Askofu Sithembele Anton Sipuka wa Jimbo Katoliki la Umtata ameteuliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Cape Town, nchini Afrika ya Kusini. Askofu Sithembele Anton Sipuka wa Jimbo Katoliki la Umtata ameteuliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Cape Town, nchini Afrika ya Kusini. 

Askofu Mkuu Sithembele Anton Sipuka Jimbo Kuu la Cape Town, Afrika ya Kusini

Askofu mkuu mteule Sithembele Anton Sipuka wa Jimbo kuu la Cape Town, alizaliwa tarehe 27 Aprili 1960, huko Idutywa, Jimbo la Queen. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Desemba 1988 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 8 Februari 2008, Papa Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Umtata, Afrika ya Kusini na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 3 Mei 2008., tarehe 10 Januari akateuliwa kuwa Askofu mkuu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 9 Januari 2026 amemteuwa Askofu Sithembele Anton Sipuka wa Jimbo Katoliki la Umtata kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Cape Town, nchini Afrika ya Kusini. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Sithembele Anton Sipuka wa Jimbo kuu la Cape Town, alizaliwa tarehe 27 Aprili 1960, huko Idutywa, Jimbo la Queen. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Desemba 1988 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 8 Februari 2008, Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Umtata, Afrika ya Kusini na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 3 Mei 2008.

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM

Kati ya Mwaka 2019 hadi Mwaka 2024 alichaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini “Southern African Catholic Bishops’ Conference (SACBC), na kati ya Mwaka 2019 hadi Mwaka 2022 alichaguliwa kuwa ni Makamu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katokiki Afrika na Madagascar, SECAM, ambalo kimsingi ni matunda ya Maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Tarehe 4 Julai 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV akamteuwa kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini.

Cape Town

 

10 Januari 2026, 18:11