Gallagher:Kujenga Upya Uaminifu na mazungumzo katika dunia yenye giza,vita na migawanyiko
Daniele Piccini na Angella Rwezaula – Vatican.
Heri na mantiki ya aminifu, wito wa tumaini, maadhimisho ya Miaka 25 ya Mkataba kati ya Slovakia na Vatican, maombi kwa ajili ya Ukraine na watu wote walioathiriwa na migogoro, yamo katika meneno Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, aliyosema katika mahubiri yake katika Misa aliyoiongoza, Dominika tarehe 1 Februari 2026, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Martin huko Bratislava, wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya Mkataba kati ya Vatican na Jamhuri ya Slovakia. "Ulimwengu wetu umetiwa giza na vita na migogoro, na mgawanyiko mkubwa. Katika hali kama hiyo, tumaini linaweza kuonekana kuwa mbali, hata kutoeleweka." Lakini tumaini hili linaweza kulishwa tu na jukumu, linalochukuliwa na kila mmoja wetu, la "kujenga upya uaminifu pale ambapo umeharibiwa, kudumu katika mazungumzo wakati ni polepole na magumu, na kuweka wazi njia zinazoongoza kwenye amani."
Katika Injili ya Mlimani, Yesu anaanzisha mantiki ya historia ya mwanadamu
Kwa Mahubiri ya Mlimani, somo lasiku lililochukuliwa kutoka Injili ya Mathayo, Yesu alianzisha mantiki mpya kabisa katika historia ya mwanadamu. "Kabla ya kutoa amri, kabla ya kutuomba chochote, Bwana hutangaza baraka," Askofu alisema. Kristo anawatazama zaidi ya yote "maskini wa roho, wapole, wenye huruma, wapatanishi, wale wenye njaa ya haki, na kusema: heri ninyi." Mabadiliko haya ya mtazamo yanabadilisha maadili na vipaumbele vya historia. "Katika ulimwengu uliozoea kupima maisha kwa mafanikio," Askofu Mkuu Gallagher alisema, "usalama na utambuzi, Kristo anatufungulia mtazamo mwingine. Anafunua mtindo wa maisha usioumbwa na utawala, bali kwa uaminifu; si kwa kujithibitisha, bali kwa ushirika; si kwa hofu, bali kwa tumaini lililojikita katika Mungu." Kwa hivyo, Heri si utopia, "shairi lililotengwa na ukweli," lakini linaelezea "mwendo wa neema katika historia," likiandika njia ambazo "Mungu hufanya ambapo utoshelevu wa mwanadamu unaishia." "Yeye," mwanadiplomasia wa Vatican alisema zaidi, "hujenga ambapo ulimwengu hauoni mengi ya kujenga juu yake.
Mpango wa kiroho, kiutamaduni na kisiasa
Kuwa wa Kristo kunamaanisha kuruhusu mantiki hii kutuumba, ili unyenyekevu uwe mahali pa uhuru, huruma aina ya nguvu, uvumilivu tangazo la kimya kimya la matumaini. Kwa hivyo, tumaini si hisia, bali ni "wito wa kutekelezwa," kama Papa Leo XIV, ulivyonukuliwa na Askofu Mkuu Gallagher, pia alivyoelezea katika Ujumbe wake wa kwanza wa Siku ya Amani Duniani. Papa alitukumbusha kwamba "lazima tutie moyo na kuunga mkono kila mpango wa kiroho, kiutamaduni, na kisiasa unaoweka matumaini hai." Historia ya Slovakia yenyewe inashuhudia "tumaini hili la kudumu," alisisitiza askofu. "Imani ya Slovakia haikuzaliwa kwa urahisi," Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka, "bali kwa uinjilishaji wa subira, uaminifu usioyumba, na uvumilivu wa kimya, kama inavyoshuhudiwa na wanaume na wanawake wengi watakatifu."
Familia na jamii ziungwe mkono
Kuanzia na walinzi wa watu wa Ulaya ya Mashariki, Watakatifu Cyril na Methodius, na Mtakatifu Gorazd, Askofu na Shahidi wa Praga, ambao walishuhudia mantiki hii mpya ya Heri na hivyo kuwakilisha "mfano wa safari hii," kwa sababu "hawakutegemea nguvu au upendeleo, bali kazi ya uvumilivu ya Neno, kuunda lugha, kuunda utamaduni, na kufungua mioyo kwa Injili."Mahusiano kati ya Vatican na Slovakia zenyewe yanaendana na mtazamo huu wa "uaminifu," unaofundishwa na Heri. Katika mtazamo huu huo," alisema mwanadiplomasia wa Vatican, "tunaweza kuweka miaka ishirini na mitano ya Mkataba wa Msingi kati ya Vatican na Slovakia. Ukiwa umezaliwa kutokana na mazungumzo na utambuzi wa pande zote mbili, unaonesha kujitolea kwa pamoja kwa kumtumikia mwanadamu katika ugumu wote wa maisha ya kisasa. Kwa kuheshimu tofauti inayofaa kati ya maagizo ya kiroho na ya kidunia na kukuza ushirikiano kwa manufaa ya wote, inalinda nafasi ambapo dhamiri inaheshimiwa, ambapo familia na jamii zinaungwa mkono, na ambapo uhuru wa kidini huzaa maisha ya kimaadili na kitamaduni ya jamii.
Mfumo wa Utu wa mwandamu uweze kudumishwa
Kwa hivyo, uhusiano kati ya mataifa hayo mawili hutoa "mfumo ambao utu wa binadamu unaweza kudumishwa, mazungumzo yanaweza kustawi, na matumaini yanayotokana na imani, upendo, na haki, yanaweza kuota mizizi na kukua kimya kimya." Kwa mara nyingine tena, masomo ya siku kuhusu Heri, alisema Askofu Mkuu Gallagher, "yanarudi kwa uwazi mpya," kwani "yanatukumbusha kwamba amani haizungumzwi tu, bali huundwa, hupandwa, na kuishi. Inaota mizizi katika mioyo yenye uwezo wa huruma, katika jamii zinazopenda kutafuta haki ya haki, katika taasisi zinazochagua mazungumzo badala ya kutengwa." Mwishoni mwa mahubiri yake, mawazo ya Askofu Mkuu Gallagher yaliwaendea "watu wanaoteseka wa nchi zote zilizoraruliwa na vurugu, hasa Ukraine," akiomba kwamba Roho atuumbe "kama mafundi wa amani, wenye uwezo wa kudumisha tumaini hata linapoonekana dhaifu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here