2021.09.14 TRASFERIMENTO da Bratislava a Košice.

Gallagher nchini Slovakia kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 25 ya Mkataba na Vatican

Kuanzia Januari 30,hadi Februari 1,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa anatembelea Jamhuri ya Ulaya ya Kati na Mashariki.Programu hiyo inajumuisha mikutano ya kitaasisi na kidiplomasia,Kongamano katika Chuo Kikuu kikubwa zaidi nchini,ziara ya Nitra,na Misa ya kufunga katika Kanisa Kuu la mji mkuu.

Vatican News

Kuanzia, Januari 30, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, yuko Slovakia kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya Mkataba wa Msingi kati ya Vatican na Jamhuri ya Slovakia.

Ziara hiyo itaendelea hadi Dominika Februari 1. Siku imepangwa kufanyika kuanza Ijumaa Februari 30 kama ilivyoelezwa katika programu iliyochapishwa kwenye akaunti ya X ya Sekretarieti ya Vatican @TerzaLoggia, na Mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje, Juraj Blanár, na ziara ya heshima kwa Rais wa Jamhuri, Peter Pellegrini, utahitimisha siku hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Slovakia na Askofu Mkuu Gallagher
Waziri wa Mambo ya Nje wa Slovakia na Askofu Mkuu Gallagher

Siku hiyo itahitimishwa kwa mkutano na Kikosi cha Kidiplomasia katika Baraza la Wawakilishi.

Wakati Jumamosi tarehe 31 Januari 2026, ratiba  itajumuisha ushiriki katika Kongamano kuhusu Mkataba wa Msingi katika Chuo Kikuu cha Comenius, ikifuatiwa na ziara katika jiji la Nitra.

Siku ya Dominika tarehe Mosi Februari 2026, Misa Takatifu itaadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Martin huko Bratislava.

30 Januari 2026, 14:26