Papa Leo XIV Bunge,Hispania:Dunia inakabiliwa na mgogoro wa kiroho na kiutamaduni

Papa katika Bunge la Hispania Juni 8,mada zilikuwa kuanzia siasa,amani,mazungumzo,upangaji upya,uhamiaji,sheria,mgawanyiko;mada za kimaadili,familia na ulinzi wa maisha katika awamu zake zote;uhamiaji na kuwajali masikini.“Kila jamii yenye haki ya kweli imejengwa juu ya utambuzi wa utu usioweza kuepukika wa mwanadamu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alizungumza katikati ya Bunge la kitaasisi, kisheria, na kidemokrasia la Hispania yaani katika Bunge la Manaibu. Ni Papa wa kwanza kuhutubia katika Ukumbi huo . Wabunge na maseneta mia tano wamehudhuria katika tukio hilo, ambalo walimpongeza kuingia kwa makofi ya kudumu wakati wa kuingia lakini pia mara baada ya hotuba yake ndefu. Alifika yapata saa 4:30,  Jumatatu asubuhi tarehe 8 Juni 2026 akikaribishwa na Spika wa Bunge na Seneti, Francina Armengol na Pedro Rollán na Waziri Mkuu Pedro Sánchez, ambaye tayari alikuwa amekutana naye kwenye Mkutano wa faragha pia alikuwepo. Papa Leo XIV aliwashukuru, huku akawasalimia  na kushikana mikono na wawakilishi mbalimbali wa taasisi, akisaini Kitabu cha Heshima.

Bunge la  Hispania
Bunge la Hispania   (@Vatican Media)

Vipengele vilivyozungumziwa katika hotuba

Katika hotuba ya Papa Leo XIV kwa lugha ya Kihispania alikabiliana na masuala ya kisiasa, amani, mazungumzo, upangaji upya, uhamiaji, sheria, mgawanyiko; mada za kimaadili: familia na ulinzi wa maisha katika awamu zake zote; kisha alitoa wito wa uhuru wa dhamiri na dini, (ikiwa ni pamoja na usiri wa maungamo,) kuwatunza maskini, na hatimaye ujumbe kwa Hispania, Ulaya, na dunia nzima.  Mara baada ya hotuba ya Spika wa Bunge, Baba Mtakatifu alianza, akimshukuru Spika kwa maneno yake lakini pia kwa mwaliko ambao Makao ya Kitume yalipokea katika fursa ya ziara yake hiyo katika Nchi na kwa namna walivyomkaribisha kwa heshima katika Jumba hilo la kihistoria la Bunge la Manaibu, kiti kikuu cha maisha ya kitaasisi, kisheria, na kidemokrasia cha Ufalme wa Hispania. Mara moja Papa alijitambulisha kufika kwake kama: “Askofu wa Roma na Mchungaji wa Kanisa Katoliki,” akitambua  kwamba utume aliokabidhiwa kwa Mrithi wa Mtume Petro kama kanuni na msingi wa umoja wa Maaskofu na waamini (taz. LG, 23) unaweka Kiti Kitakatifu, kwa njia maalum, katika mazungumzo na watu na Mataifa.”

Hispania inajitambulisha kihistoria na imani yake

Kwa sababu hiyo, Papa Leo XIV alisema kuwa “ninapozungumzia maisha ya umma, ninafanya hivyo kwa heshima ya dhamira maalum ya taasisi na jukumu halali la wale waliopewa jukumu la kutunga sheria. Inatambua "uhuru wa hali halisi za kidunia" na "tofauti kati ya jumuiya ya Kanisa na jumuiya ya kisiasa." Na, hasa kutokana na ufahamu huu, inatoa taswira iliyotokana na hamu ya kutumikia manufaa ya wote na kukumbuka kinachofanya kuishi pamoja kuwa binadamu kweli. (Taz. Magnifica humanitas, 18-19).” Kwa njia hiyo Papa alieleza, zaidi ya utofauti halali wa nafasi, kila shughuli ya kutunga sheria huishia kukabiliwa na swali muhimu: ni dhana gani ya mwanadamu inayohamasisha sheria na ni aina gani ya jamii ambayo sheria hizi huunda. Kwa kukabiliwa na swali hili, Hispania ina kumbukumbu nzuri sana. Utambulisho wake wa kijiografia na kisiasa umeunganishwa na historia ambayo imani na akili, sanaa na sheria, tamaduni na mawazo vimeunganishwa kwa mafanikio. Katika makanisa na vyuo vikuu vyake, katika fasihi yake isiyokufa, katika taasisi zake za kisheria, na katika roho ya watu wake, urithi unaoishi ambao umeunda njia tofauti ya kupata uhuru, kutenda haki, na kupanga maisha ya jamii.”

