Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 4 Mei 2026 alikutana na kuzungumza na Rais Halla Tómasdóttir, wa Jamhuri ya Watu wa Iceland. Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 4 Mei 2026 alikutana na kuzungumza na Rais Halla Tómasdóttir, wa Jamhuri ya Watu wa Iceland.  (ANSA)

Rais Halla Tómasdóttir wa Jamhuri ya Watu wa Iceland Akutana na Papa Leo XIV

Viongozi wameonesha kuridhika kwa uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili. Wamekazia kuhusu mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi; malezi na makuzi ya vijana wa kizazi kipya. Baadaye, Papa Leo XIV na mgeni wake walijikita zaidi katika masuala ya Kikanda na Kimataifa mintarafu vita inayoendelea sehemu mbalimbali za dunia na kwamba, kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujikita katika majadiliano katika ukweli na uwazi

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 4 Mei 2026 alikutana na kuzungumza na Rais Halla Tómasdóttir, wa Jamhuri ya Watu wa Iceland, ambaye pia alibahatika kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa.

Papa Leo XIV amekutana na Rais wa Iceland na Ujumbe wake
Papa Leo XIV amekutana na Rais wa Iceland na Ujumbe wake   (ANSA)

Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wameonesha kuridhika kwa ona uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili. Wamekazia zaidi kuhusu mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi; malezi na makuzi ya vijana wa kizazi kipya. Baadaye Baba Mtakatifu Leo XIV na mgeni wake walijikita zaidi katika masuala ya Kikanda na Kimataifa mintarafu vita inayoendelea sehemu mbalimbali za dunia na kwamba, kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujikita katika majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi kwa ajili ya mustakabali wa amani duniani.

Diplomasia Vatican
05 Mei 2026, 15:03