2026.05.11: Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Observatory wa Vatican. 2026.05.11: Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Observatory wa Vatican.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Tunawajibu mkuu wa kulinda sayari yetu na walio hatarini zaidi!

Papa alikumbuka jukumu la pamoja la kutunza sayari na ustawi wa walio hatarini.alithibitisha tena thamani ya unajimu inayotusaidia kutafakari Mbingu:hazina inayoweza kufikiwa na wote na chanzo cha furaha ya Ulimwengu wote katika Dunia uliyogawanyika.Alisema hayo akukutana Mei 11 na wajumbe wa Bodi ya mfuko wa Observatory,wa Vatican,Shirika lenye makao yake Marekani linalounga mkono na kuhamasisha shughuli za Taasisi ya uchunguzi wa Kisayansi za Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na wanachama wa Bondi ya  Mfuko wa Taasisi ya Kipapa ya Utafiti wa unajimu, Jumatatu tarehe 11 Mei 2026 mjini Vatican, shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu huko Tucson, Arizona nchini Marekani, linalounga mkono na kuhamasisha  fedha za shughuli za kisayansi na kielimu za Observatory, Vatican ambayo ni "taasisi pendwa na muhimu ya Jiji la Vatican kwa huduma ya Vatican na Kanisa la ulimwengu wote. Papa alisema kuwa “Miaka 135 iliyopita, mtangulizi wake Papa Leo XIII alianzisha kituo cha Uchunguzi wa Vatican kwa namna ambayo “ili  wote waweze kuona kwa uwazi kwamba Kanisa na Wachungaji wake, hawapingi  sayansi ya kweli na thabiti, iwe ya kibinadamu au kimungu, lakini ambayo inakumbatia, inatia moyo na kuendeleza kuhamasisha  kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo  kujitolea.”

Wajumbe wa mfuko wa Mfuko wa Taasisi ya Kipapa ya Utafiti wa Kisayansi wa unajimu
Wajumbe wa mfuko wa Mfuko wa Taasisi ya Kipapa ya Utafiti wa Kisayansi wa unajimu   (@VATICAN MEDIA)

Kulinda Sayari na wanaoishi ndani mwake wadhaifu

Papa Leo XIV kwa Lugha ya Kiingereza alieleza kwamba, “wakati huo, sayansi ilikuwa daima inawakilishwa kama kisima cha kweli cha kukinzana na dini, na hivyo Kanisa lilikuwa likihisi uhitaji wa haraka wa kupingana na ukuaji wa uelewa kuwa imani na sayansi zinakuwa maadui.” Hata hivyo Papa Leo XIV, alieleza kuwa “leo hii, iwe sayansi au dini zinakabiliana na hatari tofauti na labda danganyanyifu zaidi: Ile ya wale wanaokataa sawa na ukweli halisi. Watu wengi katika ulimwengu wetu wanakataa kutambua kila ambacho sayansi na Kanisa linafundisha wazi “kwamba tunawajibu mkuu wa kulinda sayari yetu na kuhakikisha wema wa wanaoishi humo, hasa walio hatarini zaidi, ambao maisha yao yananyonywa,  kwa kutofikiriwa,  iwe kama watu, na iwe kama ulimwengu asili. Ni katika muktadha huo ambapo Kanisa linajitolea katika sayansi kwa bidii na ukarimu mkubwa,  si tu kuwa thamani, lakini pia muhimu.”

Anga wakati wa usiku limefunguliwa kwa wote maskini na matajiri

“Mnajimu anayo nafasi maalum katika utume huu,” Papa alikazia kusema.  “Uwezo wa kutazama kwa mshangao jua, mwezi na nyota ni zawadi iliyotolewa kwa kila binadamu, kwa kutembea na hali yake kijamii au kila muktadha. Inaibua ndani mwetu kitu safi kwa maana ya kipimo. Kutafakari mbingu, Papa Leo XIV alisisitiza “kunatualika kutazama woga wetu na ukosefu wetu katika mwanga mkuu wa Mungu.” Anga wakati wa usiku, ni tunu ya uzuri iliyofunguliwa kwa wote, masikini na matajiri na katika ulimwengu wa namna hii uliogawanyika kwa uchungu sana, unabaki kuwa moja ya kisima cha furaha kweli ulimwenguni.”

Picha ya Pamoja
Picha ya Pamoja   (@Vatican Media)

Dunia inatishiwa

Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea kusema kuwa cha kusikitisha, hata zawadi hii sasa inatishwa. Kwa maneno mengine, Papa Benedikto alisema kuwa tumejaza anga zetu na nuru iliyotengenezwa na mwanadamu ambayo inatupofusha tusione nuru ambazo Mungu ameweka hapo: taswira inayofaa, alipendekeza, ya dhambi yenyewe. (Mahubiri ya Papa Benedikto XIV, 7 Aprili 2012). Katika muktadha huo, Papa Leo XIV alipenda kutoa shukrani za kina kwa kazi ya Mfuko huo. Jitihada zao zinawawesha wanasayansi wa Vatican kushirikiana kwa njia ya kujenga na umma kwa ujumla na jumuiya ya wanasayansi duniani.

Papa alisema Darubini na maabara za Uchunguzi (Observatory) zinabaki vile zilivyokusudiwa kuwa
Papa alisema Darubini na maabara za Uchunguzi (Observatory) zinabaki vile zilivyokusudiwa kuwa

Ukarimu kwa Taasisi ya Uchunguzi

Ukarimu wao unaruhusu Taasisi hiyo ya uchunguzi kushikirisha maajabu ya unajimu kwa wanafunzi kutoka Ulimwenguni kote ili kupendekeza, maabara, na shule za kiangazi kwa wale ambao wanafanya kazi katika shule za kikatoliki na maparokia. Na hatimaye, ni kujitolea kwao kuhakikisha kwamba darubini na maabara za Uchunguzi (Observatory) zinabaki vile zilivyokusudiwa kuwa: mahali ambapo utukufu wa uumbaji wa Mungu unakutana kwa heshima, kina, na furaha. “Hatupaswi kamwe kupoteza mtazamo wa maono ya kitaalimungu yanayohuisha haya yote. Dini Yetu ni ya Umwilisho. Maandiko yanatufundisha kwamba tangu mwanzo Mungu amejitambulisha kupitia vitu alivyoviumba (taz. Rm 1:20), na kwamba Mungu alipenda uumbaji wake sana hata akamtuma Mwanawe kuingia ndani yake na kuuokoa (Yh 3,16).”

Papa akiwaaga wajumbe wa Mfuko wa Vatican wa Kisayansi
Papa akiwaaga wajumbe wa Mfuko wa Vatican wa Kisayansi   (@Vatican Media)

Watu wenye imani wanalazimika kuchunguza asili na utenda kazi wa ulimwengu

Kwa kuhitimisha Papa alisema, “Basi, haishangazi kwamba watu wenye imani kubwa wanahisi kulazimishwa kuchunguza asili na utendaji kazi wa ulimwengu. Hamu hii kubwa ya kuelewa uumbaji kwa undani zaidi ni kielelezo cha hamu hiyo isiyotulia ya Mungu ambayo iko ndani kabisa ya kila nafsi ya mwanadamu. Papa Leo XIV kwa mara  nyingine tena alitoashukrani na msaada wao, kwa utashi wake juu yao na juu ya familia zao aliwabariki kwa Baraka ya Mwenyezi Mungu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

11 Mei 2026, 15:25