Papa mbele ya wanabunge nchini Hispania
Papa mbele ya wanabunge nchini Hispania   (@Vatican Media)

Papa Leo XI aliendelea kusisistiza kuwa “Kutoka kurasa za ulimwengu za Padre  Quixote, ambapo Cervantes alitangaza kwamba "uhuru [...] ni mojawapo ya zawadi za thamani zaidi ambazo mbingu imewapa wanadamu" (Padre Quixote wa La Mancha, II, 58), hadi kina cha kiroho cha Mtakatifu Teresa wa Ávila, na kutoka kwa tamaduni  kubwa ya kisheria ya Hispania hadi kutotulia kwa kimetafizikia kwa Unamuno, ambaye alikumbusha kwamba mwanadamu "hajiachi kufa kabisa" (Kwa Hisia ya Uhai ya Kusikitisha, I), Hispania imewaona wanadamu kama zaidi ya sehemu tu ya utaratibu wa kijamii, kiuchumi, au kisiasa: imewatambua kama viumbe walio wazi kwa ukweli, waliopewa uhuru, na wanaoendeshwa na kiu ya umilele ambayo hakuna ukweli wa muda unaoweza kuzima; kwa neno moja, kama mtu ambaye hadhi yake inatangulia matumizi yote na ambaye hatua ya kisheria ya utumishi wake iko chini ya mamlaka yake.”

Hispania ilikabiliwa na majukumu ya kihistoria

Papa Leo  XIV alisisitiza “Kwa hivyo, tunapozungumzia mwanadamu leo, kumbukumbu kwa kawaida huongoza Salamanca na wazo lililokua hapo. Uwepo wa mfano wa Wafalme Isabella na Ferdinand katika ukumbi huu unarudi nyuma hadi wakati ambapo Hispania ilikabiliwa na majukumu ya kihistoria yenye umuhimu wa ulimwengu; miaka michache baadaye, Salamanca ingelazimika kuchukua, kwa uwazi wa pekee, tafakari ya kimaadili na kisheria ambayo hali hiyo ilihitaji. Katika mazingira hayo ya chuo kikuu, miaka mia tano iliyopita, wakati ulimwengu mpya na uwezekano mkubwa ulipokuwa ukifunguka katika mahusiano kati ya watu, baadhi ya walimu walielewa kwamba akili haiwezi kutumika ili kuhalalisha ni nguvu au maslahi gani yaliyowasilishwa kama ya haraka.

Bunge la Hispania
Bunge la Hispania   (@Vatican Media)

Kwa hivyo waliingiza katika utambuzi wa kihistoria swali la thamani lisilopunguka la kila mwanadamu na mipaka ya kimaadili ya nguvu. Lazima ikubaliwe kwamba jamii na Kanisa lenyewe hazijaishi kulingana na maarifa yaliyorejewa katika tamaduni zao za Kikristo. Hata hivyo, swali hilo lilifungua upeo wa kiakili na kimaadili ambao ulifikia mbali zaidi ya muktadha wake wa kihistoria. Hisia ya totus orbis, yaani “Ulimwengu wote” ya jumuiya ya binadamu pana kuliko nguvu yoyote maalum, iliruhusu uthibitisho wa uwepo wa vifungo vya kisheria na kimaadili kati ya watu. Kutoka Hispania, tafakari za Shule ya Salamanca hasa ya Ndugu  Francisco de Vitoria, pamoja na Wadominikani na Wajesuit wengine, zilisaidia kuunda dhamiri ya kisheria na kimaadili inayoweza kukumbuka kwamba mamlaka daima huhusisha uwajibikaji na kwamba kila mwanadamu lazima atambuliwe kama mhusika wa haki na wajibu. Tamaa hiyo inaendelea kusikika leo: kwamba utu, haki, na manufaa ya wote viwe kipimo cha mahusiano ya kijamii, kitaifa na kimataifa.

