Mama Maria wa Fatima. Mama Maria wa Fatima.  (AFP or licensors)

Kard.Parolin,Ureno,anatembelea Fatima na Eneo la ajali huko Lisbon

Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican atakuwa nchini Ureno kuanzia Septemba 12,hadi Dominika Septemba 14.Atakuwa katika maombi katika eneo ambapo lift ya Glória iliacha njia katika mji mkuu wa Ureno na kusababisha vifo na majaeruhi, na atashiriki katika Jubilei ya Mamlaka za Kiraia.

Vatican News

Safari ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican nchini Ureno ilianza kwa kutembelea Madhabahu ya Fatima, mahali ambapo mamilioni ya mahujaji hufika kila mwaka kusali na kutoa heshima zao. Kwa njia hiyo Kardinali huyo atakuwa nchini kuanzia Septemba 12 hadi 14. Kulingana na mpango huo, uliochapishwa na Sekretarieti ya akaunti ya X ya Vatican @TerzaLoggia, Kardinali atakuwa katika Madhabahu ya Fatima tarehe 13 Septemba 2025 mahali ambapo atasali Rozari katika Kikanisa cha Tokeo la Mama Maria(Capelinha das Aparições).

Kardinali aidha atasafiri hadi Lisbon, ambako kituo cha maombi kimepangwa katika eneo la ajali ya (Funicolar da Glória), ya moja mojawapo ya lifti za kihistoria za jiji hilo, ambayo iliacha njia yake na kuanguka mnamo tarehe 3 Septemba 2025  na kusababisha vifo na majeruhi. Pia huko Lisbon, Kardinali Parolin atakutana na Waziri Mkuu wa Ureno, Bwana Luís Montenegro, na kushiriki katika Jubilei ya Mamlaka za Kiraia.

Siku hiyo hiyo, Kardinali Parolin ataongoza adhimisho la Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Fatima. Atafanya hata Ziara ya heshima kwa Rais wa Jamhuri, Marcelo Rebelo de Sousa Siku ya Dominika tarehe 14 Septemba 2025.

12 Septemba 2025, 16:00