2026.01.10 Sanda: Uliwakilishwa Mpango wa "Avvolti" kwa Papa wa Torino. 2026.01.10 Sanda: Uliwakilishwa Mpango wa "Avvolti" kwa Papa wa Torino. 

"Avvolti"ni mpango uliowakilishwa kwa Papa wa usomoji wa Sanda kupitia mfumo wa kidijiatali

Wakati wa Mkutano mjini Vatican kati ya Kardinali Repole na Papa Leo XIV,Januari 9,Papa alikuwa wa kwanza kukubali mpango uliozinduliwa wa Jimbo Kuu la Torino kwa ajili ya Jubilei ambayo unaruhusu"kusafiri"kuptia picha za Sanda Takatifu kwa kutumia kila kifaa chochote cha kielektroniki na kutokea mahali popote Ulimwenguni.

Vatican News

Sanda ni kama ambavyo haijawahi kuonekana hapo awali. Tarehe 9 Januari 2026, Baba Mtakatifu  Leo XIV alikuwa wa kwanza kujiunga na mpango uitwao Avvolti yaani Aliyefunikwa, ulioundwa na Jimbo Kuu la Torino nchini Italia kwa ajili ya Jubilei, ambao unatoa uzoefu wa usomaji wa kidijitali wa picha za Sanda Takatifu ya Torino, unaopatikana mtandaoni duniani kote. Programu hiyo iliwasilishwa kwa Papa na Mlinzi wa Kipapa wa Kanisa Kuu linalohifadhi Sanda Takatifu, Kardinali Roberto Repole, Askofu Mkuu wa Torino, wakati wa Mkutano iliyohudhuriwa katika Jumba la Kitume mjini  Vatican.

Kuleta umma karibu na Sanda

Programu hii ni ya kwanza: itawezekana kuunganishwa na programu hiyo mtandaoni kutoka katika  tovuti:www.avvolti.org  kama pia Tofuti rasimi:www.sindone.org , kwa kutumoa kifaa chochote:( smartphone, tablet, pc) yaani simu mahiri ya mkono, kompyuta kibao, Kompyuta kamili, yenye ufikiaji wa kimataifa ya Kieletroniki. Shukrani kwa programu hii, unaweza "kutembelea" picha ya Sanda Takatifu kwenye skrini yako, na kuongeza maelezo muhimu zaidi (Uso, Taji la Miiba, n.k.). Kila upanuzi unaambatana na maelezo na viungo vya vifungu vya Injili vinavyoelezea Mateso ya Yesu. Usomaji wa kidijitali unakusudiwa kuleta umma kwa ujumla, duniani kote, karibu na picha ya Sanda Takatifu na maana zake. “Licha ya ukali wa kisayansi wa maandishi na picha, tumejitahidi kuunda bidhaa inayoweza kufikiwa na wote, badala ya mpango unaolenga wataalamu.”

Uzoefu wa Kidijitali wa Kimataifa

Kardinali Repole alikumbusha kwamba uchapishaji wa uzoefu wa kidijitali wa kimataifa ni sehemu ya mpango wa "Sanda ya Uchungaji" ambao Kanisa la Torino ulizindua mwaka  2024, ambao Avvolti imekuwa msingi wa Mwaka wa Jubilei 2025. Mipango mingine itapangwa na kuendelezwa katika miezi ijayo, ili kuunda safari ya kusindikiza kuelekea Jubilei ya 2033. Kipindi cha masika iliyopita ya 2025, hema la Avvolti liliwekwa kwenye Uwanja wa Castello huko Torino,  kwa njia hiyo miongoni mwa vipengele vingine, hema hilo liliwasilisha usomaji wa kidijitali wa Sanda, likitoa picha hiyo kwa kipimo cha 1:1 kwenye meza yenye urefu wa mita 5 iliyoundwa maalum. Hema hilo lilitembelewa na zaidi ya watu 30,000 kutoka nchi 79 wakati wa ufunguzi wake wa siku nane (Aprili 28 hadi Mei 5).

Programu iliyowasilishwa mezani, ikiwa imebadilishwa ipasavyo, sasa inapatikana kwa kila mtu mtandaoni. Picha na maandishi kutoka kwa uzoefu yanaweza kupatikana kwenye tovuti www.avvolti.org na kwenye mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram,).

10 Januari 2026, 17:00