Padre Joseph Francis Badji ameteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo Katoliki la Kolda nchini Senegal. Padre Joseph Francis Badji ameteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo Katoliki la Kolda nchini Senegal.  (@Vatican Media)

Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji Jimbo la Kolda, Senegal

Papa Leo XIV amemteua Mheshimiwa Sana Padre Joseph Francis Badji kuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo Katoliki la Kolda nchini Senegal. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Majimbo ya “Saint Jean Marie Vianney” iliyoko Brin, Ziguinchor. Itakumbukwa kwamba, Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji wa Jimbo Katoliki la Kolda, alizaliwa tarehe Mosi, Januari 1966 huko Ziguinchor.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumamosi tarehe 10 Januari 2026 amemteua Mheshimiwa Sana Padre Joseph Francis Badji kuwa Askofu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo Katoliki la Kolda nchini Senegal. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Majimbo ya “Saint Jean Marie Vianney” iliyoko Brin, Ziguinchor. Itakumbukwa kwamba, Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji wa Jimbo Katoliki la Kolda, alizaliwa tarehe Mosi, Januari 1966 huko Ziguinchor, nchini Senegal. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 28 Desemba 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji, Jimbo la Kolda, Senegal
Askofu Mwandamizi Joseph Francis Badji, Jimbo la Kolda, Senegal   (@Vatican Media)

Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza dhamana na wajibu wake wa Kikasisi kama Paroko usu Kanisa kuu la “Notre-Dame des Victoires, huko Kolda kati ya Mwaka 1994-1997); Jalimu na Mlezi wa Seminari ya “Saint Jean Marie Vianney” kwa kipindi cha Mwaka 2001; Mkurugenzi wa Majiundo Endelevu ya Mapadre tangu mwaka 2011 hadi mwaka 2016. Na tangu mwaka 2017 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu Mwandamizi alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Majimbo ya “Saint Jean Marie Vianney” iliyoko Brin, Ziguinchor.

Senegal
10 Januari 2026, 17:49