Picha na maneno ya Papa yanaakisi jiji la Milele kwa ajili ya Noeli
Vatican News
Badala ya matangazo ya kawaida yenye rangi angavu ya vifurushi vya usafiri na sikukuu, picha za Papa Leo XIV zinatawala sehemu za mbele za majengo ya Roma yote. Kwa siku kadhaa, picha hizi zimeonekana kwenye skrini kubwa katika Jiji lote la Milele, zikiakisi maeneo ya umma kama vile Uwanja wa Risorgimento, kona ya Njia ya Ottaviano, na Njia ya Tunisi mbele ya Makumbusho ya Vatican. Maonesho hayo yana picha na tafakari zilizochukuliwa kutoka katika hotuba zake, zikitoa ujumbe kwa ajili ya kipindi cha Noeli na mwaliko wa matumaini. Kampeni ya Noeli inaendelezwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na Selfiestreet, kwa kutumia skrini kubwa zilizowekwa karibu na Vatican.
Picha za Papa kwenye mabango katika jiji la Roma
Wapita njia mara nyingi wanasimama kusoma jumbe zilizooneshwa kando ya picha za Papa akiwa na waamini na mahujaji wa Jubilei. Mpango huo, unaoendelea hadi Desemba 31, pia unashirikiswa sana kwenye mitandao ya kijamii. Kulingana na taarifa, "uwepo wa ujumbe wa Baba Mtakatifu katika maeneo ya umma wakati wa Noeli unatumika kama ishara ya ukaribu wa kiroho na ukumbusho wa maadili ya amani, matumaini, na udugu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku, bofya hapa tu: Just click here