Papa Francisko wakati wa Jukwaa la Watu wenye ulemavu kunao tarehe 11 Juni 2016. Papa Francisko wakati wa Jukwaa la Watu wenye ulemavu kunao tarehe 11 Juni 2016. 

Vatican yataka kuongezwa kwa ujumuishaji wa watu wenye utindi wa ubongo

Askofu Mkuu Ettore Balestrero,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika Mengine ya Kimataifa huko Geneva,Uswiss alisema kwamba "watu wenye utindi wa ubongo wana hadhi na thamani takatifu sawa na mtu mwingine yeyote na kwamba"tabia za ubaguzi na za kijeni zinazohusiana na uchunguzi wa ujauzito na utoaji mimba kwa watoto wanaotambuliwa na utindi wa ubongo lazima zikataliwe kabisa."

Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Askofu Mkuu Ettore Balestrero, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa na Mashirika Mengine ya Kimataifa huko Geneva, alitoa hotuba yake kando ya hafla ya mfuko wa Jérôme Lejeune katika Siku ya watu wenye Utindi wa ubongo duniani 2026. “Watu wenye utindi wa ubongo ni zaidi ya hali yao ya yale ambayo wengi hufikiria. Wao pia kama sisi, wana hadhi sawa ya asili na thamani takatifu, iliyowekwa kwao kwa makusudi na kwa upendo na Mungu tangu wakati wa kwanza wa kutungwa mimba. Sote tuna haki sawa za kimsingi."

Upweke hadi ujumuishaji 

Siku hiyo huadhimisha kila ifikapo tarehe 21 Machi ya kila mwaka, na kwa mwaka huu 2026, kauli mbiu ilikuwa: "Kutoka Upweke hadi Ujumuishaji: Kuthamini Utofauti wa Kijeni wa Binadamu ili Kuwezesha Utekelezaji Bora wa Haki kwa Watu Wenye utindi wa ubongo." Kwa njia hiyo, Askofu Mkuu, alielezea kuwa ujumuishaji sio "suala la kutoa huduma au unaofaa tu bali ni suala la kutambua watu wote katika jamii zetu." Mwakilishi wa Vatican aliwataka washiriki na waandaaji wa tukio hilo kuthibitisha tena juhudi zetu zisizoyumba za kukuza na kutetea utu wa asili, haki za msingi, na thamani isiyo na kifani ya watu wote katika kila hatua ya maisha," aliwatia wote moyo aliporejesha wito wenye shauku. Aliongeza na kusema kwamba, “desturi za kibaguzi na za kijeni zinazohusiana na uchunguzi wa ujauzito na utoaji mimba kwa watoto waliogunduliwa kuwa na utindo wa ubongo, lazima zikataliwe kabisa.” Askofu Mkuu Balestrero aliwashukuru wataalamu na taasisi nyingi kote ulimwenguni ambazo zimejitolea kuendelea kuwatunza watu wenye utindi wa ubongo na familia zao.

Mfumo wa Utunzaji na usaidizi

Hivyo basi, Askofu mkuu alithibitisha umuhimu wa upendo, ubinadamu, na kujali kutoka moyoni. Mfumo wa utunzaji na usaidizi unaweza kuwa mkamilifu kiutendaji, lakini ikiwa hauna moyo, unakuwa baridi na usio na utu, alisema, huku akikumbuka wakati Papa Leo XIV alipowakumbusha wote kwamba ubora wa maisha ya mwanadamu hautegemei mafanikio, bali upendo. Alisisitiza kwamba thamani ya maisha ya mtu haipaswi kupimwa kwa manufaa au utendaji bali kwa ukweli rahisi na wa kina wa kuwa mwanadamu, alihitimisha akisema kwamba, Juhudi zetu za pamoja ziendelee kujenga utamaduni wa maisha na ubinadamu ambapo kila mtu mwenye utindi wa ubongo anatambuliwa kama wa kipekee na asiyeweza kurudiwa na anapaswa kukaribishwa kwa hadhi na heshima.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

27 Machi 2026, 09:33