Katika Basilika ya Maria Mkuu(Santa Maria Maggiore),sala ya kila siku ya Rozari mwezi wa Mei hadi 31. Katika Basilika ya Maria Mkuu(Santa Maria Maggiore),sala ya kila siku ya Rozari mwezi wa Mei hadi 31. 

Mtakatifu Maria Mkuu:Kusali Rozari katika“Mwezi wa Maria”

Katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu,kuanzia tarehe Mosi Mei,watasali kila siku Rosari Takatifu na kufanya baadhi maadhimisho ya misa hadi Mei 31,wakati Kardinali Reina atakapoongoza tendo la Kuwekwa wakfu kwa Mama Yetu.

Vatican News

Katika mwezi Mei, uliowekwa wakfu kwa ajili ya Mama Yetu Maria, Kanisa Kuu la Kipapa la ‘Santa Maria Maggiore,’ Mtakatifu Maria Mkuu,- limezindua mfululizo wa mipango kwa ajili ya  mwezi huu wa Bikira Maria. Kwa njia hiyo ni, "Mwezi wa Maria" unaoanz kwa kusali Rozari Mei Mosi usiku saa 3.00 katika Uwanja wa Kanisa Kuu, ikiongozwa na Askofu Mkuu Luis Manuel Herrera, Mkuu wa Kanisa hilo.. Sala ya Maria, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, itaongozwa na Jumuiya tofauti za Parokia, Watawa, na  wahusika wa kielimu kama ilivyo kwa kila mwaka. Pia itawezekana kushiriki katika sala ya Rozari kila siku, kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi, saa 5:30 asubuhi,  katika Kikanisa cha Msalaba na saa 1:00 jioni katika Kikanisa cha Paulo. Hata hivyo, siku za Dominika sala hiyo itafanyika mapema saa 10.15 jioni ambayo itafutiwa na nyimbo za Masifu ya Pili ya Jioni.

Sifa kwa Maria

Wakati huo Jumanne, tarehe 19 Mei 2026,  saa 1:00 jioni, kutakuwa na mafundisho ya II ya Mama Maria ambayo yameandaliwa kwa ushirikiano na Kikundi cha "Mkutano wa Mataifa," kwa kuongozwa na mada: "Wimbo wa Maria." Jumatatu, Mei 25, saa 1:30 asubuhi  kutakuwa na Maadhiisho ya Misa katika kikanisa cha chini kinachotunza Masalia ya Kitanda Kitakatifu ambacho Mama Maria alimlaza Mtoto Yesu kwenye hori la Ng’ombe.

Mnamo Mei 30, saa 3:00 usiku kutakuwa na sala na kuimba pamoja (Akathistos,) wimbo wa sifa kwa Mama wa Mungu ulioanzia karne ya 5. Wimbo huu unaundwa na beti 24, idadi sawa ya herufi kama alfabeti ya Kigiriki. Beti 12 za kwanza zinasimulia fumbo la Umwilisho kwa kutumia watu wengi wa kishairi; zingine 12 zinarejea ushiriki wa Maria, Mama wa Mungu (Theotokos), katika ukombozi wa wanadamu kupitia mafumbo ya Kristo.

Katika mwezi mzima, mpangilio wa maua unaoonesha Maandishi (monogramu) ya Maria (Ave Maria) utaoneshwa kwenye ngazi za Uwanja wa Esquilino, na utaendelea kuonekana hadi Maadhimisho ya Siku ya (Corpus Christi) yaani Mwili na Damu ya Yesu, tarehe 6 Juni 2026. Hatimaye, saa 3:00 usiku, baada ya sala ya Rozari, kutakuwa na tendo la kuwekwa wakfu kwa Mama Yetu ambako  Kardinali Baldassare Reina, Makamu wa Jimbo Kuu la Roma ataongoza.

KUSALI ROZARI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

01 Mei 2026, 11:02