Mkutano wa Radio ya Umma ya Ulaya huko Sofia
Vatican News
Kwa kuwa mwenyeji wa Radio na Televisheni ya Umma ya Burgaria, Jukwaa litafanyika katika kituo cha John Atanasoff huko Sofia, lililoandaliwa na EBU(Umoja wa Utangazaji wa Ulaya), tukio la kila mwaka linalowakutanisha wahusika wakuu wa radio za umma barani Ulaya. Changamoto za uvumbuzi na usambazaji wa kiteknolojia, na suala la kuwavutia wasikilizaji vijana, ni baadhi ya mada ambazo wawakilishi wa vituo vya radio vya Ulaya watajadili katika mji mkuu wa Bulgaria mnamo tarehe 23 Aprili 2026. Siku hiyo itatengwa kwa ajili ya kujadili changamoto na fursa za kimkakati kwa kipindi cha 2026-2027, kwa kuzingatia uvumbuzi wa kiteknolojia, kuanzia na Akili Unde (AI,) usambazaji, na ushiriki wa hadhira changa. Radio ya Vatican pia itashiriki katika tukio hilo, ikiwakilishwa na Alessandro Gisotti, Rais wa Kikundi cha Habari za Radio na Sauti cha EBU.
Agenda: ni mikakati iliyo nyuma tayari ya Kampenii ya Radio
Mkutano huoa utatanguliwa na Mkutano wa Vyombo vya Habari vya Ulaya ambao utafunguliwa na Sibyle Veil, Rais wa Radio Ufaransa na Mkuu wa Kamati ya Radio Ulaya, ambaye ataelezea vipaumbele vya mustakabali wa radio ya Ulaya katika mazingira ya vyombo vya habari yanayozidi kuwa na ushindani na magumu. Miongoni mwa mada kuu kwenye ajenda ni mikakati iliyo nyuma ya kampeni ya Radio Tayari, inayolenga kuhakikisha uwepo wa redio katika magari mapya.
Kuwasilisha shuguli zifanyikazo kwa ngazi ya Ulaya
Mkuu wa Radio wa EBU, Edita Kudláčová pia atazungumza. Atawasilisha shughuli zinazofanywa katika ngazi ya Ulaya, akichunguza masuala yanayohusiana na usambazaji wa radio, ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa mageuzi ya FM, DAB, na IP. Mikakati ya ushirikiano kati ya tasnia na taasisi kwa ajili ya mustakabali wa radio za Ulaya pia itaainishwa. Tukio hilo pia litatoa mwanga juu ya jukumu la muziki na maudhui ya kiutamaduni katika radio ya umma, ambayo imekuwa msingi wa Umoja wa Utangazaji wa Ulaya, ambao ulisherehekea kumbukumbu yake ya miaka 75 mwaka 2025.
Imesasishwa Aprili 22 saa 4.35 asubuhi na Angella Rwezaula.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.