Maandalizi ya Sinodi Maandalizi ya Sinodi  (@Vatican Media)

Hatua zinazofuata za safari ya Kisinodi zimetangazwa!

Mnamo Aprili 17,Baraza Maalum la Sekretarieti Kuu ya Sinodi lilikutana mtandaoni kujadili njia ya kufuata katika maandalizi ya mikutano ijayo ya tathmini mwezi Juni,ambayo Papa atahudhuria moja ya kikao.Pia mezani kulikuwa na usaidizi wa maandalizi na mbinu kwa ajili ya mkutano kuhusu Amoris laetitia,ulioitishwa na Papa mwenyewe na uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.

Vatican News

Kupanga matukio mengi yanayohusisha Sekretarieti Kuu ya Sinodi ilikuwa lengo la mkutano wa Baraza la Kawaida la XVI, uliofanyika mtandaoni alasiri ya Ijumaa, tarehe 17 Aprili 2026. Hili liliripotiwa katika taarifa kwa vyombo vya habari, ambayo inasema kwamba,  baada ya muda wa sala ulioongozwa na Sista Nathalie Becquart, Katibu Msaidizi wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu Sinodi  alifungua mkutano huo kwa mawasiliano kadhaa kuhusu utekelezaji wa sasa wa Hati ya Mwisho ya Mkutano wa XVI, kazi ya Vikundi vya Utafiti, ambavyo ripoti zake za mwisho zinachapishwa kwa sasa na mkutano ujao wa mikutano miwili.

Mchango wa Papa

Mkutano wa kwanza ni kuanzia tarehe 23 -25 Juni 2026, ili kujiandaa kwa Mkutano wa Tathmini wa Bara uliopangwa kufanyika katika robo ya kwanza ya 2028. Papa Leo XIV pia atashiriki katika kikao maalum cha kazi. Kulingana na taarifa hiyo: “Wafuatao wamealikwa kwenye mkutano huo: mwakilishi wa Mapatriaki wa Baraza la Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki, Marais wa Umoja wa Kimataifa wa Mabaraza ya Maaskofu, pamoja na Marais wa Mabaraza ya Maaskofu wa Marekani na Canada, kila mmoja akifuatana na Mratibu wa Timu ya Sinodi ya chombo chao husika na ikiwezekana, Katibu Mkuu.

Mkutano kuhusu Amoris Laetitia

Katika tukio la mkutano mjini Vatican ulioitishwa na Papa, kuanzia tarehe 7-14 Oktoba 2026, ili kuadhimisha miaka kumi ya kuchapishwa kwa Wosia wa Kitume wa Baada ya Sinodi Amoris Laetitia, marais wa Mabaraza ya Maaskofu kutoka ulimwenguni kote na Sinodi za Makanisa Katoliki ya Mashariki sui iuris watakusanyika ili kujadili kuhusu familia. Katika mkutano huo, Papa Leo XIV anakusudia "kuendelea, kupitia kusikilizana kwa pamoja, na utambuzi wa sinodi kuhusu hatua za kuchukua ili kutangaza Injili kwa familia leo [...] na kuzingatia kile kinachopatikana katika Makanisa  mahalia." Litakuwa ni Baraza la kipapa la Walei, Familia, na Maisha litakaloandaa mkutano huo, ambao una asili ya mashauriano.

Hati ya Kuelekeza Njia

Wakati wa mkutano huo, Padre Giacomo Costa, Mshauri wa Sekretarieti Kuu na Katibu Maalum wa Mkutano wa XVI, alipendekeza hati ya utekelezaji wa Sinodi, hasa kwa ajili ya kufanya vikao vya tathmini. Baada ya majadiliano ya maandishi, muundo mkuu wa hati hiyo uliidhinishwa. Toleo la mwisho, lililokusudiwa kuunganisha Miongozo ya Awamu ya Utekelezaji iliyochapishwa mnamo Juni 2025, litapitiwa na Baraza la Kawaida na kuchapishwa mapema kipindi cha joto.

Hatimaye, wajumbe wa Baraza la kawaida walimwomba Kardinali Mario Grech kutoa shukrani zao kwa Askofu Luis Marín De San Martín kwa miaka yake ya utumishi katika Sekretarieti Kuu ya Sinodi, na kumhakikishia maombi yao kwa nafasi yake mpya kama Mhudumu Mkuu wa Sadaka ya Kipapa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 10:13