Ulimwengu leo hii unafunguka tena bila kufuatilia kwenye ramani 

Swali la Salamanca linaendelea kuongoza juhudi za wale wanaofanya kazi katika maisha ya umma. Leo hii ulimwengu mpya unaofunguka mbele yetu haufualiwi tena  kwenye ramani: unajitokeza katika teknolojia, uchumi, biomedicine, na ulimwengu wa kidijitali, ambapo nguvu za binadamu hufikia maeneo nyeti zaidi ya maisha ya kibinafsi na kijamii. Maendeleo hutoa uwezekano wa ajabu, na leo tunaona hili hasa katika maendeleo ya akili unde(AI) na teknolojia mpya. Kama nilivyokumbuka katika Waraka wangu wa hivi karibuni, teknolojia yenyewe si ya upande wowote, kwa sababu inachukua sura ya wale wanaoifikiria, kufadhili, kudhibiti, na kuitumia (tazama Magnifica Humanitas, 9).

Bunge la Hispania
Bunge la Hispania   (@Vatican Media)

Kwa hivyo, tukikabiliwa na mabadiliko ya wakati wetu, utambuzi wetu lazima uzingatie nafasi ya mwanadamu katika maamuzi yetu na jinsi hadhi ya kazi, mshikamano, sera ya kijamii, na manufaa ya wote yanavyowasilishwa kwa njia mpya leo hii. Utambuzi huu huanza na uthibitisho wa msingi: kila jamii yenye haki kweli imejengwa juu ya utambuzi wa utu usiovunjwa wa mwanadamu. Utu huu unatangulia makubaliano yoyote na Serikali na hauwezi kuwekwa chini ya makubaliano ya kijamii yanayobadilika au mabadiliko ya walio wengi kwa muda mfupi (Taz. Papa Benedikto  XVI, Hotuba kwa Bunge la Shirikisho la Ujerumani, Septemba 22, 2011). Ni mali ya kila mwanadamu kiukweli wa kuwepo, na kwa hivyo lazima iongoze kila mfumo chanya wa kisheria. Imani ya Kikristo inatangaza kwa msingi wa Ufunuo; akili ya mwanadamu inaweza kuitambua kama sharti lililoandikwa katika ukweli wa mwanadamu (tazama ibid.). Imani hii inapobaki hai, sheria inakuwa ulinzi wa wote na dhamana dhidi ya kuwekewa maslahi na ajenda fulani.

Utamaduni wa kutupa na Ulinzi wa maisha ya mwanadamu

Papa Leo XIV aliendelea kubainisha kuwa “Kwa msingi huu, nimepewa fursa leo kuzungumzia neno tulivu na la uamuzi kwa wale wanaobeba jukumu kubwa la kudhibiti kisheria kuishi pamoja kijamii. Uwepo huu wa pamoja unaweza kutishiwa na utamaduni wa kutupa vitu, kama Papa Francisko alivyosema mara kwa mara (taz. Hotuba kwa Mkutano Mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, Septemba 27, 2021). Kwa maana hiyo ikiwa maisha yataacha kutambuliwa kama thamani ya msingi, jamii zetu zinaweza kuwa na mustakabali gani? Je, jamii inaweza kuzingatiwa kuwa ya haki kikamilifu ikiwa inampuuza mtoto ambaye hajazaliwa, wazee, wagonjwa, wale wanaoteseka kimya kimya, au wale wanaotegemea kabisa utunzaji wa wengine? Ulinzi wa maisha ya mwanadamu si jambo la maslahi au ungamo maalum: ni lengo la ustaarabu."

