Jengo la Taasisi ya Kazi za Dini(IOR). Jengo la Taasisi ya Kazi za Dini(IOR).  (AFP or licensors)

IOR yachapisha taarifa za fedha za 2025:faida ya €51 milioni,€24.3 milioni kama gawio kwa Papa

Taasisi ya Kazi za Dini imechapisha toleo la kumi na nne la Ripoti yake ya Mwaka yenye taarifa za fedha za mwaka 2025.Tume ya Makardinali imeidhinisha usambazaji wa gawio la €24.3 milioni kwa Papa,ongezeko la 76.1% ikilinganishwa na 2024.

Vatican News

Taasisi ya Kazi za Dini (IOR)ilichapisha Ripoti yake ya Mwaka ya 2025, Jumatatu, tarehe 11 Mei 2026. Taarifa za kifedha za IOR kwa mwaka wa fedha ulioishia Desemba 31, 2025 ziliandaliwa kwa mujibu wa viwango vya IAS-IFRS, pamoja na ufichuzi unaolingana na Nguzo ya Tatu ya mfumo wa Basel. Kulingana na ripoti hiyo, IOR ilirekodi mapato halisi ya Euro  51 milioni kwa mwaka 2025,  ikiwa na ongezeko la 55.5% ikilinganishwa na mwaka 2024 na matokeo ya juu zaidi katika miaka kumi iliyopita.

Taasisi ilisema matokeo hayo yalisaidiwa na utendaji bora wa uendeshaji, usimamizi hai na nidhamu wa kwingineko, hali nzuri ya soko, na ongezeko la kiasi cha mali za wateja. Jumla ya mali za wateja ilifikia euro bilioni 5.9, ikilinganishwa na euro bilioni 5.7 mwaka 2024. IOR pia iliripoti kiwango cha riba cha euro milioni 32.3, kutoka euro milioni 29.4 mwaka 2024, huku kiwango cha kamisheni kikiwa euro milioni 26.2, kwa ujumla sambamba na mwaka uliopita. Kiwango cha kati kiliongezeka hadi euro milioni 66.3, ikilinganishwa na euro milioni 51.5 mwaka 2024.

Mahitaji ya mtaji wa Taasisi

Uwiano wake  wa Tier 1 wa Taasisi, kipimo muhimu cha nguvu kuu ya mtaji wa Taasisi ya kifedha ikilinganishwa na mali zake zinazopimwa hatari, uliongezeka hadi 71.9%, huku mali halisi ikiongezeka kwa Euro Milioni 83.4 milioni hadi Euro Milioni 815.3 milioni. Ripoti inasema kwamba msimamo wa mtaji na riba za IOR unaonesha mbinu ya busara inayolenga kuwalinda wateja na kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu. Kwa kuzingatia matokeo ya 2025 na mahitaji ya mtaji wa Taasisi, Tume ya Makardinali iliidhinisha usambazaji wa gawio la €24.3 milioni kwa Baba Mtakatifu, ongezeko la 76.1% ikilinganishwa na 2024, kwa kuzingatia dhamira ya IOR ya kusaidia kazi za kidini na hisani.

Ripoti pia inabainisha kuwa mikakati yote ya usimamizi wa kwingineko ya IOR ilirekodi faida chanya na kwamba Taasisi inaendelea kukuza uwekezaji unaoendana na kanuni za imani ya Katoliki na Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa. IOR ilisema uhusiano wake na makutaniko ya kidini uliimarishwa zaidi wakati wa 2025, huku idadi ya Makutaniko yanayohudumiwa na yale yanayokabidhi mali kupitia mamlaka ya usimamizi wa mali ikiongezeka. Taarifa za fedha zilipokea maoni safi ya ukaguzi kutoka Deloitte & Touche na ziliidhinishwa kwa kauli moja na Bodi ya Usimamizi mnamo tarehe 28 Aprili 2026, kabla ya kupelekwa kwa Tume ya Makardinali kama inavyotakiwa na Sheria.

Vigezo vya uwekezaji wa Kikatoliki Duniani

Mnamo Februari 2026, Taasisi pia ilizindua fahirisi mbili mpya za hisa kwa ushirikiano na Morningstar, iliyoundwa kama vigezo vya uwekezaji wa Kikatoliki duniani kote. Fahirisi ya Morningstar IOR US Catholic Principles GR USD (ticker: MIORUCPG), na fahirisi ya Morningstar IOR Eurozone Catholic Principles GR EUR (ticker: MIORECPG), huwapa wawekezaji njia ya kupata faida ya kimaadili kwenye mtaji uliowekezwa. Kwa idhini ya taarifa za fedha za 2025, Jean-Baptiste de Franssu alihitimisha muhula wake kama Rais wa IOR. Taasisi ilitoa shukrani kwa huduma yake, uongozi, na kujitolea. François Pauly amechukua wadhifa kama Rais mpya.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

12 Mei 2026, 11:04