Harakati ya kimataifa ya mazingira imebadili jina kuwa Harakati ya Laudato Sì
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Hamasisha na kuhimiza jumuiya ya Wakatoliki ili kutunza nyumba yetu ya pamoja na kuleta haki ya tabiachi na mazingira”, ndiyo malengo ya awamu mpya inaliofunguliwa kwa wanaharakati katololiki wa kutetea mazingira ulimwenguni, ambayo kwa sasa tangu tarehe 29 Julai 2021 imebadilisha jina lake kuwa “Hatakati ya Laudato Si’”. Harakati hii ilianzishwa mnamo 2015 na kikundi cha mashirika 17 Katoliki na wahamasishaji 12 wa Vyuo vikuu na mashirika ya kijamii kutoka mabara yote yaliyojitolea kusaidia waamini kujibu Waraka wa Papa Francisko juu ya utunzaji wa nyumba yetu ya Pamoja uliochapishwa mwaka huo huo. Harakati leo hii ina zaidi ya hali halisi ya washirika 800.
Katika nyakati za hivi karibuni harakati hii imefanya safari ya utambuzi inayodumu sasa kwa zaidi ya miezi 18, kwa mujibu wa ufafanunuzi uòiotolewa kwa Vatican News na Tomás Insua, mwanzilishi mwenza na mkurugenzi mtendaji wa ukweli huu. Ni tafakari juu ya utambulisho, utume, jina na miundo yake. Jina la awali amesema “lilikuwa refu sana na gumu kukumbukwa na kwa kufikiria kazi ya uongofu wa ekolojia na baada ya kuchunguza orodha ya majina 25 yanayowezekana, jina la “Harakati ya Laudato si '” ndilo likachaguliwa.
Lorna Gold, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, na ambaye ametoa habari mpya katika mkutano kwa njia ya mtandano, ameangazia jinsi ilivyo muhimu kutambua kwamba ujumbe umepanuliwa kujumuisha dhana ya haki ya ekolojia, kwa kuzingatia roho ya Laudato si ', ambapo 'kila kitu kimeunganishwa'”. Waraka wa Papa, ndiyo msingi wa kila kitu tunachofanya na kuandaa, kutoka Wiki ya Laudato si hadi Kozi kwa ajili ya wahamasishaji wa Laudato si ', kutoka kwa Duru zetu hadi kufika masomo maalum, ni ahadi ambayo haijawahi kukatika hata katika dharura ya mlipuko wa Covid, kiasi kwamba kuna wahuishaji elfu 25 wa Laudato Si 'ulimwenguni, watu wengi wanahusika katika ukweli wa parokia, ushirika na dini lakini pia watu wa kawaida ambao wanahisi kwa njia fulani wito wa kujumuisha ekolojia, wakijiweka katika huduma ya jamii yao”.
Aidha Bwana Insua amesema kuwa “bado kuna mengi ya kufanya, hasa leo hii: katika mwaka huu tunahitaji kuzingatia viongozi wakuu wa Umoja wa Mataifa”, akimaanisha Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Bioanuwai, Cop15, uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 11 hadi 24 Oktoba nchini China, na Mkutano wa UN juu ya Mabadiliko ya Tabianchi, wa COP26, utakaofanyika huko Glasgow kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 12 Novemba mwaka huu na ambapo pia kuna matazamio ya kufanya mkutano “Imani na Sayansi: Kuelekea Cop26”, utakaofanyika tarehe 4 Oktoba jijini Vatican na Roma.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa Harakati ya Laudato Si, ametafakari kuwa Viongozi wakuu wa UN, wana lengo la kuleta familia ya kibinadamu pamoja ili kuchukua hatua haraka mbele ya shida hizi kubwa: wanasayansi wanatuambia kuwa wao ni wa haraka zaidi mwaka baadaye mwaka. Kuna ishara nyingi, kwa mfano moto huko Sardinia, joto kali na moto nchini Canada, ukame huko Madagascar, kilio cha dunia na masikini ambacho kina nguvu zaidi. Kwa njia hivyo tunahitaji kuchukua hatua”. Sisi wa naharakati tupo tunasaidia kuhuisha mpango fulani. Na huo unaitwa “Sayari yenye afya, watu wenye afya '. Ni ombi na ukweli zaidi ya washirika 200 Kikatoliki kuzindua wito kwa viongozi wakuu washiriki wa UN, na itakuwa kipaumbele chetu katika miezi ijayo na hasa katika Wakati wa kipindi cha Kazi ya Uumbaji, kuanzia tarehe 1 Septemba. Tunaomba kuongeza kiwango cha shauku katika mipango miwili ijayo: hasa katika muktadha wa Cop26 amesisitiza Insua, kwani kuna mazungumzo juu ya kufikia uzalishaji wa gesi chafu sifuri kwa ngazi ya ulimwenguni kufikia 2050. Lakini tunajua kwamba nchi tajiri, ambazo zina jukumu la kihistoria, la karne nyingi za uzalishaji, zina uwezekano wazi wa kufanya mabadiliko tayari ifikapo 2035 - 2040”.
Kutoka kwa Papa kuna motisha wa kuendelea kujitolea kwa Harakati. “Tuliandika barua kwa Papa, tukimjulisha juu ya mchakato huo na kuomba maoni yake na baraka zake kabla ya kuendelea kubadilisha jina letu”. Hata hivyo Papa Francisko aliandika jibu fupi ambalo lilifika wakati wa masifu ya Pentekoste mnamo tarehe 22 Mei 2021 na ambayo ilikuwa ishara nzuri sana. Kwa kuzingatia kwamba mchakato huu ulikuwa na mazingira ya sala ya sinodi, ya kumwomba Roho Mtakatifu mwanga, maneno ya Papa yalifika katika sikukuu ya Pentekoste na ilikuwa ishara ambayo inatuhamasisha zaidi huku akituelekeza sisi wanaharakati wa Laudato Si; akitushukuru kwa utume wa kuhamasisha ekolojia fungamani na kwa msaada unaotolewa kwa Kanisa ulimwenguni, na kuongeza kutoa matashi mema kwa ajili ya Wiki ya Laudato Si ambayo ilikuwa ikiendelea siku hizo”. Msukumo mwingine muhimu alio utafakari mhusika huyo wa Harakati ya Laudato sì ni kuishi 'Laudato si ', ambayo haipaswi kubaki katika hati iliyoandikwa tu, kama maktaba, lakini iwe hati hai kabisa.