2026.01.20 Kifuniko cha kitabu cha Kardinali Radcliffe 2026.01.20 Kifuniko cha kitabu cha Kardinali Radcliffe 

"Mshangao wa Matumaini,"Tafakari kuhusu Kanisa linalotembea"

Kurasa za kitabu kilichochapishwa na Nyumba ya Uchapishaji ya Vatican (LEV)kinakusanya baadhi ya michango ya Kardinali Timothy Radcliffe wa Sinodi kuhusu Sinodi.Kitabu hicho kinafunua maono tajiri, ya vitendo na ya kuvutia ya Kanisa katika ulimwengu mamboleo.

Angella Rwezaula, - Vatican News

Mshangao wa Matumaini: Tafakari juu ya Kanisa linalosonga mbele kilichoandikwa na Kardinali Timothy Radcliffe kinapatikana katika Duka la vitabu  la Vatican kuanzia tarehe 22 Januari 2026,(chenye kurasa 160 kwa Euro 14).

Kitabu kipya cha Mtaalimungu wa Shirika la Wadominikani, ambaye alipewa jukumu la kutafakari kwa  kwa ajili ya ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa kwanza Maalum uliyoitishwa na  Baba Mtakatifu Leo XIV mnamo Januari 7 na 8, 2026, kinatoa tafakari pana juu ya utume wa Kanisa katika jamii za kisasa na njia yake ya mazungumzo. Katika ulimwengu uliojaa mgawanyiko, vita vinavyoendelea  na majeshi, na migogoro ya maneno inayozidi kuwa mikali, inayozidi kuongezeka kutokana na mitandao ya kijamii, kazi ya Kanisa ni ipi? Je, Injili ya wakati wote inaweza kuzungumza kwa njia mpya leo? Ni maswali tunayokutana ndani ya kitabu hicho.


Kutembea pamoja

Kardinali Timothy Radcliffe, mmoja wa waandishi wa kiroho wanaosomwa sana duniani, anaamini kwamba uwepo wa Kikristo ni zaidi ya wakati wowote mbebaji wa wema na mustakabali: "Katika utamaduni wa Magharibi wenye ubinafsi mkubwa, imani yetu ni kinyume cha utamaduni. Tunaamini kwamba kila mmoja wetu anaweza kuwa sisi wenyewe kikamilifu tu  ikiwa atakuwa kwa ajili ya wengine. Kuwa mwanadamu kunamaanisha kuwa na uhusiano."

Na hasa utekelezaji wa Sinodi ni njia ambayo Kanisa linataka kutimiza kwa uaminifu kazi yake ya kutangaza Injili kwa kila mtu: "kutembea pamoja" ambayo inamtazama kila mtu kwa huruma kubwa, kusikiliza kwa usikivu, na roho ya urafiki. Kardinali Radcliffe anamtazamo wake  kuanzia sinema hadi Taalimungu, riwaya za kisasa hadi Mababa wa Kanisa, ili kutusaidia kufurahia uhai usio wa kawaida ambao mawazo ya Kikristo yanaweza kuupatia ulimwengu. Kurasa hizi, zenye nguvu ya imani na hekima tele, ni uthibitisho mpya na wa kuvutia kwa hili.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

22 Januari 2026, 16:49