2026.03.14 Messa inaugurazione dell'anno Giudiziario del Tribunale dello Stato della Citta' del Vaticano

Kard.Parolin:Kusudi lenyewe la Sheria ya Kanisa,kiukweli ni wokovu wa roho

Haki ya binadamu inalenga katika ukarabati kamili wa kibinadamu na kijamii wa waliohukumiwa. Ndivyo Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican alibainisha wakati wa kuongoza misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Paulo kwenye Jumba la Kitume kwa washiriki wa ufunguzi wa mwaka wa mahakama Kuu ya Rufaa ya Vatican,Jumamosi tarehe 14 Machi 2026.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican, Jumamosi tarehe 14 Machi 2026 katika Kikanisa cha Paulo kwenye  Jumba la Kitume kwa washiriki wa ufunguzi wa mwaka wa mahakama  Rufaa ya Jiji la Vatican aliongoza ibada ya misa. Katika mahubiri alisisitiza kwamba, kama vile haki ya Mungu inavyoweza "kutunza, kupenda, kuokoa, na msamaha kwa mwenye dhambi anayetubu, haki ya binadamu, iliyoongozwa na ile ya kwanza, inapaswa pia kuwa na uwezo wa kuimarisha lengo la kielimu la adhabu, ambalo badala yake mara nyingi hufuatiliwa kwa unyonge kutokana na uhaba wa rasilimali zilizotengwa kwa taasisi za kurekebisha tabia.

Mungu anaendelea kutenda ili mtu akue katika ushirika na Agano naye

Kardinali alipanua mtazamo wake ili kujumuisha mifumo ya mahakama ya nchi zingine, akibainisha kwamba, licha ya uthibitisho wa kanuni kuhusu kusudi la kuelimisha upya adhabu ya jinai," zimeundwa kwa njia ambazo "zinadhoofisha" kile kinachopaswa kuwa "kusudi lao muhimu zaidi," yaani, urekebishaji wa kibinadamu na kijamii wa waliohukumiwa. Sura ya sita ya Kitabu cha Nabii Hosea, iliyopendekezwa na masomo ya siku hiyo, inafafanua haki ya Mungu kama nuru inayoangazia historia ya watu wa Mungu, historia ya ubinadamu na ya kila mtu hasa,"ikionesha kwamba sio mfuatano wowote wa adhabu na adhabu zinazotokana na kutoamini kwingi lakini, Kardinali Parolin alisisitiza: "kama utunzaji na marekebisho ambayo Mungu ameyafanya na anaendelea kuyafanya ili kila mtu akue katika ushirika na agano naye."

Injili:Haki katika Nabii Hosea na Injili ya Mtoza ushuru

Hata katika kifungu cha Injili ya Luka, "haki ile ile iliyozungumziwa na nabii Hosea inaonekana." Katika mfano uliosimuliwa na Yesu, mtoza ushuru na mfarisayo kwenda hekaluni kusali, lakini wanafanya hivyo kwa mitazamo tofauti. Wa kwanza "atahesabiwa haki," wa pili "atatangazwa kuwa na hatia." Mfano wa Injili, Katibu Mkuu wa Vatican  alisema, unalenga "kutuhimiza" tusonge mbele zaidi ya "mantiki ya kulipiza kisasi ya haki" iliyopo katika ufunuo wa Biblia, "hasa ​​katika Agano la Kale." "Kusudi kuu la haki ya kimungu," kardinali aliendelea, "si kupima sifa au makosa ya kila mtu kwa kipimo baridi na kisicho na utu, bali kumrekebisha mtu huyo ndani na hivyo kumwongoza kwenye uongofu mkubwa kwa Bwana, kukuza mabadiliko ya moyo, ambayo kisha hujidhihirisha katika toba na utambuzi wa unyenyekevu wa dhambi za mtu." Hasa tafakari hii ya haki ya kimungu" ambayo "inaongeza kusudi la kuelimisha upya adhabu," lazima "iangaze zaidi katika mfumo wa kisheria wa Vatican, alisema Kardinali Parolin."

Mtu aliyehukumiwa anaweza kuunganishwa katika jamii

Kuhakikisha kwamba mtu aliyehukumiwa, baada ya kutumikia kifungo chake, anaweza kuunganishwa tena katika jamii na kuchangia vyema katika maisha yake si kitu cha asili ya mapambo au mwelekeo, bali ina nafasi kuu. Kardinali  Parolin aliongeza, kusudi lenyewe la Sheria ya Kanisa, kiukweli ni "wokovu wa roho," na "sheria kuu ya haki ya kidunia daima ni na kwa vyovyote vile ni faida ya watu." Watendaji wa haki ni "wakalimani" na "wanaowajibika" kwa kusudi hili, na ili kutimiza hilo, Kardinali alisisitiza, haitoshi kuwa na "usingizi wa kutosha wa mafunzo ya kiufundi na kitaaluma" na "sifa bora za kibinadamu." Kardinali aliongeza kusema  ni muhimu, kuanza safari ya kibinafsi na ya kiroho ya uongofu." Ni wale tu "wanaojua ugumu na furaha ya safari endelevu ya uongofu ambao ni uhusiano wa karibu na Bwana pekee wanaoweza kutoa" ndio wanaweza kuwa "watendaji wa haki," bila kuanguka katika mtazamo wa Mfarisayo aliyeelezwa katika Injili. Na Kwaresima yenyewe ni "wakati mzuri" wa "kuanza na kuanza upya safari hii," ulinzi ambao hatimaye Kardinali Parolin aliukabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria, "kioo cha haki."

PAROLIN MISA KWA MAHAKAMA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

14 Machi 2026, 14:19