Ruffini:"Vyombo vya habari viongoze kumtetea binadamu"
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Karibu makampuni hamsini yanayoongoza nchini Italia, vyama, na mashirika katika sekta ya tatu yalikaa chini katika "Connact" kujadili kile ambacho nchi inafanya na kuendeleza katika ngazi mbalimbali. Majopo kumi na matatu ya majadiliano, kilimo-chakula, uchumi wa mviringo, ulinzi, demokrasia na haki, nishati, fedha, chakula, viwanda na masoko, vyombo vya habari, vifaa, teknolojia, dawa, utafiti na uvumbuzi, yalifupisha vipaumbele vya ajenda ya Ulaya. "Ulaya kwa sasa inakabiliwa na changamoto yake ngumu zaidi: kuunganisha vitendo na ukweli na maono ili kuupatia mfumo wetu wa kiuchumi mustakabali," alisema hayo Antonella Sberna, Makamu Rais wa Bunge la Ulaya, akizungumzia mkutano na ubadilishanaji kati ya mfumo wenye tija na siasa. Katika mazingira tata ya kimataifa ya kipindi hiki cha kihistoria, kama ilivyoakisiwa katika hotuba zingine za wawakilishi wa Italia ndani ya EU, mawasiliano na taarifa zina jukumu muhimu, hasa leo zinakabiliwa na maendeleo makubwa ya akili unde
"Uraia wa kidijitali unaofahamu na kuwajibika"
Katika suala hili, kando ya mkutano, huo Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, alibainisha kwamba mazingira ya sasa ya vyombo vya habari yanahitaji kutafakari kuhusu vipengele mbalimbali vya mawasiliano, kimsingi uwazi na ufuatiliaji wa vyanzo, ambavyo lazima vihusishe tasnia ya teknolojia pamoja na wabunge, ulimwengu wa kitaaluma na kisanii, tasnia za ubunifu, na wale wanaotoa taarifa. Kila mtu, Dk. Ruffini alisema, akimaanisha ujumbe wa Papa Leo XVI kwa ajili ya Siku ya 60 ya Mawasiliano Duniani, lazima kuhisi "kuhusika katika kujenga na kutekeleza uraia wa kidijitali wenye taarifa na uwajibikaji."
Changamoto iliyo mbele yetu si kuzuia uvumbuzi wa kidijitali
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alikumbuka kwamba tangu mwanzo wa upapa wa Leo XIV, aliwasihi waandishi wa habari hasa "wasikubali kamwe ujinga," changamoto ambayo Ruffini anaiona kama wasiwasi wa kila mtu. Akikumbuka kazi inayofanywa na Baraza la Kipapa, kwa asili yake maalum ya kimataifa - wahariri na wafanyakazi wa kiufundi kutoka zaidi ya nchi 70, lango la vyombo vya habari vya Vatican News, vyenye watumiaji wa kipekee karibu milioni sita kwa mwezi, katika takriban lugha 60, vikijumuisha lugha tatu za ishara, na wastani wa kila mwezi wa takriban watazamaji milioni 20. Dk. Ruffini alirudia, hata maneno ya Papa Leo XIV, kwamba "changamoto iliyo mbele yetu si kuzuia uvumbuzi wa kidijitali, bali kuuongoza." Aliongeza kuwa kila mmoja wetu ana kazi ya "kuinua sauti zetu, pamoja, katika kuwatetea wanadamu, ili zana hizi ziweze kuunganishwa kweli nasi kama washirika."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here