Codex   ya Kale  katika maktaba ya mjini Vatican. Codex ya Kale katika maktaba ya mjini Vatican. 

‘Codex’ ya Kilatini ya Palatine katika Maktaba ya Vatican

Hati hii muhimu ilipatikana hivi karibuni kutoka duka la vitabu la Vienna.Codex,yaani Hati ya kale yenye karatasi nyingi zilizokunywa katika kitabu ina maisha ya watakatifu watano na Historia ya Langobardorum ya Paulo Diacono.

Vatican News

Katika majuma yaliyopita, katika duka la vitabu “Inlibris” la  Hugo Wetscherek, huko Vienna, Maktaba ya Kitume Vatican, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, kwamba  Maktaba ya Vatican  iliweza kupata (Codex),Hati ambayo awali ilikuwa  mojawapo ya makusanyo yake, Mkusanyo wa Kilatini wa Palatine. Kitabu hicho kilikuwa kimevutia umakini wa Mkurugenzi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Heidelberg, Dk. Jochen Apel, ambaye kisha alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Maktaba ya Vatican, Padre Mauro Mantovani. Ni Hati ya mkono ya karatasi yenye kurasa 115(pamoja na karatasi ya kulinda), historia ya maisha ya Watakatifu watano(Cyriacus, Gallus, Maurus Abbot, Goar, Burchard Askofu wa Worms) na Historia Langobardorum iliyoandikwa na Paul Diacono; kuhusiana na maisa ya watakatifu, (Codex)yaani Hati hiyo inajitokeza  uhaba wa yale yanayothibitisha.

Kazi ya waandishi kadhaa, ilitengenezwa Ujerumani, labda huko Worms, ambapo labda uchaguzi wa maandishi ya hagiografia unaonekana kutegemea, mwanzoni mwa karne ya 16. Kifuniko kilichofunga hati hiyo kinaonesha cha 1556 ambacho kimehifadhi mabamba mawili yenye picha ya Mteule Palatine Ottheinrich. Umuhimu wa ununuzi huo unatokana hasa na ukweli kwamba (Codex ), hati  hiyo inatambulika kama ile iliyo katika Maktaba ya Vatican iliyoandikwa Pal. lat. 851, ambayo, pamoja na mingine, ilionesha kukosekana wakati wa kusasisha kunako 1798. Ilikuwa imefika hapo mwaka 1623, baada ya safari ngumu iliyoratibiwa na Leone Allacci, Scriptor Graecus wa Maktaba ya Vatican, pamoja na hati zingine kutoka Maktaba ya Palatine, zilizotolewa na Maximilian I wa Bavaria kwa Papa Gregori XV kwa shukrani kwa msaada wake wakati wa Vita vya Miaka Thelathini.

Tendo la kutoa, sababu za mchango huo, na mpangilio wa nafasi za kuiweka zimeandikwa katika epigrafu ambayo bado inaonekana katika Jumba la Pango Hifadhi la Urbano VIII, sasa katika Makumbusho ya Vatican. Historia ya maktaba ya Maktaba ya Palatine, kuanzia kuwasili kwake Vatican hadi mahali pake pa mwisho, inaweza kujengwa upya kupitia orodha, ambazo pia zinathibitisha utambuzi wa Pal. lat. 851. Zaidi ya hayo, kwenye karatasu za juu, saini na mabamba mbalimbali ya vitabu yanathibitisha uhamisho na mauzo yake miongoni mwa wakusanyaji mbalimbali, kuanzia mwishoni mwa karne ya kumi na nane hadi sasa (Frederick North,Mfale wa tano wa Guilford, Sir Thomas Phillips, Maurice Burrus).

Kwa hivyo, operesheni muhimu ya kiutamaduni na kisayansi, ilikamilishwa katika siku chache tu kutokana na kazi ya wote waliohusika—Maktaba ya Chuo Kikuu cha Heidelberg, Maktaba ya Vatican, na duka la vitabu la Inlibris, ambao walitekeleza mpango huo pamoja na utayari, maelewano, na taaluma, wakiongozwa na hamu ya pamoja ya kuifanya hati hiyo ipatikane kwa wasomi katika maktaba, na hasa katika ile inayohifadhi umiliki wa hati hiyo.

Ushirikiano kati ya Maktaba ya Ujerumani na Maktaba ya Vatican si jambo jipya; umekuwa ukifanywa upya kila mara baada ya muda kupitia hafla na mipango ya kisayansi: kutoka katika mpango wa Leo XIII, ambaye mnamo 1886, katika hafla ya maadhimisho ya miaka 500 ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha jiji hilo, alituma orodha za kwanza za Maktaba ya Palatine zilizochapishwa mahsusi kwa kusudi hili kwa Heidelberg, kwa sherehe hizo miaka 100 baadaye, wakati idadi kubwa ya Vitabu vya  Vatican vilipoazimwa ili kuoneshwa katika maonyesho yaliyowekwa huko Heiliggeistkirche, hadi 2010, wakati Vatican ilipozindua kampeni ya kidijitali ya hati za mkono(digi.vatlib.it).

Mpango mkuu ahasa ulikuwa unashikirishwa na Universitätsbibliothek ya Heidelberg ( Maktaba ya Palatine – digital: https://digi.ub.uni-heidelberg.de/de/bpd/index.html),kwa lengo la kulinda ushuhuda wa thamani wa zamani, na kuufanya upatikane zaidi katika wakati uliopo na kuuhifadhi kwa ajili ya wakati ujao. Historia zinazoendelea kuingiliana katika huduma ambayo Vatican inatoa kwa wanadamu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku.Just click here

26 Januari 2026, 11:06