"Todos, todos, todos!"

Simulizi katika picha za Papa Francisko,mwaka mmoja baada ya kifo chake.Kwa hiyo zaidi ya kumbukumbu hai ni mtazamo ambao hata baada ya kifo chake unaendelea kuhoji hali ya sasa ya Kanisa na Ulimwengu wote.

Vatican News

"Tumehurumiwa; na tuwe na huruma." Ni maneno machache yanayogusa roho ya Papa na historia ya Baba Mtakatifu pamoja na hayo "jinsi gani ningependa Kanisa ambalo ni maskini na kwa ajili ya maskini," alitamka mwanzoni mwa huduma yake.  Kwa hiyo, mwaka mmoja baada ya kifo cha Papa Francisko, Vatican News – Radio  Vatican na Osservatore Romano wanakumbuka matukio yake muhimu zaidi katika makala ya dakika 27 yenye kichwa: “Todos, todos, todos”, kuanzia ishara nyingine ya Papa ya ukaribu na pembezoni, wito wake usiokoma wa amani katika ulimwengu uliogawanyika na vita vya dunia vilivyogawanyika vipande vipande.

"Todos, todos, todos!," ambayo itapatikana kwenye majukwaa ya vyombo vya habari vya Vatican yenye manukuu katika Kiitaliano, Kihispania, Kiingereza, na Kiarabu, kwa hivyo ndiyo mada kuu ya simulizi inayoonesha kiini cha uchungaji cha upapa wa Bergoglio. Kupitia picha za kumbukumbu na mfuatano wa ishara, video inaonesha Kanisa linaloendelea mbele, lenye uwezo wa kufanya mazungumzo na uwepo katikati ya majeraha ya historia.

Kuanzia kiini cha huruma hadi ujenzi wa mahusiano ya moja kwa moja, miaka ya Papa Francisko kama Papa inajitokeza kama uzoefu wa kikanisa uliotafsiri Injili katika ishara halisi na zinazoeleweka kwa wote.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 09:05