Kard.Krajewski:Tunapaswa Kuwasaidia Waukraine Wanaoteseka
Na Svitlana Dukhovych & Benedetta Capelli – Vatican.
Mwanga wa mshumaa unaonesha kwa upole uso wa mama aliyemshika mtoto wake, akiwa amevikwa blanketi nyingi ambazo huficha viungo vyake. Inaweza kuonekana kama picha iliyojaa huruma, lakini inafichua maafa ya watu wa Ukraine, ambao kwa miaka mingi hawajajua amani. Watu wa Ukraine kwa sasa wanaishi katika giza, hali joto ikiwa chini ya sifuri, bila joto, wala umeme kwa sababu ya uvamizi mkali wa Warusi kwenye mji mkuu Kyiv- uvamizi wa hivi karibuni ulifanywa usiku kucha.
Kardinal Konrad Krajewski,(Krayeski), Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo, alizindua wito maalum kwa nchi “iliyomwaga damu” kwa vita, nchi ambayo ameitembelea walau mara kumi kwa niaba ya Baba Mtakatifu. Kardinali huyo ambaye ni mzaliwa wa Poland, ametembelea mara kadhaa Ukraine kwa ajili ya kuwafikishia huduma ya chakula, nishati kwa njia ya generata, na hata kuwapatia magari kwa ajili ya wagonjwa(ambulance), ameelezea ukaribu wa Kanisa kwa matendo na pia kuwasaidia kwa njia ya sala.
Wito wa Upendo
“Hakuna anayepaswa kwenda kinyume na maumivu, kwa wanaoteseka, lazima tufanye kitu,” alihimiza Kardinali, kwa sababu kuna hatari kama alivyosema Papa Leo XI, kuwa “utandawazi wa ukosefu wa Uwezo” hata zaidi ya “utandawazi wa kutokujali.” “Sisi kama wakristo,” ni lazima tufanye kitu, aliongeza Kardinali Krajewski,(Krayeski) hii ina maana ya Kanisa kuwapatia mahitaji watu wa Ukraine, hasa kutoka Roma, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Sophia, mahali ambapo malori yaliyobeba misaada kutoka Baraza hili la Kitume huanzia safari, misaada iliyotolewa na watu wakarimu na wenye mapenzi mema. Kwa sasa tunaalikwa kupelka kupitia Njia ya Boccea 478, Jijini Roma vifaa kama vile: vitakasa mikono, miguu, nguo za joto, soksi za joto, blanketi za joto na za dharura, chupa za joto; Karanga na chocolate pia zinaweza kutolewa kama sehemu ya msaada. “Kila mchango” linabainisha Kanisa Kuu la Mtakatifu Sophia, likimaanisha chochote chenye kutia mwili joto, chakula na hata nafasi ya kuishi tena kwa wale wanaohitaji.”
Caritas -Spes Ukraine: Matatizo Makubwa
Padre. Vyacheslav Hrynevych, Mkurugenzi mtendaji wa Caritas Ukraine, aliunga mkono ombi la Kardinal Krajewski(Krayeski). “Ni vyema tusielekeze macho yetu mbali kwa kile kinachoendelea Ukraine,” Padre alizungumza na Vatican News, “siyo kufikiria kama vita ya mbali au mzozo rahisi kati ya nchi zingine katika mipaka ya nchi za Ulaya. Ni lazima kusimama upande wa wahitaji, wale wanaotamani walau kuishi maisha ya kawaida na kuona siku zijazo. Padre Vyacheslav alizongumzuzia magumu mengi ambayo yanahitaji majibu ya haraka kwa wahitaji, katika hali hii ambayo imekuwa ngumu kwa siku za hivi karibuni kwa ajili ya Urusi kushambulia miundombinu.
Ustahimilivu na Uvumilivu
Kinachozidisha hali hiyo ni joto la chini sana, usiku joto hushuka mpaka hasi -15 degrees chini ya kipimo cha Celsius, wakati wa mchana inaweza kuwa kati ya nyuzi joto 10-12 hasi. Baada ya mgomo wa usiku Januari 19-20, kwenye mji mkuu majengo 5,635 yaliachwa bila umeme, karibu ya majengo hayo asilimia 80 ya majengo haya yalikuwa ndiyo yamemalizika tu kufanyiwa ukarabati. “Watu wengi,” alieleza, “wanalazimika kutafuta malazi au kwa muda kuacha nyumba zao, siyo kukimbia au kukwepa mabomu bali pia kwa sababu ya baridi.” Maisha ya kila siku, yanazidi kuwa magumu: kwenda kazini, kwa mfano, siyo rahisi kwa sababu lazima barabara zisafishwe kuondoa theluji na barafu, hivyo magari na treni haziwezi kwenda kwa kasi kwa sababu ya ukosefu wa umeme unaohitajika kwa ajili ya huduma hii.
Ni “mapambano ya kutafuta kuishi” alisema Mkurugenzi wa Caritas, ambaye hata hivyo anaangazia nguvu za watu wa Ukraine: uthibiti na msimamo. Tunapoona jinsi watu wanavyotenda hata wakati wa mlipuko wa mabomu au kukatika kwa umeme kwa muda mrefu, wakati wanakuja pamoja, wanapotaka wasaa wa kushirikishana-tunang’amua ya kuwa sisi ni watu wenye ujasiri. Watu wanajua namna ya kushirikishana na kusaidiana.”
