2026.04.26 Watakatifu 5 walinzi wa Siku ya Vijana Ulimwenguni(WYD)2027 huko Seoul,Korea Kusini. 2026.04.26 Watakatifu 5 walinzi wa Siku ya Vijana Ulimwenguni(WYD)2027 huko Seoul,Korea Kusini. 

COL,yatangaza Watakatifu Walinzi wa WDY huko Seoul 2027!

Mtakatifu Yohane Paulo II,Mtakatifu Andrew Kim Taegon,Mtakatifu Francesca Xavier Cabrini,Mtakatifu Josephine Bakhita na Mtakatifu Carlo Acutis:hawa ndiyo mifano ya imani ambayo vijana wanaweza kuitegemea na kuitafakari kwa kina waliochaguliwa katika tukio hilo.Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Ndani kwa Siku ya Vijana Duniani ijayo 2027.

Vatican News

Katika taarifa ya Kamati ya Maandalizi mahalia (COL) kuhusiana na  Siku ya Vijana Duniani (WYD)ijayo ya 2027 huko Seoul  nchini Korea Kusini ilitangaza majina ya Watakatifu watano wa WYD, ikiwaonesha kama "mifano ya imani kwa vijana na kama miongozo kupitia ushuhuda wa maisha yao na hali yao ya kiroho." Hawa ni: Mtakatifu Yohane Paulo II (1920–2005), mwanzilishi wa Siku ya Vijana Duniani, anayekumbukwa kwa kujali kwake vijana, familia, na hadhi ya maisha ya mwanadamu; Mtakatifu Andrew Kim Taegon (1821–1846) na wenzake, Padre wa kwanza Mkatoliki wa Korea, ishara ya imani na ujasiri, aliyeuawa kishahidi akiwa na umri mdogo; Mtakatifu Francesca Xavier Cabrini (1850–1917), mmisionari aliyejulikana kwa kuwatunza wahamiaji na maskini; Mtakatifu Josephine Bakhita (1869–1947), mtumwa aliyeachiliwa huru ambaye baadaye akawa mtawa, shuhuda wa matumaini, uhuru, na imani iliyobadilishwa kupitia mateso; Mtakatifu Carlo Acutis (1991–2006), mtakatifu kijana wa enzi ya kidijitali ambaye maisha yake yanabaki kuwa mfano wa uinjilishaji wa kidijitali.

Kuwaombea walinzi

Chaguo lilianza muda mrefu uliopita, na mchakato wa uteuzi ulioanza mwishoni mwa 2024 na utafiti wa kitaifa wa vijana, wafanyakazi wa huduma ya vijana, na waelimishaji, ikifuatiwa na mapitio ya wagombea na uteuzi wa mwisho na kamati hiyo COL. Baadaye, taarifa kwa vyombo vya habari inasema, kundi la vijana wa kujitolea walitumia miezi miwili kusoma maisha na hali ya kiroho ya watakatifu watano walinzi. Kupitia majadiliano na tafakari ya pamoja, vijana waliandaa sala ya kujitolea na ishara ya mwakilishi kwa kila Mtakatifu, wakitafuta kuelezea ushuhuda tofauti ambao kila mmoja hutoa kwa vijana wa leo hii.

Farrell:Utakatifu si wazo la mbali

"Watakatifu walinzi wana jukumu la msingi katika maandalizi ya kila Siku ya Vijana Duniani:" Haya yalisemwa na Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Walei, Familia, na Maisha. Kulingana na Kardinali, "wanawaalika vijana, waelimishaji, na wachungaji kutafakari juu ya karama ya wito wa Mungu, kuhusu ubatizo, ukuhani, dini, na wito wa ndoa, wakitutia moyo kuitikia kwa ukarimu na ujasiri katika kumfuata Kristo aliyeshinda ulimwengu, kama mada ya WYD inayofuata inavyokumbusha." Kardinali Farrell anatumai kwamba ushuhuda wao utawatia moyo vijana, hasa katika mazingira yaliyojaa shida na mateso, kuona kwamba utakatifu si wazo la mbali, bali ni wito wa kujibiwa.

Askofu Mkuu wa Seoul:Kifungu cha kina cha Kiroho na Watakatifu

"Watakatifu hawa walinzi," alielezea Askofu Mkuu Peter Soon-taick Chung wa Seoul, rais wa Kamati ya Uandaaji ya WYD Seoul 2027, "huzunguka mabara na vizazi, na kila mmoja wao hutoa njia halisi ya kuishi imani katika hali halisi ambayo vijana wanakabiliana nayo leo." Matumaini ya Askofu Mkuu ni kwamba vijana wataanzisha uhusiano wa kina wa kiroho na walinzi wao.

Wewe ni Mtakatifu gani?

Kamati ya Maandalizi ya Eneo inawasilisha maisha na hali ya kiroho ya watakatifu walinzi kwenye tovuti rasmi ya WYD Seoul 2027 na kwenye njia zake za mitandao ya kijamii kupitia maudhui na programu za ziada ili kuwasaidia vijana kushiriki kwa karibu zaidi na ushuhuda wao. Pia kuna kipengele shirikishi kinachoitwa "Gundua Mlinzi Wako Mtakatifu!" Kikiwa kimeundwa kwa mtindo wa majaribio ya utu na majaribio shirikishi, kipengele hiki kinawaalika watumiaji kujibu mfululizo wa maswali ya kuchagua ili kugundua ni yupi kati ya watakatifu watano walinzi anayelingana vyema na utu hadhi yao.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

26 Aprili 2026, 14:57