Kila maisha ya mwanadamu lazima yatambuliwe

Kila maisha ya mwanadamu lazima yatambuliwe na kulindwa tangu kutungwa mimba hadi mwisho wake wa asili, katika kila hali ya kuwepo kwake. Wakati uhakika huu unapofichwa, walio hatarini zaidi ni waathiriwa wa kwanza, na sheria hupoteza maana yake ya ndani kabisa: kumtumikia na kumlinda kila mtu. Kwa sababu hii, ukuu wa kimaadili wa taifa unaonyeshwa, zaidi ya yote, katika uwezo wake wa kuongozana, kulinda, na kupenda maisha hayo unaoonyeshwa na udhaifu mkubwa zaidi. Manufaa ya wote, kwa maana fulani, ni "aina ya kijamii ya utu wa binadamu" (taz. Magnifica Humanitas, 59). Hayajumuishi  maslahi maalum tu, bali katika "jumla ya masharti ya maisha ya kijamii ambayo huruhusu vikundi na watu binafsi kufikia utimilifu wao kikamilifu na kwa urahisi zaidi" (Gaudium et Spes, 26). Wakati manufaa ya wote yanapokoma kuwa upeo wa pamoja, hatua za umma zina hatari ya kugawanyika katika maslahi ya sehemu, yasiyoweza kulinda yaliyo ya wote.

Katika muktadha huo, familia, uhalisia wa kwanza wa mwanadamu na msingi wa asili wa jumuiya, ni muhimu sana. Ndani ya familia, vizazi vimeunganishwa na kumbukumbu hai hupitishwa, na kutoa mwendelezo wa ndani kwa jamii. Pale ambapo familia inaungwa mkono, utulivu wa kiroho na kijamii wa mataifa pia huimarishwa. Familia itakuwa shule ya kwanza ya ubinadamu, ambapo, kabla ya mahali pengine popote, tunajifunza sarufi ya msingi ya kuishi pamoja: maisha ya kukaribisha, kuwajali wengine, kusamehe, kuhudumia, na kuwa mali. Taasisi za elimu pia zina jukumu muhimu katika kazi hii. Ndani yao, vizazi vipya vinaweza kujifunza kutafuta na kupenda ukweli, kuhoji maana ya maisha na hadhi ya kila mtu. Kwa hivyo, wazazi wengi, wakiwa na hamu ya watoto wao kujifunza kuhusiana na wengine, kufikiria kwa kina, na kupata maadili thabiti, huwawekea matumaini makubwa kama washirika wa thamani katika malezi yao. Ushirikiano huu lazima uheshimu "haki ya msingi na isiyoweza kuondolewa" ya wazazi ya "kuchagua aina ya mafundisho na malezi ya kuwapa watoto wao, kulingana na imani zao za kimaadili, kiutamaduni, na kidini" (Magnifica Humanitas, 143; Agano la Kimataifa la Haki za Kiraia na Kisiasa, kip. 18.4).

Utu wa Mwanadamu si wa kufikirika:wengi wanalazimika kuacha kila kitu kutafuta amani

Papa aleleza kuwa uthibitisho wa utu wa binadamu hauwezi kubaki kuwa wa kufikirika wakati watu wengi wanalazimika kuacha kila kitu nyuma kutafuta amani, usalama, na mustakabali. Mgogoro wa uhamiaji wa kusikitisha pia unapinga dhamiri za mataifa na msingi wa maadili wa utaratibu wa kimataifa. Wanaume, wanawake, na watoto wengi wanalazimika, mara nyingi kutokana na hali ngumu, kuacha jamii zao na kuacha wapendwa wao, hadithi, na vifungo. Hali ya wahamiaji na wakimbizi inahitaji mwitikio unaowaweka watu katikati, kushughulikia sababu zinazowalazimisha kuondoka, na kwenda zaidi ya usimamizi rahisi wa mtiririko. Hili linasababisha hitaji la haki ya kijamii mara mbili: kutoa njia salama na za kisheria, makaribisho ya heshima, na fursa halisi za ujumuishaji; na, wakati huo huo, kukuza haki ya kubaki katika nchi yako mwenyewe, kufanya kazi ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayelazimika kuacha nyumba yake kutokana na ukosefu wa amani, usalama, au hali ya maisha yenye heshima, ukosefu wa usawa wa kiuchumi, au athari za mgogoro wa hali ya hewa (Magnifica Humanitas, 81).

