Papa Leo XIV alipotembelea SantaMaria Galeria :kituo cha kurushia matangazo cha Radio Vatican. Papa Leo XIV alipotembelea SantaMaria Galeria :kituo cha kurushia matangazo cha Radio Vatican.  (ANSA)

Radio Vatican yaadhimisha miaka 95 kwa vipindi saba vya lugha nyingi!

Mnamo Februari 13, 2026,katika maadhimisho ya Siku ya Radio Duniani(WRD),Radio Vatican–Vatican News inatangaza mpango maalum katika lugha saba zenye vipindi saba vya radio ambavyo vitakuwa podikasti zenye mada maalum zilizokita na mustakabali wa Radio,utumishi wa umma,uvumbuzi na uhusiano kati ya vyombo vya habari,jamii na akili unde,kwa kaulimbiu:"AI ni chombo,siyo sauti."

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Mpango maalum katika lugha zaba zenye vipindi vingi vya Radio Vatican, unakuja siku moja baada ya maadhimisho ya miaka 95 ya Radio ya Mapapa: tarehe 12 Februari 2026.  Radio ilianzishwa mnamo mwaka 1931 kwa idhini ya Papa Pio XI na kuanzishwa na baba wa radio, Guglielmo Marconi, ambapo kituo cha Papa kinawakilisha mojawapo ya uzoefu wa zamani zaidi wa utangazaji wa radio duniani. Iliundwa ili kuunganisha Kanisa Kuu na kila sehemu ya sayari na kuwafikia watu, tamaduni, na lugha mbalimbali.

AI is a tool,not a voice(Akili Unde)ni chombo na si sauti

Katika kitovu cha programu kutakuwa na mada iliyochaguliwa kwa ajili ya Siku ya Radio Duniani WRD 2026: AI is a tool, not a voice yaani  Akili Unde(AI)  ni chombo na siyo sauti, Mazungumzo pia kwa kuzingatia Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Siku ya Mawasiliano Duniani 2026, unaokumbusha thamani ya uwajibikaji wa binadamu, utambuzi, na sauti halisi katika mawasiliano katika enzi ya akili unde.

Sauti za Wataalamu wa Kimataifa,Watendaji,Wasomi na Wavumbuzi

Vipindi hivyo saba vitawashirikisha wataalamu wa Kimataifa, watendaji wa utangazaji, wasomi, wavumbuzi, na wataalamu wa radio na vyombo vya habari, ambao watatafakari jinsi radio, kituo kikubwa cha kibinadamu, kilichojengwa juu ya sauti, mahusiano, na ukaribu, kinavyoweza kustawi katika enzi ya Akili Unde(AI) bila kupoteza utambulisho wake. Wazungumzaji wa kipindi cha lugha ya Kiitaliano watakuwa pamoja na Andrea Borgnino, Mkurugenzi wa Uhariri wa RaiPlay Sound; Ivana Faccioli, Mkurugenzi wa RTL 102.5 News; Massimiliano Menichetti, Naibu Mkurugenzi wa Uhariri wa Radio Vatican–Vatican News; na Alessandro Gisotti, Rais wa Kikundi cha Habari za Radio na Sauti cha EBU.

Wageni katika vipindi vya Kiingereza,Kifaransa na Kijerumani

Kipindi cha lugha ya Kiingereza kitamshirikisha Padre Felmar Castrodes Fiel, SVD, Meneja Mkuu wa Radio Veritas Asia; Elizabeth O’Malley, Meneja wa Uhariri na Programu, Radio Maria England. Kwa kipindi cha lugha ya Kifaransa, wageni watakuwa ni pamoja na Baptiste Detombe, mwandishi wa kitabu "L'homme démantelé"; Padre Ernest Kouadio, Dk wa mawasiliano ya kijamii na mtaalamu katika uhusiano kati ya Kanisa na Akili Unde; na Florent Latrive, mkuu wa mikakati ya kidijitali ya  Radio France. Kwa kipindi cha lugha ya Kijerumani, wageni watakuwa Gregor Schmalzried, mtaalamu wa akili Unde, mwandishi wa habari, na mtangazaji wa podikasti, ARD (Ujerumani); Stefan Kollinger, Afisa Mkuu wa Ubunifu, ORF (Austria); na Philip Meyer, Bodi ya Uhariri ya SRF (Uswiss).

Sauti za programu za Kihispania,Kireno na Kipoland

Wageni katika kipindi cha Kihispania watakuwa Noel Diaz, mkurugenzi wa mtandao wa Radio ESNE (Marekani na Amerika ya Kati); Fray Miguel Gullon, rais wa Muungano wa Amerika Kusini wa Elimu na Mawasiliano Maarufu; Eva Fernandez, mwandishi wa Radio COPE Uhispania. Kwa Kireno, wageni watasikika: Padre José Inácio de Medeiros, CSsR, mkurugenzi mkuu wa zamani wa Rádio Aparecida; Fernando Geronazzo, mshauri wa mawasiliano wa Jimbo kuu la São Paulo; na Kadinali Odilo Scherer; Padre Danilo Pinto dos Santos, Jimbo kuu la Salvador; na mkurugenzi wa Rádio Excelsior da Bahia (Dom Avelar Brandão Vilela Foundation). Hatimaye, kwa lugha ya Kipoland, washiriki watakuwa: Patrycja Michońska, Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Plus (Eurozet); Padre Mariusz Wedziuk, mkurugenzi wa Jukwaa la Vituo Huru vya Radio Katoliki; Mirosław Kasprzak, mkurugenzi wa Radio Lublin; na Krzysztof Kiryczyk, mratibu wa wafanyakazi wa uhariri wa Radio Zet.

Radio ya Vatican:kuunganisha ulimwengu na masafa  ya sauti

Vipindi hivyo vitaleta pamoja uzoefu kutoka Ulaya, Afrika, Amerika Kusini, na Asia, kuonyesha jinsi redio inavyoendelea kuwa chombo kisichoweza kubadilishwa kwa ajili ya kufikia watu, elimu, uinjilisti, huduma kwa umma, na uvumbuzi. Miaka 95i baada ya kuanzishwa kwake, Radio ya Papa, iliyojengwa na Marconi, inathibitisha wito wake wa awali: kuunganisha ulimwengu kupitia masafa ya sauti, sasa pia kupitia podikasti na majukwaa mapya ya kidijitali. Katika enzi ya akili unde, radio inataka kukumbusha ulimwengu kwamba: teknolojia inaweza kuwa chombo, lakini sauti inabaki kuwa ya kibinadamu kila wakati.

Miaka 95 ya Radio Vatican.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

10 Februari 2026, 13:26