Alama maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Papa Francisko
Ofisi ya Posta ya Vatican imetoa alama maalum ya kumbukizi ya mwaka wa kwanza wa kifo cha Papa Francisko,kilichotokea tarehe 21 Aprili 2025.
Vatican News
Uso wa Papa Francisko, uliochochewa na picha, unaonekana kwenye alama maalum ya Posta kwa kumbukuizi ya mwaka baada ya kifo chake(Dies Natalis,)kilichotekea tarehe 21 April 2025.
Katika alama hiyo iliyotayarishwa na Posta na karakana ya Vatican kuna maandishi: "Maadhimisho ya kwanza ya Dies Natalis ya Papa Francisko(2013-2025)" na "Poste Vaticane - 21.04.2026."
Kipenyo cha madali hiyo maalum ni milimita 38. Vifaa vilivyotengeneza na kutiwa muhuri ipasavyo ambapo kwa mwombaji, lazima ifike kutoka Sehemu ya Huduma ya Posta na philately ifikapo tarehe 30 Mei 2026.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.
21 Aprili 2026, 09:42