Kard.Parolin:Mungu anasikia Maombi Yetu kwa ajili ya Haiti
Edoardo Giribaldi na Angella Rwezaula – Vatican
Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, alitoa wito wa kukomeshwa kwa vurugu nchini Haiti wakati wa Misa iliyoadhimishwa alasiri tarehe 9 Mei 2026 katika Kikanisa cha Sforza cha Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu, jijini Roma ambapo sauti yake katika mahubiri alisisitiza kuwa “Amani itawale milele nchini Haiti. Hili ni tumaini lililoinuliwa dhidi ya kutojali mateso ya watu wa Caribbiean na wengine wengi ambapo vitendo vya kibinafsi na visivyo vya kibinadamu vinaharibu jamii nzima.” Katika misa iliyoudhuliwa na Mapadre, watawa, Mabalozi wa nchi hiyo kwa Italia na Kiti Kitakatifu, na waamini wengine kutoka nchini Haiti, miongoni mwa wengine kulikuwa pia na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Alix Didier Fils-Aimé, ambaye hata hivyo alipokelewa katika mkutano asubuhi hiyo na Papa Leo XIV, mjini Vatican
Zawadi ya Kwanza ya Aliyefufuka ni Amani
Kardinali Parolin alisisitiza katika mahubiri yake, aliyotoa kwa lugha ya Kifaransa kuwa: kuna haja ya amani ambayo "sio kama ile ambayo ulimwengu unatupatia mara nyingi huwekwa kupitia vurugu na udanganyifu." Upatanisho ulioitishwa na Kardinali ulikuwa ni ule unaotamaniwa na Yesu, ambao "alijiwasilisha mbele ya jumuiya ya Kanisa baada ya Ufufuko wake," akiongoza hatua za kwanza za jumuiya ya wamini. Kwa hivyo, hii ndiyo zawadi ya kwanza ya Aliyefufuka na ishara ya uwepo wake." Kwa kuikaribisha Kardinali Parolin alielezea, inahusisha dhamira ya kujenga ushirika. "Pale Kristo alipo, amani hutawala." Upatanisho ambao, hata hivyo, "hauwezi kuwekwa," lakini umependekezwa na kukubaliwa kwa uhuru na kila mtu.
Hitaji la dunia la amani
Kwa hivyo, amani si tu kutokuwepo kwa migogoro, bali ina mizizi katika kukubalika kwa Kristo na katika hadhi ya mwanadamu," hivyo akizungumza pia na wasioamini. "Kwa kuzingatia hali ya sasa ya Kimataifa," Kardinali Parolin alisema, "sote tunaweza kutambua jinsi ulimwengu wetu unavyohitaji uwepo wa Mungu na, kwa hivyo, zawadi ya amani."
Mungu Anasikia Maombi Yetu
Katika kukabiliana na mikasa mingi, Kardinali Parolin alitoa uhakikisho: "Mungu anasikia kilio cha waathiriwa wote wa dhuluma na umaskini ambao, ulimwenguni kote, wanamtolea maombi yao." Kwa hivyo, matarajio ya wale walioko Haiti wanaotamani "kuishi pamoja bila vurugu, ambapo wanaweza kuishi kama kaka na dada," hayawezi kukosa kusikilizwa.
Ahadi Muhimu ya Jumuiya ya Kimataifa
Kardinali alindelea kusema kwamba Kipindi cha Pasaka kinatualika kueneza uwepo wa Kristo, tukiwapa sauti wale wanaoteseka kimya kimya na kuwashirikisha wote tunaokutana nao njiani, "bila ubaguzi," ili "ulimwengu uweze kumwamini Mungu anayetoa amani." Dhamira pana sana hivi kwamba inahitaji kujitolea kwa jumuiya ya kimataifa kwa manufaa ya wote, zaidi ya "mipaka, mila desturi za kidini, na tamaduni," kupitia "ushirikiano wa kimfumo wa taaluma mbalimbali, kuunganisha taasisi, mashirika ya kisayansi, na viongozi kutoka nyanja tofauti." Ahadi muhimu kwa sababu, Parolin aliongeza, "sisi sote ni kaka na dada wanaowajibika kwa kila mmoja."
Kuhakikisha haki kwa kuheshimu sheria
Kwa hivyo, kila mtu anaitwa kuchukua majukumu yake, akijitolea kurejesha maelewano na kufanya kazi kwa ajili ya haki "kwa kuheshimu sheria na haki za binadamu," akilenga "kwa manufaa ya taifa kupitia ujenzi mpya wa taasisi na utekelezaji wa njia zote zinazowahakikishia raia maisha yenye heshima."
Amani katika siku zijazo
Katibu Mkuu wa Vatican kisha alikumbuka maneno ya Papa Leo XIV wakati wa ziara yake kwa Maqam Echahid, kwenye Ukumbusho wa Mashahidi wa Algeria, na wakati wa safari yake ya mwisho ya Kitume, ambayo kulingana na "Mungu anataka amani kwa kila nchi," na hii inaweza kupatikana tu kupitia msamaha. "Mapambano ya kweli ya ukombozi yatapatikana tu wakati amani ya moyo itapatikana," Kardinali Parolin alirudia. "Mustakabali ni wa wanaume na wanawake wa amani."
Sala kwa wale wanaobaki katika huduma
Kardinali alihitimisha mahubiri yake kwa kuwakabidhi Maria wale walio Haiti "wanaotoa bora yao katika huduma kwa wanyonge," ambapo "vurugu huonyesha sura yake mbaya zaidi." Kardinali pia aliwakumbuka maaskofu, mapadre, na watawa wanaoendelea na utume wao wa kichungaji nchini, "pamoja na wanaume na wanawake wengi wenye mapenzi mema ambao, katika majukumu yao mbalimbali, wameelewa kwamba kumfuata Mfufuka kunamaanisha kufanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya amani, mara nyingi wakijisahau."
Mgogoro nchini Haiti
Ikumbukwe tangu 2021, Haiti imekabiliwa na mgogoro ambao haujawahi kutokea unaohusishwa na vurugu za magenge. Watu milioni 1.4 wamehamishwa na makundi yenye silaha ambayo yamekuwa yakiiharibu nchi kwa miaka mingi. Kulingana na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, mwaka wa 2025 pekee, zaidi ya watu 5,500 waliuawa na zaidi ya 2,600 kujeruhiwa.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.