Vatican:Maendeleo lazima yahakikishe upatikanaji endelevu wa chakula
Vatican News
Eneo la Asia-Pasifiki ni nyumbani kwa baadhi ya uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani, lakini wakulima wadogo wa eneo hilo wanakabiliwa na changamoto nyingi: kuanzia ukuaji wa idadi ya watu na ukuaji wa miji hadi upotevu wa bayoanuwai na udhaifu wa mabadiliko ya tabianchi. Haya yalisemwa na Askofu Mkuu Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwa FAO, IFAD, na WFP, katika hotuba yake katika Mkutano wa XXXVIII wa Kikanda wa Asia-Pasifiki unaoendelea huko Bandar Seri Begawan, mji mkuu wa Brunei ulioanza tangu tangu Aprili 20 na utahitimishwa tarehe 24 Aprili 2026.
Mabadiliko ya dhana
"Kwa sababu hiyo, Askofu Mkuu Chica Arellano alibainisha, "mabadiliko ya dhana yanayotegemea utu wa kibinadamu usioweza kuondolewa kutoka kwa Mungu ni muhimu, ili uvumbuzi na maendeleo yasaidie kuhakikisha kwamba kila mtu, hasa maskini na walio katika mazingira magumu zaidi, wakiwemo watoto wachanga, wanapata chakula chenye afya, lishe, na cha kutosha kwa njia endelevu." "Katika sekta ya kilimo," Mwakilishi wa Kudumu alisisitiza “hii inahusisha kuanzishwa kwa teknolojia za kisasa, kupitishwa kwa mazoea endelevu, na maendeleo ya mikakati inayoboresha matumizi ya maliasili katika mnyororo mzima wa uzalishaji. Hata hivyo, uvumbuzi hauzuiliwi tu katika matumizi ya teknolojia mpya; pia unahusisha mabadiliko ya jinsi tunavyozalisha, kusambaza, na kula chakula.
Kuhamasisha Utu wa Binadamu
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Chica Arellano alihakikishia kuwa, Vatican "itaendelea kuunga mkono na kuhimiza maendeleo ya kiteknolojia. Lakini kwa upande mwingine, "ni muhimu kukuza sayansi kwa ajili ya manufaa ya wote, ili uvumbuzi ufaidishe walio hatarini zaidi na kulinda mazingira." Alihitimisha akinukuu kifungu kutoka ujumbe wa Papa Leo XIV wa Siku ya 60 ya Mawasiliano Duniani kuwa “Changamoto halisi ya uvumbuzi, inajumuisha kuiongoza na kuielekeza kuelekea kuishi pamoja kati ya ubinadamu na mazingira ambayo huweka heshima ya binadamu kwanza."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.