Siku kuu ya Vesak. Siku kuu ya Vesak.  (AFP or licensors)

Vatican kwa Vesak 2026:Wabudha na Wakristo wawe wasanii wa amani

Katika ujumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini katika fursa ya Siku kuu ya Vesak kwa 2026,unawaalika Wabudha na Wakristo kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ujenzi wa"amani isiyo na silaha na inayopokonya silaha”yenye mizizi katika huruma,mazungumzo na mabadiliko ya ndani.Vesak ni mojawapo ya siku kuu muhimu zaidi katika kalenda ya Wabuddha,ikiadhimisha kuzaliwa,kuelimika na kupita katika Nirvana ya mwisho ya Siddhartha Gautama,Buddha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kabla ya siku kuu ya Wabuddha ya Vesak kwa mwaka 2026, Baraza la Kipapa kwa ajili ya  Mazungumzo ya Kidini limechapisha ujumbe wake kama kwa kila mwaka kwa Jumuiya za Wabuddha duniani kote, likiwaalika Wakristo na Wabuddha kutembea pamoja katika kuhamasisha kile kinachoelezea kama “amani isiyo na silaha na inayopokonya silaha.” Ujumbe huo, uliosainiwa na Kardinali George Jacob Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Indunil Janakaratne Kodithuwakku Kankanamalage, unaanza na salamu nna pongezi kwa sherehe hiyo muhimu ya Vesak, pamoja na kutafakari kuhusu amani katika wakati unaooneshwa na vita, mgawanyiko, na kutokuaminiana kunakoongezeka.

Mzunguko hatari wa tuhuma na uadui

Katika ujumbe, Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini linasisitiza umuhimu wa desturi hizi. Amani, si tu hamu ya kisiasa au kutokuwepo kwa migogoro ya kivita, bali ni kitu kinachoanzia moyoni mwa mwanadamu. Ukinukuu Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Siku ya Amani Duniani 2026, unabainisha: "Amani ipo; inataka kukaa ndani yetu. Ina nguvu ya upole ya kuelimisha na kupanua uelewa wetu; inapinga na kushinda vurugu." Hata wakati ni dhaifu, ujumbe unaendelea, amani lazima ilindwe "kama mwali mdogo unaotishiwa na dhoruba za chuki na hofu." Katika hali ya vita vinavyoendelea, kuongezeka kwa utaifa wa kikabila na kidini, na kile ambacho Baraza la Kipapa linakiita "udanganyifu wa dini," maandishi hayo yanaonya kwamba ubinadamu una hatari ya kuanguka katika "mzunguko hatari wa tuhuma na uadui." Katika hali kama hiyo, inasema, mila za kidini zina jukumu maalum, sio kuongeza mgawanyiko, bali kuziponya. Ujumbe huo unaongeza kwamba “wema unaondoa kabisa,” unaoweza kuvunja “mzunguko wa tuhuma” na kufungua “njia ambazo hazikuonekana kuwa inawezekana.”

"Mtu yeyote asimdanganye mwingine au kumdharau kiumbe chochote"

Kitu kikuu kati ya maandishi ya Kibuddha yaliyotajwa,  ni mstari wa tano wa Dhammapada, mojawapo ya makusanyo yaliyosomwa sana ya misemo ya Buddha. Sehemu ya Kanuni ya Pali, maandiko ya msingi ya Ubuddha wa Theravāda, Dhammapada inakusanya mafundisho mafupi kuhusu hekima, maadili, na njia ya ukombozi. Mstari ulionukuliwa na Baraza la Kipapa unasomeka kuwa: “Chuki hairidhishwi kamwe na chuki; chuki huridhishwa na kutochukia pekee.” Kifungu hiki kinaonesha mada inayojirudia ndani ya mafundisho ya Kibuddha: kwamba hasira huendeleza mateso, huku huruma na nidhamu ya ndani vikiweza kuvunja mzunguko wake. Ujumbe huo pia unataja Metta Sutta, mojawapo ya mijadala inayojulikana zaidi katika tamaduni ya Kibuddha na maandishi ya msingi kuhusu wema. Neno "metta" linamaanisha aina ya ukarimu wa ulimwengu wote, upendo usio na ubinafsi unaotolewa kwa viumbe vyote hai bila ubaguzi. “Mtu yeyote asimdanganye mwingine au kumdharau kiumbe chochote,” maandishi yanasema.

"Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa"

“Mtu yeyote kwa hasira au kwa uovu asimtakie mwingine madhara.” Ikiwa inasomwa kijadi katika monasteri na nyumba, Metta Sutta ina nafasi muhimu katika sala na tafakari ya Kibuddha. Inawataka waumini kukuza huruma hata kwa wale ambao wanaweza kuonekana kama maadui. Ujumbe wa Baraza la Kipapa kisha unaweka mafundisho haya pamoja na maneno ya Kristo katika Injili ya Mathayo: “Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa,” na “Heri wapatanishi,” ikisisitiza kile inachokiona kama muunganiko wa kina wa kiroho kati ya Ubuddha na Ukristo. “Mila zote mbili hukutana,” ujumbe unasema, “katika kuelekeza kwenye amani inayoishi ile inayoondoa silaha mioyo kabla ya kuondoa silaha mikononi.” Badala ya kuelewa amani kama kitu kinachowekwa nje tu, ujumbe unaelekeza kwenye mabadiliko ya ndani yanayoweza kuijenga upya jamii yenyewe.

Kila Jumuiya ya kidini inapaswa kukutana 

Ujumbe unaendelea kusisitiza kwamba,  amani kama hiyo inahitaji zaidi ya ishara za ishara au lugha ya kidiplomasia. Inasema viongozi wa kidini, wanaitwa kuwa washirika halisi katika mazungumzo na mawakala wa kweli wa upatanisho, huku waamini wenyewe wakialikwa kuwa wasanii wa amani. Wito huu unachukua umuhimu maalum katika enzi ambapo dini wakati mwingine hutumiwa kuhalalisha kutengwa au vurugu. Baraza la Kipapa linaonya dhidi ya ukimya na kutojali, huku likihimiza jamii kutoshiriki katika hofu. Badala yake, kila jumuiya ya kidini inapaswa kuwa mahali "ambapo uadui hushindwa kupitia kukutana, ambapo haki hutekelezwa, na ambapo msamaha huthaminiwa."

Ukimya,tafakari,uvumilivu na matendo ya kila siku ya wema wa amani

Ujumbe unahitimisha kwa kusisitiza kipimo cha ndani cha amani. Kwa kurudia desturi ya kutafakari ya Kibuddha na desturi ya Kikristo ya sala, unaelekeza ukimya, tafakari, uvumilivu, na matendo ya kila siku ya wema kama misingi ambayo amani hujengwa juu yake. Baraza la Kipapa linasema kwamba amani hulelewa si tu katika mazungumzo ya kimataifa au matamko ya umma bali pia katika mahusiano ya kawaida ya kibinadamu—katika kukataa kulipiza kisasi, katika ujasiri wa kusamehe, na katika uamuzi wa kutumaini hata wakati upatanisho unapoonekana kuwa mgumu. "Amani si ndoto au wazo la mbali," ujumbe unasema. "Ni uwezekano halisi ambao tayari umewekwa karibu nasi, unaosubiri kukaribishwa na kushirikishwa.” Kuhitimisha ujumbe huo, Baraza la Kipapa la Mazungumzo  ya Kidini linarejesha matumaini yake kwamba Wabudha na Wakristo wanaweza kuwa pamoja "mashahidi wa amani hii inayoondoa silaha" - amani inayoweza kuponya majeraha, kurejesha mahusiano yaliyovunjika, na kufungua upeo mpya kwa wanadamu.

Sherehe ya Vesak:kutafakari,matendo ya hurumana kupyaisha mafundisho ya Buddha

Siku Kuu ya Vesak ni mojawapo ya sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya Wabuddha. Inaadhimisha kuzaliwa, kuelimika, na kupita katika Nirvana ya mwisho ya Siddhartha Gautama, Buddha. Husherehekewa katika mila na tamaduni  zote za Kibuddha, kuanzia jamii za Theravada huko Sri Lanka na Asia ya Kusini-mashariki hadi tamaduni za Mahayana na Vajrayana barani  Asia yote Mashariki na Himalaya na kwa hakika ni wakati wa maombi, tafakari, matendo ya huruma, na kujitolea upya kwa mafundisho ya Buddha. Ingawa tamaduni za  Kibuddha zinaweza kukaribia kuelimika na nirvana kupitia mitazamo tofauti ya kitaalimungu, Vesak inabaki kuwa kumbukumbu ya pamoja ya maisha ya Buddha, kupyaishwa, na urithi wa kiroho unaodumu. Inapozingatiwa kulingana na kalenda za mwezi, sherehe za Vesak hutofautiana kutoka nchi hadi nchi. Katika sehemu nyingi, siku kuu yenyewe hudumu kwa siku moja, ingawa sherehe na vipindi vya maombi mara nyingi hudumu kwa siku kadhaa, hasa katika monasteri na mahekalu.

UJUMBE KWA VISAK 2026

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

11 Mei 2026, 16:20