Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Joaquim Nhanganga Tyombe kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Uìje, nchini Angola. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Joaquim Nhanganga Tyombe kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Uìje, nchini Angola. 

Padre Joaquim N. Tyombe, Askofu Jimbo Katoliki la Uìje, Angola!

Askofu mteule Joaquim N. Tyombe alizaliwa tarehe 22 Novemba 1969. Tarehe 24 Novemba 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Lubango. Kati ya Mwaka 2010- 2012 alitumwa mjini Lisbon, Ureno kujiendeleza zaidi na huko akajipatia Shahada ya Uzamivu Kati ya Mwaka 2010 hadi mwaka 2016 alijiendeleza zaidi na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika uongozi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Joaquim Nhanganga Tyombe kutoka Jimbo Katoliki la Lubango, nchini Angola kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Uíje, nchini Angola. Kabla ya uteuzi huu, Padre Joaquim Nhanganga Tyombe alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Taalimungu ya Padre Leonardo Sikufinde iliyoko Jimbo kuu la Lubango. Askofu mteule Joaquim Nhanganga Tyombe alizaliwa tarehe 22 Novemba 1969. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 24 Novemba 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Lubango.

Katika maisha na utume wake kama Padre amewahi kuwa: Paroko-usu, Mlezi na Mkurugenzi wa Taasisi ya “Ciêcias Riligiosas de Angola” (ICRA). Kati ya Mwaka 2010- 2012 alitumwa mjini Lisbon, Ureno kujiendeleza zaidi na huko akajipatia Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Kitaalimungu toka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ureno, ’Universidade Católica Portuguesa di Lisbona” na baadaye kati ya Mwaka 2010 hadi mwaka 2016 alijiendeleza zaidi kwenye Chuo Kikuu cha Lisbon “Universitário de Lisboa” na huko akajipatia Shahada ya Uzamivu katika masuala ya uongozi wa taasisi za elimu. Tangu mwaka 2016 akateuliwa kuwa Gambera na mwalimu wa Seminari kuu ya Kitaalimungu ya Padre Leonardo Sikufinde iliyoko Jimbo kuu la Lubango.

Papa: Angola

 

 

 

 

 

02 February 2021, 15:54