanza kabisa na Askofu Mwenyeheri Jurgis Matulaitis, ambaye mnamo tarehe 14 Mei 1926, alisoma Katiba ya Kitume ya Pio XI iliyoibua jumuiya ya waamini: mtu wa ajabu, kama Askofu Gallagher alivyomelezea, ambaye kuzaliwa kwake Mbinguni kutashereheka miaka mia moja baadaye mwaka ujao." Katika Misa hiyo Askofu Mkuu alitoa “shukrani kwa Bwana kwa kazi kubwa zilizofanywa katika Kanisa hilo la mashahidi, katika maadhimisho ya miaka mia moja ya Lituanorum Gente, zinaweza kutuimarisha tu katika safari yetu ya kwenda Mbinguni."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

30 Juni 2026, 12:32