Askofu Mkuu Caccia,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa. Askofu Mkuu Caccia,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa.  

Ask.Mkuu Caccia:Kufufua Azimio la Maadili la Dunia Dhidi ya Uhalifu wa Ubinadamu

Katika ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Kidiplomasia wa Umoja wa Mataifa kuhusu:“Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu,Askofu Mkuu Gabriele Caccia,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa,huko New York,alithibitisha tena uungaji mkono mkubwa wa Vatican wa mfumo mzuri wa kimataifa wa kushughulikia uhalifu huu mkubwa.

Na Sr. Christine Masivo,CPS, – Vatican.

Mnamo  tarehe 19 Januari 2026, huko  jijini New York, wakati muhimu na wa kutia moyo ulitokea katika Ofisi za Umoja wa Mataifa wakati Kamati ya Maandalizi ilipokutana kwa Kiikao cha Kwanza kabla ya Mkutano wa Kidiplomasia kuhusu mada ya “Kuzuia na kuadhibu uhalifu dhidi ya ubinadamu.” Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican, katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa alitoa hotuba yake wakati muafaka na wa kushawishi kimaadili, ikiikumbusha Jumuiya ya Kimataifa kwamba mafunzo mabaya zaidi ya kihistoria yanabaki kuwa mambo ambayo hayajakamilika.

Wito Uliojikita katika historia, uliopywaishwa na migogoro ya leo

Katika hotuba yake Askofu Mkuu Caccia Aliweka mijadala ya sasa ya Umoja wa Mataifa katika mwendelezo mrefu wa kimaadili na kisheria. Kwa kukumbuka Wito wa Papa Pio XII kunako 1953 kuhusu makubaliano sahihi ya kimataifa kufuatia ukatili wa Vita vya Pili vya Dunia, alisisitiza kwamba kushindwa kutekeleza kikamilifu maono haya bado ni jambo la dharura. Zaidi ya miongo saba baadaye, vurugu zilizoenea dhidi ya raia zinaendelea kuumiza jamii na kupinga dhamiri ya maadili ya ubinadamu. Askofu Mkuu Caccia  alibainisha kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu hauzuiliwi na zamani tu. Katika maeneo mengi, watoto, wanawake, na wajumbe wa makabila madogo na kidini bado wanakabiliwa na mateso na vurugu za kimfumo. Ukweli huu unaongeza umuhimu wa kazi ya Kamati ya Maandalizi na kuakisi gharama ya kutochukua hatua katika ngazi za Kitaifa na Kimataifa.

Kutoka utambuzi wa kisheria hadi uzuiaji ufanisi

Ingawa uhalifu dhidi ya ubinadamu tayari umepigwa marufuku chini ya sheria za kiutamaduni za kimataifa, Vatican ilisisitiza kwamba utambuzi wa kisheria pekee hauhakikishi ulinzi. Jukumu kuu mbele ya jumuiya ya kimataifa ni kuimarisha mifumo ya kuzuia na uwajibikaji. Hii ni pamoja na kuhakikisha kwamba wahalifu wanawajibika na kwamba mifumo ya haki ina uwezo wa kujibu kwa ufanisi wakati uhalifu kama huo unapotokea.

Askofu Mkuu Caccia alisisitiza kwamba chombo chochote cha kisheria cha siku zijazo kinapaswa kujengwa juu ya sheria ya kimataifa iliyopo. Kudumisha mshikamano wa kisheria ni muhimu ili kudumisha uaminifu miongoni mwa Mataifa na kufikia makubaliano mapana. Katika muktadha huo, uwazi wa lugha na uelewa wa pamoja wa dhana za kisheria uliakisiwa kama msingi wa mazungumzo na ushirikiano wenye maana.

Jukumu kuu la mataifa na haja ya ushirikiano

Hotuba hiyo ilithibitisha tena kwamba Mataifa yana jukumu la msingi la kuzuia na kushtaki uhalifu dhidi ya binadamu. Mamlaka ya kitaifa yanabaki kuwa njia ya kwanza na muhimu zaidi ya haki. Wakati huohuo, ushirikiano wa kimataifa una jukumu muhimu la kukamilishana, hasa katika kesi zinazohusisha uhalifu wa mipakani au ambapo uwezo wa kitaifa ni mdogo. Ushirikiano kama huo, kwa mujibu wa Askofu Mkuu alibainisha, lazima uheshimu kanuni za kukamilishana, mchakato unaofaa, na haki za msingi za binadamu. Juhudi za kimataifa zinapaswa kuimarisha, badala ya kuchukua nafasi ya, mifumo ya kisheria ya kitaifa, kuhakikisha haki na uhalali katika kesi zote.

Kuwaweka waathiriwa katikati

Kipengele muhimu cha uingiliaji kati wa Vatican, kilikuwa ni mkazo wake kwa waathiriwa. Mateso yao hayahitaji tu uwajibikaji, bali pia ulinzi, usaidizi, na utambuzi wa utu wao. Mifumo ya kisheria ya siku zijazo, Askofu Mkuu Caccia alisema, lazima ihakikishe kwamba waathiriwa na mashuhuda wanalindwa na kupewa sauti inayofaa, huku wakiheshimu kikamilifu viwango vya haki vya kesi.

Kutazama mbele kwa uwajibikaji na matumaini

Kamati ya Maandalizi inapoanza kazi yake, Vatican ilielezea kujitolea kwake kwa ajili ya mazungumzo ya wazi kama dira ya maadili na wito wa kuwajibika na yenye kujenga. Askofu Mkuu alihitimisha kwa kuwasihi wajumbe wote kushiriki, kwa lengo la pamoja la kukuza mwitikio wa kimataifa unaofaa, unaoaminika, na wa kudumu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

ASK MKUU CACCIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

22 Januari 2026, 17:36