Mji wa Vatican na Basilika ya Mtakatifu Petro. Mji wa Vatican na Basilika ya Mtakatifu Petro. 

Vatican:Kanuni ya Mikataba ya Umama na Zabuni imechapishwa

Tarehe 9 Agosti,imechapishwa Kanuni ya utendaji Mkuu,iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi,Vatican(SPE) na Sheria ya Utekelezaji wa Motu Proprio juu ya Sheria za Uwazi,Udhibiti na Ushindani katika Taratibu za Mikataba ya Umma ya Kiti Kitakatifu na Mji wa Vatican na Zabuni.

Vatican News

Amri kifungu tendaji cha 1/2025 ya Sekretarieti ya Uchumi ya Vatican(SPE)ambayo ina udhibiti wa utekelezaji wa Barua Binafsi ya Motu Proprio inayohusiana na "sheria juu ya uwazi, udhibiti na ushindani wa zabuni,  wa kukabidhiwa mikataba ya umma ya Kiti Kitakatifu na Jiji la Vatican iliyochapishwa mnamo tarehe 1 Juni 2020 na kurekebishwa na barua binafasi  ya Motu Proprio kwa ajili ya kuoanisha vizuri zaidi,  ya tarehe 16 Januari 2024, imechapishwa tarehe 9 Agosti 2025.

Amri hiyo, iliyosainiwa mnamo tarehe 5 Agosti 2025 na Mwenyekiti wa Sektratarieti ya Uchumi, Vatican(SPE), Maximino Caballero Ledo, imegawanywa katika Sura nane na vipengele 52, na inafafanua njia za utumiaji wa Motu Proprio kwa usahihi "ili kuunganisha bora zaidi", juu ya sasisho za kanuni ya mikataba ya Kiti kitakatifu, tunda la ushirikiano wa kimkakati kati ya Mabaraza mengine ya  Vatican ili kurahisisha  taratibu za usambazaji.

Sasisho hilo, likithibitisha malengo ya uwazi, udhibiti na ushindani katika mikataba ya zabuni ya umma iliyoingizwa na Kiti kitakatifu na Jiji la Vatican, ni sawa na kushughulikia kati ya waendeshaji wa uchumi na kutokuwa na msimamo kati ya wazabuni, hupendelea wakati wa hatua ya kiutawala na utekelezaji wa kanuni za ufanisi, ufanisi na uchumi kwa kufuata Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa Katoliki(KKK).

Na Gombo jipya la ununuzi, lilithamini uzoefu uliopatikana, sambamba na Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium (Hubirini Injili) imekusudia kuendana na mahitaji ya uwazi na udhibiti na hitaji la kuboresha kwa njia ya kiutendaji ambayo inaelekeza uchaguzi wa kiuchumi kwa lengo la kuongeza maadili na utumiaji endelevu wa rasilimali. Amri hiyo ilitangazwa kupitia uchapishaji wa Osservatore Romano na inaanza kutumika tangu tarehe 10 Agosti 2025, baada ya kuchapishwa kwenye Tovuti ya www.bandipubblici.va na kujumuishwa katika Acta Apostolicae Seis (Gazeti rasmi la Kiti Kitakatifu.)

Kanuni ya SPE

 

09 Agosti 2025, 14:09