Papa akutana na Waziri Mkuu wa Sudan
Vatican News.
Baba Mtakatifu Leo XIV alimpokea katika mkutano, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Sudan, Bwana Kamil El-Tayeb Idris Abdelhafiz. Mara baada ya mkutano huo Waziri Mkuu alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Monsinyo Mihăiţă Blaj, Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na Nchi za Nje na Mashirika ya Kimataifa.
"Wakati wa mkutano wa kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu, ilibainisha kuwa, "umuhimu wa mahusiano kati ya Kiti Kitakatifu na Sudan na mchango mkubwa wa Kanisa mahalia kwa manufaa ya nchi ulisisitizwa.
Mgogoro mkubwa ambao umeikumba Sudan iliyokumbwa na vita kwa zaidi ya miaka mitatu pia ulishughulikiwa." "Kwa maana hiyo," taarifa hiyo iliendelea, "hitaji la haraka la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, kutoa msaada kwa idadi ya watu, na kuanzisha mazungumzo ya dhati miongoni mwa vipengele vyote vya taifa la Sudan lilirudiwa, ili kukomesha mgogoro huo na kujenga amani pamoja."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