Sehemu ya “Ustahimilivu”
Kwa hiyo ubinadamu unapinga vitisho vya vita na hii ni motisha kwa kazi ya Caritas kujibu kwa upendo mahitaji ya watu. Mfano, Padre Vyacheslav Hrynevych alieleza inawezekana kufunga generata ili kuhakikisha kugawa chakula cha moto kwa watu wa Kyiv mara kadhaa kwa Juma. “Kila mara,” alisisitiza Padre, “walau watu 200 wanafika kupokea chakula.” Kwa jinsi siku zinavyoenda, mahitaji nayo yanaongezeka, awali, wahitaji walitegemea jiko la supu, lakini kwa sasa idadi ya watu wanaogeukia kwao inaongezeka. Caritas-Spes Ukraine inahitaji usaidizi kuwafikishia huduma “wale wasioweza kutoka katika makazi yao, kuwapatia makazi yenye joto, hata ikiwa ni kwa masaa machache tu,na kuwasaidia kustahimili baridi.” Mkurugenzi alieleza kuwa, huko Kyiv, wametenga “eneo la ustahimilivu,” eneo lenye generete lenye uwezo mkubwa wa kuchaji vifaa vya umeme, kuwaka na joto na kupata kinywaji cha joto.
Ubunifu
Mpango huu pia umepanuliwa hadi Kharkiv, ambapo Caritas-Spes-Ukraine pamoja na miradi ya kujumuisha upya nafasi za kazi na ujenzi wa nyuma- imepanga usambazaji wa vyakula vya moto na kuanzisha kituo ambapo watu wanaweza kupokea msaada wa kimwili na kujipasha moto. Padre Vyacheslav aliongeza kuwa, “Kati ya watu 100 hadi 150 wanakaribishwa.” “Hali bado inaendelea kubaki kuwa tete: Kyiv ina wakaazi milioni miatatu mpaka mia nne, na asilimia 50 ya majengo katika mji huu yanabaki bila joto. Waasi pia wanaharibu miundombinu, na baridi inaharibu zaidi – kuna hatari kubwa ya kupooza kabisa.” Parokia zinajaribu kujipanga zenyewe, kwa usaidizi wa Askofu Vitalii Kryvytskyi, Askofu wa Kilatin Kyiv-Zhytomyr, kila mmoja anafungua makazi katika maeneo yao. “Pia tunatathmini,” mkurugenzi wa Caritas aliendelea, “uwezekano wa kufunga mahema yaliyopashwa moto.” Parokia mojawapo pia imeanzisha kituo kwa ajili ya kufua nguo za jamii, hivyo watu wanaweza kufua nguo zao.”
Majira ya Baridi ya Kikatili
Changamoto inayotokana na mshikamano na ukaribu pia inaelezewa na Padre Taras Zhephlinsky, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano ya Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiukreni. Katika video iliyotumwa kwa Vatican News, inasimulia shida za kila siku zinazowakabili wakaazi wa Kyiv, waliochoshwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi “dhidi ya mitambo ya nishati” huku pia akizungumzia faraja inayohisiwa na wale ambao hawajisikii kuacha.
Uso wake pia, unaanza na mwanga hafifu wa mshumaa na mapambo ya Noeli nyuma yake, yenye kubeba ujumbe “kukataa kujisalimisha kwa giza la vita,” ambalo Padre huyo alieleza, “mwaka 2025, kulishuhudia idadi ya waadhiriwa ikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 ikilinganishwa na 2024, kulingana na utafiti wa Umoja wa Mataifa. “Hii ni baridi kali sana hasa kwa miaka ya hivi karibuni,” alisisitiza katika video hiyo, pamoja na halijoto kuwa chini ya nyuzi 156, tumekuwa bila umeme, alieleza. Takribani majengo 6,000 hayana joto, baadhi ya vitongoji katika mji mkuu hata maji havina. Katika kanisa kuu la Ufufuko wa Kristo, mjini hapo anasema, linaweza tu kuwasha taa za juu, maduka yamefungwa,kwa sababu generata haliwezi tena kufanya kazi.
Kuwalinda Watoto
Historia ya huko Kyiv, inaweza kuishia hapa anasema Padre Taras pia hutazama furaha inayotokana na mambo madogo au makubwa kwa sababu ya furaha ya kuwa mtu wa Mungu. “Katika siku hizi za hatari na giza, kwenye moja ya familia za padre wetu mtoto wa tatu amezaliwa, mtoto wa kiume. Furaha ya kweli inakuwa kazi yetu. Tunajisikia kuwa na wajibu wa kulinda kwa nguvu zertu zote maisha yam toto, kama maisha ya mamilioni ya wa watu wengine wa Ukraine na watoto. Katika kutekeleza jukumu hili, Kanisa la Ukraine, hatupo peke yetu: tunajisikia kuungana na kanisa la ulimwengu, upendo na ukarimuu wa Papa Leo XIV, na ukarimu wa wale wote wanaotukumbuka.”
Maneno yake ya Mwisho yana Matumaini na Mwelekeo
“Sisi Waukreini,” alisema, ni bahati mbaya kuwa tunapitia kipindi hiki cha baridi na katika mashambulizi haya tutashinda giza lote linaloletwa na vita, kkwa kuwa tunatambua kuwa hatujaachwa peke yetu. Tumemkaribisha mkombozi aliyezaliwa kwentu Noeli, na kama nabii Isaiya alivyotabiri, “Watu wale waliotembea katika giza wameuona mwanga, mwanga mkuu umewashukia, katika giza kuu Nuru imewaangazia.” “Tupo gizani na katika uvuli wa mauti,” alihitimisha, “lakini kati yetu mwanga umetuangaria, mwanga wa Kristo na mwanga wa mshikamano wenu ulimwenguni kote.” “Asante yake ya mwisho ni ukarimu wa ulimwengu wote, kutegemeza na ukarimu wa dhati kwa “mikono iyoyoganda baridi, nyuso na nyumba zetu,” joto ambalo ni Upendo wa Kimungu, alihitimisha.