Ujumuishaji kwa wahamiaji

Hakuna taifa linaloweza kukabiliana na changamoto kubwa kama hii peke yake. Hii ndiyo sababu mwitikio ulioratibiwa, unaounga mkono, na wenye ufanisi ni muhimu, unaoweza kuhakikisha ulinzi, kukubalika, na fursa halisi za ujumuishaji kwa wahamiaji. Mwitikio wa kitaasisi unapofaa, usawa, na uratibu, mipaka huacha kuwa sehemu za kutelekezwa na inaweza kuwa nafasi za ulinzi wa heshima ya binadamu kwa uwajibikaji.

Dunia inakabiliwa na mgogoro wa kiroho na kiutamaduni

Dunia inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiroho na kiutamaduni, unaojidhihirisha katika aina nyingi za vurugu, utengano, na kutoaminiana. Katika muktadha huu, amani inajionesha kama matarajio ya kisiasa na, zaidi ya hayo, kama sharti la kweli la kimaadili. Inahitaji mazungumzo ya umma yanayowaheshimu wale wanaofikiri tofauti, taasisi zinazohudumia mkutano, kumbukumbu ya kihistoria inayotafuta ukweli na upatanisho, na maisha ya kijamii yanayoweza kudumisha urafiki wa kiraia na kuheshimiana hata katikati ya kutokubaliana.

Papa akihutibia Bunge la Hispania
Papa akihutibia Bunge la Hispania   (@Vatican Media)

Kwa ngazi ya kimataifa amani inahitaji ujasiri wa kidiplomasia

Katika ngazi ya kimataifa, amani inahitaji ujasiri wa kidiplomasia, uwajibikaji wa kimaadili, na maono ya mustakabali kulingana na heshima ya utambulisho wa kila watu na wajibu wa mataifa kutatua migogoro yao kupitia njia za amani zinazotolewa na sheria ya kimataifa. Kila vita hatimaye inawakilisha kushindwa kwa uchungu kwa uwezo wa mazungumzo na dhamiri ya pamoja ya binadamu inayotambua vifungo vya haki kati ya mataifa. Silaha zinaweza kulazimisha ukimya wa muda, lakini haziwezi kamwe kujenga amani ya kweli na ya kudumu. Kwa sababu hiyo, inatia wasiwasi kwamba, katika sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni pamoja na Ulaya, upangaji silaha unaibuka tena kama jibu lisiloepukika kwa udhaifu wa mazingira ya kimataifa. Hata hivyo, usalama wa kweli unatokana na haki, mazungumzo ya subira, heshima kwa sheria ya kimataifa, na sera inayoweza kuweka maisha ya watu mbele ya maslahi yanayofaidika na vita. Maendeleo ya teknolojia mpya na akili unde(AI) katika uwanja wa kijeshi pia yanahitaji uangalifu mkubwa wa kimaadili, ili maamuzi kuhusu maisha na kifo yasiachwe kamwe kwa mifumo ya moja kwa moja au kuondolewa kutoka katika jukumu la kimaadili la mwanadamu (Taz. Chuo Kikuu cha La Sapienza, 14 Mei 2026).

