Kutangazwa kuwa mwenyeheri shahifi wa Hungaria. Kutangazwa kuwa mwenyeheri shahifi wa Hungaria.  (ANSA)

Mária Magdolna Bódi:mwenye haki na Mtakatifu anaweza kuwa kitovu cha kiroho na msaada wa jumuiya nzima

Huko Veszprém,Hungaria,Kardinali Erdő alimtangaza kuwa mwenyeheri mwanamke kijana ambaye aliuawa mnamo 1945 na askari wa Jeshi Nyekundu baada ya kujaribu kupinga jaribio la ubakaji.Haikuwa bahati mbaya isiyotarajiwa,lakini kilele cha maisha ya kujitolea.

Vatican News

"Mfiadini wa usafi wa moyo:" hivi ndivyo Kardinali Péter Erdő, Askofu Mkuu wa Metropolitan Esztergom-Budapest, alivyoeleza Mária Magdolna Bódi, ambaye alimtangaza mwenyeheri asubuhi ya Jumamosi, tarehe 6 Septemba 2025, huko Veszprém, Hungaria. Akiongoza ibada ya misa Takatifu ya kumwakilisha Baba Mtakatifu  Leo XIV, Kardinali huyo alijikita  tena hatua kuu za maisha ya mwanamke huyo kwa kina, aliyeuawa mnamo 1945, akiwa na umri wa miaka 24 tu, mikononi mwa askari wa Kisoviet. Umri ule ule ambao Pier Giorgio Frassati alikufa, na ambaye anatangazwa Mtakatifu siku moja baada ya kutangazwa kwa msichana wa Hungaria kuwa mwenyeheri. "Leo, kuzungumza juu ya usafi kunahitaji ujasiri," Kardinali alisema katika mahubiri yake.

"Kujitoa kwa usafi wa kiadili sio aina fulani ya shughuli kali, lakini chaguo kuu la upendo wa kibinafsi kwa Kristo." Kwa hivyo, alisisitiza ukweli kwamba "kila mtu, kulingana na hali yake, amepokea mwito wa usafi wa moyo, wanandoa kwa uaminifu; vijana kujitayarisha kwa nidhamu kabla ya maamuzi makubwa ya maisha yao; wale ambao wamekubali useja na ubikira wamepokea wito wa kujitoa kikamilifu kwa Kristo na huduma kamili kwa wanadamu."

Kuwawa kwa Maria

Mkuu wa Kanisa la  Hungaria aliongeza, "kuuwawa kwa Mária Magdolna, haikuwa bahati mbaya isiyotarajiwa, lakini taji la maisha ya vijana na ya kujitolea na ya dini kubwa na ya kujitolea ya Kikatoliki." Ijapokuwa alizaliwa katika hali ngumu na hakuweza kuwa mtawa kwa sababu wazazi wake hawakuwa wameoana, kijana alikuwa  na roho ya kitume" moyoni mwake, na kama mwanamke mlei, "alihisi nguvu ya neema." Akiwa mchapakazi kwa bidii katika kiwanda cha Fűzfő-Gyártelep, “aliona kuwa ni wito wake kuwaongoza watenda kazi wengine kwa Kristo,” kwa sababu hakuhisi “bidii ya kitume tu, bali pia upendo wa pekee” Kwake, akiwatia moyo wengine kufanya vivyo hivyo.

Kisha Askofu Mkuu wa Esztergom-Budapest alikumbuka jinsi mwanamke huyo kijana aliweza kumshawishi mwenzake aache kukufuru na jinsi mara nyingi alivyokuwa akiwaazima wengine viatu na koti ili waweze kuhudhuria Misa. Na alipohisi huzuni, aliingia kanisani na "kumwambia Yesu kila kitu," akipata faraja Kwake. Siku zote kutokana na upendo kwa Mwana wa Mungu, hakuweza kuwa mtawa, tarehe 26 Oktoba 1941, Siku kuu ya Kristo Mfalme, aliweka nadhiri ya ubikira wa milele.

Vita vya 1944

Mwishoni mwa 1944, Vita vya Pili vya Ulimwengu vilikaribia Litér, mji wa nyumbani kwa Mária. Vikosi vya Kisoviet vilifika mnamo tarehe 23 Machi 1945, wakati mwanamke huyo kijana pamoja na wanawake kadhaa na watoto, walikuwa kwenye mlango wa makazi. Askari wawili wa Kisoviet walimshambulia; alijaribu kujitetea kwa mkasi mdogo, kisha akajaribu kutoroka, akiwaonya wanawake wengine juu ya hatari hiyo. Lakini kilio chake kilinyamazishwa na risasi sita zilizopigwa na askari mmoja kati ya wale wawili. Katika risasi ya pili, Mária aliinua mikono yake mbinguni na kusema: "Bwana, Mfalme wangu! Nichukue pamoja nawe!" Kisha akafa.

Sadaka ya shahidi kijana, Kardinali Erdő alisisitiza, pia ilikuwa na "athari ya moja kwa moja kwa wale walio karibu naye": wanawake na watoto waliokuwa pamoja naye waliepuka hatari; Wazazi wake walioana, na mara baada ya kifo chake, sala nyingi zilijibiwa. Hii ni kwa sababu "mtu mwenye haki na Mtakatifu anaweza kuwa kitovu cha kiroho na msaada wa jumuiya nzima." Hatimaye, akimnukuu Mtakatifu Ambrose, mshereheshaji alilinganisha sura ya yule  Mwenyeheri mpya  na Mtakatifu Agnes, kwani katika wote  mawili, "kuna mashahidi wawili: wa usafi na wa imani." Alihitimisha.

06 Septemba 2025, 15:45