Muhtasari wa dakika moja wa Ziara ya Kitume ya Papa kwenda Hispania
Vatican News
Nje na mpangilio kutokana na shida ndogo ya kuharibika kwa Injini ya Ndge ya Iberia (Airbus A320) ambayo ilitakiwa kumrudisha Roma kutoka Tenerife, na badala yake akarudi akiwa ndani ya Falcon ya kijeshi iliyotolewa na Mfalme Philip VI, ya ziara yake ya kitume ya Papa Leo XIV kwenda Hispania ilimalizika. Picha za kipekee za Vyombo vya Habari Vatican zinafuatilia matukio mbali mbali ya kukaa kwa Papa kwa siku saba katika Ghuba ya Iberia, ikijumuisha Madrid, Barcelona na Visiwa vya Kanari(6-12 Juni 2026). Kuanzia mkutano na Jumuiya ya Jimbo, katika Uwanja wa Santiago Bernabéu hadi uzinduzi wa Mnara wa Yesu Kristo katika Basilika ya ‘Sagrada Familia,’ picha ambazo zimeonekana ulimwenguni kote. Mikutano ya kusisimua na wahamiaji na mashirika yaliyojitolea kuwakaribisha pia yalifanyika katika visiwa hivyo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
