Biashara haramu ya binadamu. Biashara haramu ya binadamu. 

Vatican kwa OSCE:Waathiriwa wana uwezekano mdogo wa kutambuliwa

Mwakilishi wa Vatican alisisitiza vipaumbele vitatu muhimu vya kupambana na biashara haramu ya binadamu katika aina zake zote:'Kanuni isiyo ya adhabu kwa waathiriwa,''kupanga upya sera za uhamiaji na usalama kupitia lenzi inayozingatia ulinzi'na'kuimarisha kinga na ushirikiano'.”Ni katika hotuba iliyotolewa huko Vienna,Austria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Ulaya Osce,Aprili,2026.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwakilishi wa kudumu wa Vatican,  katika Baraza la Usalama la Umoja wa Ulaya (OSCE) wakati wa Mkutano wa Mshikamano dhidi biashara haramu ya wanadamu huko  Viena, Austria,  tarehe 21 Aprili 2026 alitoa hotuba yake ambapo alibainisha kuwa ujumbe wake unavyokaribisha lengo la Mkutano huo wa 26 wa Muungano kuhusu biashara haramu ya binadamu kwa madhumuni ya unyonyaji wa jinai. Waathiriwa, mara nyingi wanawake, watoto, wahamiaji, wakimbizi na watu binafsi katika hali za udhaifu mkubwa, wana uwezekano mkubwa wa kulazimishwa kufanya shughuli za uhalifu na baadaye kutendewa kama wahalifu, na hivyo kuzidisha mateso yao badala ya kutambuliwa kama watu wanaohitaji ulinzi, utambuzi, usaidizi, utunzaji na haki.

Wito wa Papa Leo XIV

Hivi karibuni Papa Leo XIV alitoa "wito wa haraka" wa kukabiliana na kukomesha uhalifu mkubwa kama huo wa kuwanyonya wale ambao tayari wamejeruhiwa na vita, kuhama makazi yao na umaskini. Alionya kwamba aina mpya za "utumwa wa mtandaoni" zinaibuka, ambapo watu wanavutiwa na mipango ya mtandaoni na kulazimika kushiriki katika ulaghai wa kifedha na shughuli zingine za uhalifu. Katika suala hilo, Ujumbe wake unathibitisha kwamba usalama mzuri hauwezi kupatikana isipokuwa Mataifa yachukue hatua madhubuti na zilizoratibiwa dhidi ya biashara haramu ya binadamu katika aina zake zote. Mwakilishi wa Vatican aliomba  kusisitiza  vipaumbele vitatu muhimu vya kupambana na biashara haramu ya binadamu katika aina zake zote.

Mamlaka za kutekeleza sheria

Kwanza, "kanuni isiyo ya adhabu" inapaswa kuzingatiwa ili kuhakikisha kwamba waathiriwa hawaadhibiwi au kushtakiwa isivyo haki kwa matendo ambayo huenda waliyatenda kama matokeo ya moja kwa moja ya kusafirishwa nje ya sheria. Mamlaka za kutekeleza sheria, waendesha mashtaka na majaji wanapaswa kuzingatia hasa ukweli kwamba waathiriwa wa usafirishaji haramu mara nyingi pia ni waathiriwa wa unyonyaji wa kingono, wakilazimishwa kushiriki katika mitandao ya ukahaba, binacha mbaya na ngono ya mtandaoni inayotegemea mtandao.

Bila shaka hii inahitaji kuanzishwa na utekelezaji wa ulinzi wa kisheria ulio wazi, pamoja na utoaji wa mafunzo maalum kwa mamlaka husika za kutekeleza sheria. Kama itagundulika kwamba mwathiriwa wa biashara haramu ya binadamu aliadhibiwa isivyo haki kwa kosa ambalo alilazimishwa kufanya, hatua zinazofaa zinapaswa kuchukuliwa ili kurejesha haki, ikiwa ni pamoja na kufuta rekodi za uhalifu.

Waathiriwa wana uwezekano mdogo wa kutambuliwa

Pili, kupanga upya sera za uhamiaji na usalama kupitia lenzi inayozingatia ulinzi. Uzoefu unaonesha kwamba, kesi za biashara haramu ya binadamu zinaposhughulikiwa kimsingi kupitia lenzi ya udhibiti wa uhamiaji, waathiriwa wana uwezekano mdogo wa kutambuliwa na wana uwezekano mkubwa wa kukamatwa au kufukuzwa nchini. Kwa hivyo, Mataifa Shiriki yanahimizwa kuhakikisha kwamba hatua "dhidi ya uhalifu na biashara haramu ya binadamu hazitakuwa kisingizio cha kudhoofisha heshima ya wahamiaji na wakimbizi".

Ukosefu wa ajira kwa vijana na udhaifu wa kidijitali

Tatu, kuimarisha kinga na ushirikiano. Ongezeko kubwa la uhalifu wa kulazimishwa katika eneo la OSCE, ikiwa ni pamoja na ulaghai unaowezeshwa na mtandao, linasisitiza hitaji la dharura la Mataifa kushughulikia sababu kuu za suala hili, kama vile kutengwa kijamii, ukosefu wa ajira kwa vijana na udhaifu wa kidijitali. Wakati huo huo, juhudi lazima ziongezwe ili kuchunguza na kuzuia kuajiri mtandaoni na uendeshaji wa vituo vya ulaghai.

Jumuiya ya kimataifa inaweza kuziba kwa ufanisi "pengo linaloongezeka kati ya matajiri na maskini [ambalo] linawalazimisha wengi kuingia katika hali hatarishi, nakuwaacha wakiwa katika hatari ya kukabiliwa na ahadi za udanganyifu, za waajiri" kupitia mshikamano na hatua madhubuti za Mataifa yanayoshiriki, mashirika ya pande nyingi, mashirika ya kidini na asasi za kiraia.

MWAKILISHI WA VATICAN OSCE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

22 Aprili 2026, 11:38