Papa Leo XIV:Ni huruma ya Mungu pekee inayoweza kuingiza mioyoni upendo wa kibinadamu!
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa mwaliko wa kufuata, katika barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, iliyoelekezwa kwa Askofu Maurizio Malvestiti wa Lodi, wakati wa Siku ya 27 ya Columbanus, ambayo ilifanyika kati ya 4 na 5 Julai 2026, katika jiji la Mkoa wa Lombardia. Papa Leo XIV alibainisha kuwa “kelele za shutuma, zinazozidisha uharibifu na vifo vinavyosababishwa na migogoro, lazima zipingwe kwa ombi la unyenyekevu na ukimya wa huruma, kwa kuomba moyo mpya unaoweza kumfikia adui.”
Pongezi kwa mipango mingi
Papa alipongeza uvumilivu katika kufuata mpango ambao kwa miaka mingi umewaunganisha jumuiya za kikanisa na za kiraia zilizojitolea kwa Mtakatifu Columbanus barani Ulaya, kukuza uelewa wa Abati, urithi wake wa kiroho, na umuhimu wake kwa utamaduni wa Ulaya. Barua hiyo pia ilisisitiza jinsi, ambavyo "ni muhimu kujifunza kutoka kwake kwa kutotunza zawadi za Mungu binafsi bali kuzishirikisha kila mtu. "Kwa njia hiyo siku zilizowekwa kwa mtakatifu husaidia kuwaunganisha watu wa lugha na mataifa tofauti, "kuwaalika kugundua upya maadili ya tamaduni za Kikristo ili kukabiliana na changamoto za wakati wetu."
Ni huruma ya Mungu tu inaweza kuingiza huruma moyoni mwa binadamu
Mtakatifu Columbanus pia ni mwalimu wa mtazamo ambao ni "muhimu" kwa njia yoyote halisi ya upatanisho, aliandika Papa Leo XIV: Mgogoro unapogeuka kuwa vita, na matokeo ya kusikitisha ya kifo na uharibifu, badala ya kushtakiana, lazima tuombe huruma kutoka kwa Mungu, Hakimu mwenye huruma. Ni huruma ya Mungu pekee inayoweza kuingiza upendo wa kibinadamu mioyoni na kusababisha maadui kuwasiliana. Barua hiyo ilihitimisha kwa kukumbuka ziara ya hivi karibuni ya kichungaji ya Papa katika eneo la Lodi ili kutoa heshima kwa Mtakatifu Francesca Xavier Cabrini.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