Jumuiya ya Kimataifa igundue tena thamani ya mazungumzo

Jumuiya ya kimataifa inaitwa kugundua upya thamani muhimu ya mazungumzo kama njia ya uvumilivu kuelekea makubaliano ya haki na ya kudumu, yaliyoanzishwa kwa heshima ya mikataba, uwazi katika hatua za kidiplomasia, na hamu ya dhati ya kuweka kipaumbele amani kuliko matumizi ya nguvu. Kutokana na hili huibuka uaminifu na matumaini. Kama kauli mbiu ya Umoja wa Ulaya inavyokumbuka, “Katika makubaliano ya aina mbalimbali, umoja wa kweli hauleti umoja, bali huunda mshikamano katika utofauti, na kufanya tamaduni, hisia, na tamaduni  kuwa fursa ya kujitajirisha pamoja. Vivyo hivyo, ndani ya jamii zenyewe, ni muhimu kukuza utamaduni wa kurudishana. Wingi wa kisiasa haupaswi kuharibika na kuwa kumdharau adui wa kudumu. Katika kuishi pamoja kwa pamoja, hata migogoro inaweza kuwa jiwe la kuelekea amani, wakati tofauti zinapopunguzwa kwa kusikiliza na zinaelekezwa kutambua mahitaji, matarajio, na uwezo wa wote.

Wanye jukumu la umma wanawajibu wa kulinda kuondoa lugha ya silaha

Lakini amani si ukweli wa kisiasa au kitaasisi tu, Papa alisisitiza. Pia huzaliwa katika dhamiri, ambapo chuki, kutojali, na chuki huacha nafasi ya upatanisho. Kwa hivyo, pia huanzishwa na kulindwa kupitia lugha. Maneno yanaweza kufungua njia au kuzifunga; yanaweza kuangazia ukweli au kuupotosha hadi kufikia hatua ya kufanya kukutana kusiwe rahisi. Kwa hivyo, wale wanaotekeleza jukumu la umma wana wajibu maalum wa kulinda neno ili "kuondoa lugha silaha" (Ujumbe wa Kwaresima 2026, Februari 13, 2026). Uimara hauhitaji dharau; kutokubaliana hakumaanishi aibu. Kutokana na heshima hii kwa wengine pia kunatokea wajibu wa kulinda nafasi ambayo imani zao, dhamiri zao, na uhusiano wao na Mungu hukomaa. Kuzingatia ulimwengu huu wa ndani kunaturuhusu kuelewa vyema suala muhimu kwa kila jamii ya kidemokrasia ya kweli: uhuru wa mawazo, dhamiri, na dini, haki ya msingi inayolinda nyanja ya ndani zaidi ya watu. Uhuru ambao serikali ya kisasa imeanzishwa, ikiwa ni ya kweli, unatambua mwelekeo wa kidini wa wanadamu, unauheshimu, na unaulinda kisheria; na humzuia mtu yeyote kuacha kuchangia katika jamii anayoishi kwa sababu ya imani yake.

Bunge a Ulaya
Bunge a Ulaya   (@Vatican Media)

Bila kuchanganya mipango ya kisheria na maadili, ni vizuri pia kukumbuka kwamba uhuru unahitaji uelewa kamili wa nafsi yake. Kuwa huru haimaanishi tu kuishi bila vikwazo au kuwa na chaguzi nyingi; inamaanisha kuweza kutambua mema na kuyafuata kwa uwajibikaji. Kwa hivyo, kila jamii huru kweli pia inahitaji uwekaji mipaka wa haki wa nguvu za umma, ili uhuru wa watu binafsi, jamii, na vyama usiwe na mipaka isiyo ya lazima (tazama Dignitatis Humanae, 1). Kutoka kwa mtazamo huu, uhuru halali wa utaratibu wa kidunia haupaswi kamwe kufasiriwa kama uadui dhidi ya jambo la kidini. Imani haidai kujilazimisha kupitia marupurupu au kulazimishwa; hata hivyo, wala haiwezi kuachwa kimya kana kwamba haina maana kwa maisha ya umma.

