2024.02.07 Sudan Refugees Wedweil Carine

Papa Leo XIV Siku ya Wakimbizi duniani:Ninawasihi kuwakaribisha wanaoathiriwa na mateso ili waishi kwa amani na heshima

Ninatumaini kwamba roho iliyochochea maendeleo ya chombo hiki muhimu cha kimataifa itaendelea kuelimisha dhamiri za viongozi wa kitaifa leo hii.Hakuna anayeweza kuwaacha wale wanaotafuta ulinzi na usalama.Pia ninawasihi kila mtu kuwakaribisha wale walioathiriwa na mateso,ili waweze kuishi kwa amani, heshima na kutazamia mustakabali kwa matumaini.”Ni Wito wa Papa Leo XIV,mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,Juni 21 katika muktadha wa Siku ya Wakimbizi duniani,Juni 20.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kila ifikapo tarehe 20 Juni ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa unafanya kumbukizi ya Siku ya Wakimbizi  ambapo hadi leo hii kuna zaidi ya wakimbizi milioni 41 duniani kote, asilimia 40% yao wakiwa wanawake na watoto! Katika Bahari ya Mediterania, katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, zaidi ya watu 32,000 wamepoteza maisha au hawajulikani waliko. Ni katika Muktadha huo ambapo mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 21 Juni 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV akiwageukia waamini na mahuhaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican alikumbusha tukio hilo kwamba, “Jana, Siku ya Wakimbizi Duniani, iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa, iliadhimishwa, ikiadhimisha miaka 75 ya Mkataba unaohusiana na Hali ya Wakimbizi, ulioundwa ili kuwalinda wale wanaoteswa na kulazimishwa kuondoka nchini mwao, nyumbani, na familia zao. Papa alioendelea: “Ninatumaini kwamba roho iliyochochea maendeleo ya chombo hiki muhimu cha kimataifa itaendelea kuelimisha dhamiri za viongozi wa kitaifa leo hii. Hakuna anayeweza kuwaacha wale wanaotafuta ulinzi na usalama. Pia ninawasihi kila mtu kuwakaribisha wale walioathiriwa na mateso, ili waweze kuishi kwa amani, kwa heshima, na kutazamia mustakabali kwa matumaini.”

Papa akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume kwa tafakari na sala
Papa akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume kwa tafakari na sala   (@Vatican Media)

Wajumbe wa Mazungumzo ya kimataifa: “lex orandi, lex credendi”

Kwa Lugha ya Kiingereza Papa Leo XIV  alipenda kutoa salamu kwa Wajumbe wa 'Mazungumzo ya Kimataifa ya Pentekoste ya Kikatoliki.' "Kanisa linaamini linapoomba", na kutafakari pamoja kuhusu kanuni hiyo “lex orandi, lex credendi” inayohusu Ushirika wa Imani katika Maisha ya Kanisa” ambapo Papa Leo XIV  alisema "ni muhimu sana katika siku hizi.”

Waathiriwa wa ajali nchini Brazil

Papa alipanua salamu zake kwa wote kwa upendo, waamini wa Roma na mahujaji ambao wametoka nchi tofauti. Alielekeza Mawazo yake kwa lugha ya kireno, kwa mahujaji kutoka Brazil, huku akiwahakikishia sala zake vijana waliokufa, kwa ajali  siku chache zilizopita, katika nchi ya mbali,  Mkoa wa Ceará.

Waamini na mahujaji walifika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini na mahujaji walifika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Kuhusiana na ajali hiyo, waliokufa  walikuwa wanafunzi, wakirudi nyumbani baada ya kushinda mashindano ya mpira wa vikapu ya vijana nchini Brazil, yaliyofanyika katika jiji la Juazeiro del Norte, katikati mwa nchi. Wakati wakisafiri kwa Basi kuelekea kaskazini mashariki kwenda Sobral, safari ya karibu kilomita 600 ambapo, Basi hilo, lililokuwa limebeba abiria wapatao arobaini, lilipinduka. Ajali hiyo ilitokea usiku wa Juni 15 huko Tauá, mji katika Mkoa wa Cearà, kaskazini mashariki mwa nchi. Kupinduka huko kulisababisha vifo vya wachezaji saba, wenye umri  kati ya miaka 15 na 22. Karibu abiria wengine wote walijeruhiwa.

papa baada ya sala ya Malaika wa Bwana

Hatimaye Papa aliwasalimia vijana wa  kipaimara kutoka Parokia mbili ya Ozieri, Sardegna. Na aliwatakia wote Dominika njema!

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

21 Juni 2026, 12:29