2026.02.10 Kardinali Czerny akitoa hotuba yake katika Chuo cha Kichungaji huko Chiclayo. 2026.02.10 Kardinali Czerny akitoa hotuba yake katika Chuo cha Kichungaji huko Chiclayo. 

Kard.Czerny:Afya kamili haipo bila upande wake wa kiroho

Katika fursa ya Siku ya XXXIV ya Wagonjwa Duniani,iliyoadhimishwa Februari 11,katika Madhabahu ya Mama Yetu wa Amani huko Chiclayo,nchini Peru,mjumbe maalum wa Papa,Kardinali Czerny alihimiza kugundua upya huruma ya Msamaria Mwema ili kutekeleza sera zinazofaa za umma zinazowezesha upatikanaji wa huduma na kukuza utamaduni wa kweli wa huduma.

Vatican News

Kuelewa afya kutokana na  mtazamo "wa kina", unaohakikisha upatikanaji wa huduma za kimatibabu huku pia ukitoa msaada wa kiroho kwa wale wanaohitaji. Ndilo lililkuwa himizo la Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu na mjumbe maalum wa Papa kwa Siku ya XXIV ya Wagonjwa Duniani, iliyoadhimishwa katika Madhahabu ya  Mama Yetu wa Amani, katika Jimbo Katoliki la  Chiclayo, nchini Peru, tarehe 11  Februari 2026. Katika hotuba yake tarehe 10 Februari katika semina ya kitaaluma, ya kitaalimungu , na ya kichungaji katika Ukumbi wa Moliné wa Chuo cha Mtakatifu Toribio de Mogrovejo, kwenye mji wa Pero, Karidnali aliwasalimia kwa upendo na Baraza kutoka kwa baba Mtakatifu Leo XIV ambaye alimwita “ Askofu wenu” huku akikumbuka miaka akliyoiptia huko katika nchi ya Amerika Kusini.

Kardinali Czerny akitoka hotuba yake huko Chiclayo
Kardinali Czerny akitoka hotuba yake huko Chiclayo

Huruma ya Msamaria Mwema, Moyo wa Injili

Baada ya kumsalimia Balozi wa Vatican  nchini Peru, Askofu Mkuu Paolo Rocco Gualtieri; Askofu wa Chiclayo, Askofu Mkuu Edinson Edgardo Farfán; na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Amerika Kusini (CELAM), Askofu Mkuu Lizardo Estrada Herrera, Kardinali Czerny alielezea kwamba mada za semina hiyo zimeongozwa sana na ujumbe wa Papa kwa ajili ya maadhimisho haya kwa kuhuishwa  "kwenye moyo wa Injili na utume wa Kanisa."

Miongoni mwa haya, aliakisi huruma ya Msamaria Mwema, ambaye anatualika kupenda kwa kuchukua maumivu ya wengine; tafakari juu ya fumbo la mateso ya wanadamu, ambalo linapinga imani na kufungua njia ya tumaini lililofanyika mwili; na maendeleo ya huduma ya kupunguza maumivu Amerika Kusini na  ulimwenguni kote, kama usemi halisi wa heshima kwa utu wa kila mtu kuanzia mimba hadi kifo cha asili. Kardinali pia alisisitiza umuhimu wa huduma kamili ya wagonjwa, akisisitiza kwamba mwelekeo wa kiroho si nyongeza, bali ni nguzo muhimu ya usindikizaji: “ikiwa tunazungumzia afya kamili, mwelekeo wa kiroho hauwezi kukosekana; bila mwelekeo wa kiroho, si fungamani.”

Kardinali akihutubia huko Chiclayo, Peru
Kardinali akihutubia huko Chiclayo, Peru

Kutoka Utambuzi hadi hatua zenye uhalisia

Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu kisha alibainisha kuwa Siku ya Wagonjwa Duniani si mwaliko wa kutafakari na kuomba tu, bali pia kuchukua hatua kwa dhati. "Mateso ya kaka na dada zetu wagonjwa yanatutaka tuwe karibu, tusikilize, tuwe na sera zinazofaa za umma, tuwe na mafunzo ya kitaalamu yenye uwezo, na zaidi ya yote, tuwe na moyo nyeti ambao haubaki bila kujali," alisema. Kwa kufuata mfano wa Msamaria Mwema, alisema, Wakristo wanaitwa kutulia, kuwajali, na kuwa karibu na wengine, hasa wale walio dhaifu na waliosahaulika zaidi.

Roma katika Huduma ya Makanisa Mahalia

Akirejea utume wa Baraza lake, Kardinali Czerny alikumbusha kwamba afya lazima ieleweke kutoka kwa mtazamo kamili, wenye athari kwa mtu mzima na kwa jamii kwa ujumla. Katika suala hilo, alinukuu Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium na kusisitiza kwamba Baraza la Kipapa analoliongoza, linatafuta kusindikiza na kuunga mkono mipango ya Makanisa fMahalia, Mabaraza ya  Maaskofu, taasisi za maisha ya wakfu, Caritas, na wa kujitolea, bila kuwabadilisha. "Roma inahudumia Makanisa  mahalia," alisisitiza, na  kwamba mbinu ya kati kupita kiasi ina hatari ya kuzuia ukweli na uzoefu wa mahali hapo. Mbinu hii, alisema, ni sehemu muhimu ya mageuzi yaliyopendekezwa na Papa Francisko na kuendelea na Papa Leo XIV.

Mkutano huko Chiclayo
Mkutano huko Chiclayo

 

Kuunda Mitandao na Kushiriki Mbinu bora

Kardinali Czerny alitambua changamoto kubwa zinazokabili nchi nyingi katika suala la huduma ya afya, kama vile hali duni ya huduma, ukosefu wa mwongozo wa kiroho, na ugumu wa kupata huduma ya matibabu. Kwa kuzingatia hilo, alihimiza kuimarisha ushirikiano na mitandao, kuwezesha ubadilishanaji wa mbinu bora na kutumia kila kitu ambacho tayari kinazaa matunda katika jamii.

Kuelekea Utamaduni Halisi wa Huduma

Kwa kuhitimisha  hotuba yake, mjumbe maalum wa Papa alionesha hamu yake kwa semina hiyo kuwa "nafasi yenye matunda ya mazungumzo na utambuzi," ambapo mipango thabiti inaweza kutokea ambayo inaimarisha utamaduni halisi wa huduma. Alisema utamaduni, ambapo wagonjwa hutambuliwa kila wakati, huambatana, na kupendwa, wakipata katika Kanisa na Jumuiya"uso wa kibinadamu na wenye huruma kweli."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

11 Februari 2026, 12:00