Katika muktadha huu, muhuri wa kisakramenti wa Ungamo una umuhimu maalum kwa Kanisa Katoliki. Unaingia katika muktadha mpana wa uhuru wa kidini, ambao unahakikisha jamii za imani nafasi yao ya kuishi, kupanga, na nidhamu ya ndani (tazama Mkutano: Sheria ya Mwisho ya Helsinki, 1 Agosti 1975, Kanuni ya VII). Kuilinda kisheria, kama ilivyo kwa taaluma fulani, kunamaanisha kuhifadhi nafasi takatifu ya uhuru wa ndani, ambapo waumini wanaweza kufungua roho zao kwa Mungu bila hofu ya shinikizo la nje, kama sheria ya kimataifa pia inavyotambua (taz.Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu,Kanuni za Utaratibu na Ushahidi, n. 73.3).

Picha zilizopambwa kwenye Bunge

Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kuwa “acha nichukue muda kutazama baadhi ya picha zinazopamba Bunge hili. Katika ukumbi huu mwanga wa asili huingia kupitia mwanga wa angani unaopamba ukumbi huu. Mwanga unaotoka juu kutukumbusha kwamba hata siasa zimejifunza kutambua kipimo kinachotangulia na kuzidi. Pia, katika sehemu ya juu ya kuta kuu, tunaakisi usindikizaji wa Injili  na Amri za Mungu kuu za Mugu, tukikumbuka baadhi ya mambo muhimu. Bila kuchanganya utaratibu wa kisiasa na kidini, ishara hizi zinatualika kutambua kwamba uhuru wa kisasa pia uliandaliwa na elimu ndefu ya dhamiri, iliyoathiriwa sana na tamaduni ya Kikristo. Katika shule hii ya ndani, watu wamejifunza kwamba sheria lazima itumikie mema, kwamba haki huweka mipaka ya nguvu, kwamba nguvu inahitaji uhalali, kwamba maskini ni wa jamii kikamilifu, kwamba mgeni lazima akaribishwe kulingana na hadhi yake, na kwamba maisha ya mwanadamu hayawezi kamwe kuchukuliwa kama bidhaa.

Wakati wa kusaini kitabu cha Heshima
Wakati wa kusaini kitabu cha Heshima   (@Vatican Media)

Sheria haifikii ukuu wake wa kweli kwa kuidhinishwa rasmi tu; inaifikia wakati, pamoja na kuwa halali katika umbo, inaweza kusimama kwa heshima ya mtu na kupita mtihani huo bila aibu. Kwa hivyo ninakualika uinue macho yako: sio kujitenga na ukweli, lakini ukumbuke kwamba kila uamuzi unaofanywa na mamlaka ya umma unawaathiri watu halisi, haswa wale ambao hawana uwezo wa kutoa sauti zao. Kwa sababu maono ya hali ya juu yanajumuisha hasa kuangalia kwa undani zaidi kile kilicho hatarini katika kila uamuzi wa umma. Kwa hivyo, pamoja na majibu ya kiufundi na mageuzi ya kisheria, uboreshaji wa maadili pia ni muhimu. Hispania ina mengi ya kutoa katika safari hii. Ina lugha inayounganisha mabara; utamaduni wa kitamaduni, kisheria, na kiroho ambao umefanikiwa kuleta imani na sababu, sheria na dhamiri, umoja na wingi katika mazungumzo. Uzoefu huu wa kihistoria pia unatukumbusha thamani ya maelewano na juhudi za subira ili kujenga mshikamano wa amani na haki.

Taifa hili tukufu lisipoteze kumbukumbu ya mizizi yake wala ujasiri wa kutazama mustakabali. Uhispania iendelee kuwa nchi ya kukutana, utamaduni, mshikamano, na matumaini. Na maisha yake ya hadharani yaunganishe imani thabiti na heshima ya mazungumzo na ukuu wa huduma. Mungu awape amani mataifa yote ya dunia, maelewano kwa familia, na utulivu kwa dhamiri. Na juu ya Ufalme wa Hispania, ulio na alama ya ushawishi wa kitume wa Mtakatifu Yakobo na uwepo wa mama wa Bikira wa Pilar(Nguzo), siku za ustawi, haki, na amani ya kudumu ziwashukie. Asante!"

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

08 Juni 2026, 12:40