Papa akiwasalimia wanandoa wapya katika moja ya Katekesi ya mwanzoni mwa Aprili 2026. Papa akiwasalimia wanandoa wapya katika moja ya Katekesi ya mwanzoni mwa Aprili 2026.  (@VATICAN MEDIA)

Vatican:Siku ya Mafunzo:Sakramenti ya Ndoa,imani na munus docendi!

Uhusiano kati ya sakramenti ya ndoa,imani na munus docendi,kwa kuzingatia hasa malezi ya mapadre katika kuwasindikiza vijana,wanandoa,wachumba katika imani yao.Hii ndiyo mada kuu ya siku ya mafunzo itakayofanyika huko Casina Pio IV,Vatican,tarehe 28 Aprili 2026 iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha.

Na Angella Rwezaula–Vatican.

Baraza la Kipapa la Walei, Familia, na Maisha, tarehe 28 Aprili 2026, mjini Vatican limeandaa siku ya mafunzo kuhusu: "Sakramenti ya Ndoa, Imani, na Munus Docendi,"yaani kufundisha, ‘munus’ kwa kilatini, maana yake zawadi, kazi, uwajibikaji, kwa njia hiyo maneno hayo yanawakilisha kazi ya kufundisha neno la Mungu, na msingi wa utume wa kikuhani. Yanajumuisha kuhubiri, katekesi, na kushuhudia imani, kulingana na Maandiko na mafundisho.) Programu hiyo itajumuisha utangulizi kuanzia saa 2:30 asubuhi utakaotolewa na Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Baadaye itafuata mawasilisho mawili yatakayotolewa na Padre Andrea Bozzolo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesian, na Padre Fabio Rosini, msomi wa Biblia na Profesa wa Homiletiki na Taalimungu  ya Kichungaji katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu.

Mabadiliko makubwa ya kiutamaduni

Mkutano huo utamalizika saa 7:30 mchana, baada ya kipindi cha mazungumzo na majadiliano. Takriban wawakilishi 75 kutoka katika mabaraza mbalimbali ya Curia Romana na ulimwengu wa waseminari na malezi watashiriki katika mkutano huo kwa mwaliko wa: Gambera wa Seminari mbali mbali, maprofesa, na wale wote wanaoshiriki jukumu la kuwafunza wachungaji wa siku zijazo na kuunga mkono Kanisa katika utume wake wa kielimu. Mpango huu unatokana na ufahamu kwamba uhusiano kati ya ndoa, imani, na tangazo la Kanisa unawakilisha suala muhimu sana la kichungaji na la malezi leo hii. Katika kipindi hiki ambacho kimetawaliwa na mabadiliko makubwa ya kiutamaduni, siku hii italenga kutoa fursa ya kutafakari jinsi ya kusindikizana na vijana, wachumba, wanandoa, na waliooa hivi karibuni, na, wakati huo huo, jinsi ya kuwafunza wahudumu na watendaji wa kichungaji wenye uwezo wa kusaidia safari hii kwa ufahamu na uwezo mkubwa.

Maisha halisi ya familia, vijana na utamaduni

Katikati ya semina hii ni malezi ya mapadre. Mada ya ndoa ya Kikristo, kiukweli, haihusishi tu huduma ya familia kwa maana halisi, lakini kwa kuwaalika kutambua jinsi ambayo mapadre wa siku zijazo wanavyojiandaa kuelewa, kutangaza, na kusindikiza na wito wa ndoa katika nyanja zake za kibinadamu, kiroho, na kichungaji. Katika miktadha mingi ya kikanisa, kuna hitaji linaloonekana la malezi yasiyo ya kufikirika, yale yenye uwezo zaidi wa kushiriki katika maisha halisi ya familia, maswali ya vijana, na mabadiliko ya utamaduni wa hisia. Siku hiyo pia inaangukia ndani ya mfumo wa maadhimisho ya miaka kumi ya Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia, ambao unaadhimishwa 2026.

Wito wa ndoa hauwezi kuchukuliwa kama jambo la pembeni

Katika ujumbe wake wa tarehe 19 Machi 2026, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka kumi ya Wosia, Papa Leo XIV alikumbuka kwamba, kupitia sakramenti ya ndoa, wanandoa huunda "Kanisa la nyumbani" na kwamba jukumu lao ni muhimu kwa elimu na uenezaji wa imani.” Papa Leo XIV aidha alirudia mwaliko wake wa kuimarisha kujitolea kwa Kanisa katika eneo hilo, ili wale walioitwa kwenye ndoa waweze kuishi upendo wao wa ndoa katika Kristo na vijana waweze kugundua upya kina cha wito huu. Kutokana na hali hii, semina inalenga kuakisi imani inayoongezeka kwa pamoja katika maisha ya Kanisa: Wito wa Ndoa hauwezi kuchukuliwa kama suala la pili  katika maandalizi ya wachungaji wa siku sijazo. "Maisha ya kihisia na ya kifamilia kwa kiasi kikubwa huamua uwezekano wa kutangaza, kukomaa kwa imani, na uwezo wa jumuiya ya Kikristo kusindikiza vizazi vya siku zijazo."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

24 Aprili 2026, 09:55