Kardinali Kurt Koch. Kardinali Kurt Koch. 

Kardinali Koch:Miaka 40 ya ziara ya kwanza ya Papa Yohane Paulo II katika Sinagogi

Kardinali Kurt Koch,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo na Tume ya Mahusiano ya Kidini na Uyahudi,katika taarifa iliyotolewa na Vatican News na Osservatore Romano,alikumbuka kwamba,“Papa Yohana Paulo II aliandaa njia muhimu kwa ajili ya maridhiano ya baadaye kati ya Kanisa Katoliki na Uyahudi.”Leo inaadhimisha miaka 40 ya ziara ya Yohana Paulo II kwenye Sinagogi Kuu la Roma.Ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwa Papa kuingia mahali pa ibada ya Kiyahudi.

Kardinali Kurt Koch

Ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II kwenye Sinagogi ya Roma mnamo  tarehe 13 Aprili  1986, ilikuwa tukio la ajabu. Kwa mara ya kwanza katika historia, Askofu wa Roma aliingia kwenye sinagogi ili kutoa ushuhuda mbele ya ulimwengu kuhusu uthamini wake kwa dini ya Kiyahudi na watu wa Kiyahudi.

Papa alisisitiza kwamba Kanisa Katoliki lina uhusiano na Uyahudi tofauti na dini nyingine yoyote: "Dini ya Kiyahudi si ya 'nje' kwetu, lakini kwa maana fulani ni ya 'ndani' ya dini yetu wenyewe."

Aliwarejea Wayahudi kama "ndugu wapendwa sana na, kwa njia fulani, ndugu zetu wakubwa," hivyo akifupisha kwa ufanisi kile "kilichobainishwa na Mtaguso." Kupitia  ziara hasa hii ya Sinagogi ya Roma miaka arobaini iliyopita na pia kupitia kauli zake nyingi muhimu kuhusu mazungumzo ya Kikatoliki na Kiyahudi, ishara mbalimbali za ufasaha, na urafiki wa kibinafsi aliodumisha na watu wa Kiyahudi, Papa Yohane Paulo  II aliweka njia muhimu kwa ajili ya mustakabali wa maridhiano kati ya Kanisa Katoliki na Uyahudi.

MIAKA 40 YA MT PAPA YOHANE PAULI II KATIKA SINAGOGI
17 Aprili 2026, 10:45