Mchango huu unamwezesha Baba Mtakatifu Leo XIV kuwasaidia watu waliokumbwa na majanga pamoja na maafa kama vile: matetemeko ya ardhi, mafuriko, njaa, ukame na vita. Mchango huu unamwezesha Baba Mtakatifu Leo XIV kuwasaidia watu waliokumbwa na majanga pamoja na maafa kama vile: matetemeko ya ardhi, mafuriko, njaa, ukame na vita.  (MAXWELL BRICENO)

Maadhimisho ya Siku ya Mshikamano wa Upendo na Baba Mtakatifu Leo XIV 2026

Mama Kanisa anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuungana na Baba Mtakatifu Leo XIV katika maisha na utume wake wa kutafuta na kudumisha amani, kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini kwa wale waliovunjika na kupondeka nyoyo pamoja na kutangaza Injili ya upendo na mshikamano kwa wale walioathirika kwa vita, kinzani na mipasuko; waathirika wa majanga asilia pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchini! Utu na heshima!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Siku ya Upendo na Mshikamano wa Papa. “The Pence of Saint Peter” (L’Obolo di San Pietro.) ilianzishwa kunako tarehe 8 Agosti 1871 na Papa Pio IX katika Waraka wake wa Kitume “Saepe Venerabilis.”  Na tangu wakati huo, kila mwaka ifikapo tarehe 29 Juni, lakini kwa Mwaka huu inaadhimishwa tarehe 28 Juni 2026 kwa kuungana na Khalifa wa Mtakatifu Petro kuonesha mshikamano wa udugu wa upendo na ukarimu kwa: kwa njia ya sala na hasa zaidi kwa kuchangia mfuko unaogharimia shughuli mbalimbali za Injili ya upendo zinazotekelezwa na Baba Mtakatifu katika nafsi ya Papa Leo XIV sehemu mbalimbali za dunia hasa katika kipindi hiki cha athari za vita, kinzani na mipasuko ya kijamii; madhara makubwa ya majanga asilia pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Siku ya mshikamano na Papa ili kuwasaidia waathirika wa majanga
Siku ya mshikamano na Papa ili kuwasaidia waathirika wa majanga   (AFP or licensors)

Khalifa wa Mtakatifu Petro anayo dhamana ya kuendeleza: Umoja wa Kanisa; Haki, Amani na Maridhiano Duniani mambo yote haya yanafumbatwa katika mchakato wa uinjilishaji mpya unaojikita katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko! Ni katika muktadha huu, Mama Kanisa anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuungana na Baba Mtakatifu Leo XIV katika maisha na utume wake wa kutafuta na kudumisha amani, kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini kwa wale waliovunjika na kupondeka nyoyo pamoja na kutangaza Injili ya upendo na mshikamano kwa wale walioathirika kwa vita, kinzani na mipasuko; waathirika wa majanga asilia pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchini.

Mchango wa mshikamano na Papa ni kwa ajili ya waathirika mbalimbali.
Mchango wa mshikamano na Papa ni kwa ajili ya waathirika mbalimbali.   (AFP or licensors)

Mchango huu unaotolewa na waamini pamoja na watu wenye mapenzi mema unamwezesha Baba Mtakatifu Leo XIV kuwasaidia watu waliokumbwa na majanga pamoja na maafa kama vile: matetemeko ya ardhi, mafuriko, njaa, ukame na vita. Ni msaada unoalenga kumsaidia mtu mzima katika mahitaji yake: kiroho na kimwili, kwa kuchangia maboresho katika sekta ya elimu, afya na maendeleo fungamani ya binadamu. Kanisa limeendelea kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya kuwasaidia maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii, kwa kuwajengea uwezo ili kukabiliana na changamoto za maisha kwa ujasiri na moyo mkuu pasi na kukata wala kujikatia tamaa. Tangu wakati huu, Baba Mtakatifu Leo XIV anawaombea waamini na watu wote wenye mapenzi mema akisema: “Bwana na awaongoze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu,” 1The 3:12.

Siku ya Mshikamano
28 Juni 2026, 12:30