Ukumbi Vyombo vya Habari vya Vatican. Ukumbi Vyombo vya Habari vya Vatican. 

Mkutano umepangwa kati ya Kard.Fernández na Jumuiya ya Mtakatifu Pio X

Akijibu maswali ya waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Vatican alielezea kwamba kutakuwa na"mazungumzo yasiyo rasmi na ya kibinafsi"kati ya Kardinali Víctor Manuel Fernández,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Padre Davide Pagliarani,Mkuu wa Jumuiya ya Mapadre ya Mtakatifu Pio X.

Vatican News

Mkutano umepangwa kufanyika Juma lijalo kati ya Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya kanisa na PadrieDavide Pagliarani, Mkuu wa Jumuiya ya Kikuhani ya Mtakatifu Pio X. Alisema hayo Dk. Matteo Bruni, Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu wakati  akijibu maswali ya waandishi wa habari. "Mkutano huo," alielezea, "utakuwa fursa ya mazungumzo yasiyo rasmi na ya kibinafsi, ambayo yatasaidia kutambua zana bora za majadiliano ambazo zinaweza kusababisha matokeo chanya," alisema.

Taarifa hiyo inakuja siku moja baada ya kusema kwamba mawasiliano yanaendelea kati ya Jumuiya ya Mtakatifu Pio X na Kiti Kitakatifu, kwa hamu ya "kuepuka mipasuko au suluhisho la upande mmoja kuhusu masuala yaliyojitokeza." Jibu la Dk. Bruni lilitokana na tangazo la Jumuiya ya Mtakatifu Pio X mnamo Februari 2 kuhusu Daraja Kuwekwa wakfu wa Kiaskofu, uliopangwa kufanyika mnamo Julai 1 katika Seminari ya Kimataifa ya Mtakatifu Yohane wa Ars huko Flavigny-sur-Ozerain, Ufaransa.

Katika taarifa iliyotolewa na Jumuiya, ilirejewa barua iliyotumwa kwa Kiti Kitakatifu, ikielezea "umuhimu maalum wa Jumuiya kuhakikisha mwendelezo wa huduma ya Maaskofu wake." Kiti Kitakatifu, Jumuiya ilielezea, kilituma "barua ambayo haijibu maombi yetu kwa vyovyote," ambayo ilisababisha uamuzi wake wa kuendelea na njia iliyooneshwa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

06 Februari 2026, 13:01