2026.03.23  Kitambaa cha Veronica chney Uso Mtakatifu 2026.03.23 Kitambaa cha Veronica chney Uso Mtakatifu 

Kitambaa cha Veronika,Kanisa Kuu,Kard.Gambetti:kutupeleka kwa Kristo

Hija ya Kwarezima inaendelea kwa nia ya kutembelea maeneno Matakatifu Roma.Tangu karne ya Tatu,tamaduni ya kale hukusanya wanahija katika Makanisa ambayo yanahifadhi masalima ya watakatifu na mashahidi.Katika Dominika ya 5,waamini walifika katika Basilika ya Mtakatifu Petro kuona Kitambaa cha Uso Mtakatifu.Mkuu wa Kanisa hilo alisema kuwa“kifo kiwe dada yetu kwa kumkaribia Kristo."

Vatican News

Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro liliwakaribisha waamini alasiri ya  Dominika ya tano ya Kwaresima, tarehe 22 Machi 2026 walipokuwa wakisali kuzunguka Madhabahu ya Maungamo, huku wakisubiri kuonyeshwa kwa Kitambaa cha Veronica. Salia hilo, kwa maneno ya Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtatifu Peteo  "linatualika kugeuza macho yetu kuelekea Golgotha, ambapo Kristo aliyesulubiwa atadhihirisha utukufu Wake."

Sherehe

Sauti ya kengele ilitangaza kuwasili kwake. Katika ukimya, kila mtazamo uliiunuliwa kuelekea sanamu ya mwanamke aliyemhurumia Kristo njiani kuelekea Kalvari. Kutoka hapo, "Uso Mtakatifu" ulifunuliwa, ukifikiriwa na waamini katika ukimya unaobadilishwa na kujaa mateso ya Yesu, yaliyochorwa kwenye kitambaa  hicho. Damu iliyomwagika ya  Mwokozi inakumbusha, wakati huu wa Kwaresima, ubinadamu wa Yesu na umungu wake. Huruma kubwa ambayo mtu anahisi anapokabiliwa na picha hiyo inayoakisi kile ambacho Yesu alihisi kwa Lazaro. Kutoka madhabahuni  Kardinali Gambetti, wakati wa misa Takatifu alizungumzia  tofauti kubwa kati ya maisha ambayo Kristo huleta na kifo cha Lazaro. Ahadi ya Yesu inatangaza "ushindi wa mwisho juu waliohukumiwa: kuachwa, utumwa, udhaifu, kupotoshwa, kukwazwa, mateso, kifo."

Kifo Kinachokuwa Dada

Ikiwa Kitamba cha Veronica kinaashiria kifo, Kardinali alizungumzia kifo ambacho kinaweza kuwa dada, kama Mtakatifu Francis alivyohubiri: "Kinakuwa dada kinapofungua milango ya kukutana na Yesu Kristo, kama kilivyofanya kwa Lazaro. Kufa kimwili, lakini pia udhaifu wetu, hasa ule wa moyo, hufisha maisha. Kifo cha roho kinaweza kuwa dada tunapoomba kutoka ndani kabisa,” alisisitiza.

Ishara ya Huruma ya Mungu

Ufunguo wa mabadiliko yanayoleta maisha mapya kutokana na kifo ni upendo: "Injili ya leo," Kardinali aliendelea, "inamkumbuka Yesu, aliyempenda Martha, dada yake Lazaro. Upendo ndio sababu inayompeleka kuvumilia maumivu ya kupotea na marafiki zake." Kutokana na upendo huu, huruma ya Kristo huzaliwa, ambayo hutokana na hitaji la ukaribu: 'Mmemweka wapi?'" Swali lile lile "lililosumbua vifo visivyoeleweka na hali za vurugu na vita tunazoshuhudia bila msaada." Kilio cha Yesu mbele ya kaburi la Lazaro ni ishara ya huruma ya Mungu kwa sababu, Gambetti aliendelea, "mwanadamu hakuumbwa kwa ajili ya kifo, hakuumbwa kwa ajili ya kutengwa na raha za ubinafsi, hakuumbwa kuwa katika minyororo au huzuni. Mwanadamu ameumbwa kwa ajili ya uzima, aliumbwa kushiriki zawadi na wengine, kuungana, kuwa huru na furaha."

Kupata furaha ya ufufuko

Kama Lazaro, Yesu alimwita kila mmoja kwake. "Mwanamke aliyefuta uso wa Yesu kwa kitambaa chake tulichheshimu," Kardinali alihitimisha, "atufundishe hisia za kumfuata Yesu. Na Maria aliyebeba ndani yake mbegu ya uzima hata kama mwanawe alikufa na upanga ulimchoma roho yake, atusindikize hadi chini ya msalaba ili tupate uzoefu pamoja naye, kupitia machozi, furaha ya ufufuo katika kila hali, kila wakati, kila wakati."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

 

 

23 Machi 2026, 16:32