Kard.Parolin:Afya ya akili ya vijana ni dharura inayohitaji majibu ya kimuundo!
Vatican News
Akielezea mgogoro wa afya ya akili unaowaathiri vijana kama "dharura inayohitaji majibu ya kimuundo," Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican alionya kwamba jamii ya leo mara nyingi huwapa vijana "kila njia lakini hakuna kusudi." Alizungumza hayo katika Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili ya tarehe 29-30 Mei 2026 wenye mada:" Ramani za Matumaini kwa Ajenda ya Elimu ya Kikanda: Afya ya Akili, Teknolojia za Kidijitali na Elimu," uliofanyika katika Jengo la Casina Pio IV ndani ya Bustani za Vatican pamoja na mawaziri wa elimu, wasomi na wataalamu wa kimataifa. Kardinali Parolin alisema elimu inasalia kuwa "nguzo ya maendeleo fungamani ya binadamu, kuishi pamoja kwa amani na haki ya kijamii." Hata hivyo, alibainisha kuwa mifumo ya elimu leo hii inakabiliwa na changamoto mpya za ubora, ikiwa ni pamoja na malezi fungamani ya mtu, maendeleo ya kijamii na kihisia, ulinzi wa walio hatarini na ujumuishaji wa uwajibikaji wa teknolojia za kidijitali.
Mkataba wa Kimataifa kuhusu Elimu
Kardinali Parolin alisisitiza kwamba changamoto hizi haziwezi kushughulikiwa kupitia hatua zilizogawanyika, lakini zinahitaji "ushirikiano wa muundo, wa pande nyingi na wa muda mrefu." Akikumbuka Mkataba wa Kimataifa kuhusu Elimu uliozinduliwa na Papa Francisko mnamo 2019, alielekeza kwenye mkataba wa hivi karibuni wa Papa Leo XIV, Apostolic Letter kuhusu elimu, ambayo inahitaji "kundi la elimu" la kimataifa lenye uwezo wa kuhamasisha udugu, amani na haki. Alibainisha vipaumbele vitatu vilivyoakisiwa na Papa Leo XIV: utunzaji wa maisha ya ndani, "utamaduni wa kidijitali unaozingatia binadamu," na elimu ya amani. Akizingatia afya ya akili, Kardinali Parolin alisema takwimu kuhusu vijana "ni ya ufasaha na, kwa njia nyingi, ya kutisha," hasa kufuatia janga hili, ambalo limeshuhudia viwango vinavyoongezeka vya wasiwasi, mfadhaiko na dhiki ya kisaikolojia miongoni mwa vijana na watu wazima.
Umoja usiotenganishwa wa mwili, akili na roho
Katibu Mkuu wa Vatican kwa hiyo alionya dhidi ya kupunguza suala hilo kuwa tatizo la kimatibabu pekee linalopewa mifumo ya huduma za afya. "Kanisa limefundisha kila mara kwamba mwanadamu ni umoja usiotenganishwa wa mwili, akili na roho," alisema, akiongeza kwamba mfumo wa kielimu unaopuuza yoyote kati ya vipimo hivi "haujakamilika" na hauwezi kujibu mahitaji kamili ya binadamu. Badala yake, alisema elimu lazima iwape vijana sio tu maarifa na ujuzi, bali pia zana za kujielewa, kudhibiti hisia, kujenga mahusiano yenye maana na kugundua kusudi maishani. Aliunganisha maono haya na uelewa wa utamaduni wa Kikristo kuhusu "utunzaji wa roho," ambao sasa mara nyingi huonyeshwa kupitia lugha ya uwezo wa kijamii na kihisia na ustawi wa kisaikolojia.
Jukumu la shule na familia na Teknolojia za kidijitali
Kardinali Parolin alisisitiza jukumu muhimu la shule na familia. Shule, alisema, zinapaswa kuwa mahali ambapo kila mwanafunzi anahisi "kuonekana, kusikilizwa na kusindikizwa," huku familia zikibaki kuwa kinga kali zaidi kwa watoto na vijana zinapoungwa mkono ipasavyo. Akigeukia teknolojia za kidijitali, alitambua uwezo wao mkubwa wa kielimu, haswa katika kupunguza ukosefu wa usawa katika maeneo makubwa na tofauti kama vile Ibero-Amerika. Wakati huo huo, alionya kwamba kuathiriwa kupita kiasi na mazingira ya kidijitali bila mwongozo wa kutosha wa kielimu kunaweza kuathiri vibaya afya ya akili ya vijana kupitia kugawanyika kwa umakini, utegemezi wa skrini, unyanyasaji wa mtandaoni, kutengwa kijamii na kuathiriwa na maudhui yenye madhara. "Changamoto si kukubali au kukataa teknolojia, bali kuzitawala," alisema, akitoa wito wa elimu ya kidijitali inayounganisha uwezo wa kiufundi na malezi ya kijamii na kihisia.
"Mgogoro wa maana"
Katikati ya mgogoro huo, Kardinali Parolin alisema, kuna "mgogoro mkubwa wa maana."Alisema vijana wengi, wanahisi wamechanganyikiwa si kwa sababu hawana taarifa au fursa, bali kwa sababu hawana "upeo wa maana" wa kuelewa maisha na matumaini yao. "Jamii inayowapa vijana kila njia lakini hakuna kusudi; kila muunganisho lakini hakuna uhusiano halisi; kila jibu lakini hakuna swali la kina, ni jamii ambayo hatimaye inawaacha," alisema. Kardinali alihitimisha kwa kuzihimiza serikali kutambua afya ya akili ya vijana kama kipaumbele kinachohitaji uwekezaji ulioratibiwa katika elimu, huduma za afya, malezi ya walimu na usaidizi wa familia. Akirudia wito uliozinduliwa na Papa Leo XIV kwa walimu wa dini katika Waraka wa kitume ili wawe "waandishi wa dansi wa matumaini,"alisema elimu lazima iwasaidie vijana kupata zana na upeo unaohitajika kuishi "maisha kamili, huru na yenye maana."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.