Papa ametimiza mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake Papa ametimiza mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake  (AFP or licensors)

Jumbe na maoni katika kumbukizi ya Upapa wa Papa Leo XIV

Italia(CEI):“Tangu mwanzo Papa Leo XIV alituomba tuwe nabii wa amani,” Maaskofu Brazil na CELAM:“Mi mtu anayetokana na uzoefu wa kimisionari,sote tumeitwa, popote tulipo,kuwa wamisionari,”Askofu Farfán,mrithi wa Papa Leo XIV huko Chiclayo:“Urithi wake unaweza kufupishwa katika neno ushirika,"Jumuiya ya Mtakatifu Egio:Huduma yake kwa umoja wa Kanisa umekuwa ya thamani.Ni baadhi ya Jumbe za matashi mema kwa Mwaka wa Kwanza tangu kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Zimemiminika Jumbe na matashi mema kwa ajili ya kumtakia Baba Mtakatifu katika kufikisha mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake katika kiti cha Mtume Petro. Ni katika Siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Mama Maria wa Rozari Takatifu wa Pompei. Baba Mtakatifu ametumia fursa hiyo kuwepo katika Madhahau hiyo kwenye ziara yake ya kichungaji. Kwa njia hiyo katika ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia(CEI)  katika fursa hii tangu kuchaguliwa kwake Papa Leo XIV kunako tarehe 8 Mei 2025,  wlibainisha kuwa: "Kutokea kwenye Dirisha Kuu la katikati ya Basilika ya Mtakatifu Petro, katika salamu yake ya kwanza kwa watu wa Mungu, aliwasilisha kwa Kanisa na Ulimwengu maneno ya Bwana Mfufuka: 'Amani iwe nanyi nyote” na hivyo alituomba tuwe nabii wa amani; na tumeyapokea maneno haya kama agizo la kichungaji."

Rais wa CEI na Papa Leo XIV
Rais wa CEI na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Maaskofu hao wanabainisha kwamba katika salamu hiyo rahisi na ya dhati, “tulitambua kiini cha huduma yake: kumtangaza Kristo, amani yetu, na kuwaonesha wanadamu amani 'isiyo na silaha na ya kupokonya silaha, ya unyenyekevu na inayodumu'." Baraza la Maaskofu, kwa njia hiyo katika kumtakia matashi mema,  wakisema tena kwamba: “Katika mwaka huu wa kwanza, uliojaa vita, mivutano, na lugha iliyojaa migogoro, sauti yake imewaita kila mtu kwenye jukumu la amani: si kama kanuni  ya kufikirika, bali kama sharti la kiinjili na kazi ya kila siku, njia ya ukweli, haki, na mazungumzo."

Sala ya Jumuiya ya Kanisa la Italia kwa Papa

Baraza la Maaskofu aidha linakumbuka maneno yaliyosemwa na Papa kwa Maaskofu wenyewe wa Italia huko Assisi, mwishoni mwa Mkutano Mkuu wao kwamba : "mwaliko ulikuwa unabii wa amani kwa ulimwengu." Wito huu, “ unakaribishwa kama agizo la kichungaji, ili jumuiya zetu, katika Parokia, katika maeneo ya ndani, katika maeneo ya mijini na pembezoni mwa maisha, ziweze kuwa mahali pa kusikilizana, kupatanishwa, na ukaribu." Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia (CEI unahitimishwa na  uhakikisho wa "sala ya pamoja ya Jumuiya za Kanisa la Italia, kwamba Bwana “aweze kudumisha huduma yake na kulifanya Kanisa, chini ya mwongozo wake, kuwa ishara ya unyenyekevu na ya kudumu ya amani.”

Kardinali Baldo Reina, makamu Jimbo Kuu la Roma

“Katika ushirika na watu wote watakatifu wa Mungu wanaoishi Roma, leo tunakusanyika kumzunguka Askofu wetu, Papa Leo XIV, ili kuonesha upendo wetu na kumhakikishia maombi yetu, mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kwake kuwa Papa.” Ndivyo anaandika Kardinali Baldo Reina, Makamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Roma katika fursa hii muhimu ya kumbukizi. Kardinali Reina anabainisha kuwa: "Yeye ni miongoni mwetu mfano wa Mchungaji Mwema anayebeba furaha na matumaini ya kundi alilokabidhiwa, anayetangaza amani na huruma, anayefanya Injili ya upendo ionekane, na anayepanda tumaini kwa ukarimu.

Papa Leo XIV wakati wa Misa na Kardinali Baldo Reina
Papa Leo XIV wakati wa Misa na Kardinali Baldo Reina   (@Vatican Media)

“Madhimisho haya ya kwanza yanaangukia wakati ulio na migogoro na migawanyiko hatari, anaendelea Kardinali Reina,  "Shauku  ya amani ambayo Askofu wetu aliita tangu mwanzo wa upapa wake inakuwa unabii unaozidi kuwa muhimu kwa ulimwengu." “Kwa sababu hiyo, Kardinali Reina anabainisha tena: “tunaposema "asante" kwa Papa Leo kwa yote aliyoshiriki nasi katika mwaka huu wa kwanza, kwa uangalifu wake usiohesabika, kwa ziara zake nyingi, kwa mafundisho yake yenye matunda, kwa ukaribu wake uliooneshwa mara nyingi, na kwa upendo anaotuunga mkono, tunaahidi kwake kujitolea kwetu kuendeleza hamu ya wema na amani aliyoibeba moyoni mwake kwa ajili ya Roma na kwa ajili ya ulimwengu mzima.” Bikira Maria, Salus Populi Romani, amlinde na aambatane na nyayo zake kila wakati,” anahitimisha.

Maaskofu wa Brazil na CELAM

"Umekuwa mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV. Uchaguzi huo hauwakilishi mpasuko, kama mtu anavyoweza kufikiria wakati mwingine. Kuna mwendelezo. Na mwendelezo huu unatuletea, kila wakati upya, yaani, kila wakati kwa njia mpya, pumzi ya matumaini." Haya yameandikwa na Kardinali Jaime Spengler, Askofu Mkuu wa Porto Alegre, rais Baraza la Maaskofu nchini Brazili na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini katika tafakari yake kwenye tovuti ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki la Amerika Kusini(CELAM).

CELAM
CELAM

Papa ni mzoefu wa Kimisionari

Katika tafakari hiyo anabainisha kwamba, “Papa Leo XIV ni mtu anayetokana na uzoefu wa kimisionari, mmisionari bora kabisa. Na sote tumeitwa, popote tulipo, kuwa wamisionari: wamisionari wa matumaini, wamisionari wa maisha kamili kwa wote, wamisionari wa amani. Hakika, Papa Leo alizindua huduma yake kwa kutangaza kile ambacho Aliyefufuka anaendelea kutuomba sote kila wakati katika historia: kwamba tuwe watangazaji wa amani, mashuhuda wa amani, yaani  amani ambayo Aliyefufuka anatupatia."

Amani si sawa tu na kutokuwepo kwa migogoro

Rais wa CELAM, anabainisha kuwa: "Amani si sawa tu na kutokuwepo kwa migogoro. Amani ni zaidi ya hayo. Na Papa Leo XIV ametukumbusha hili kwa kuendelea, kwa mfano kupitia katekesi yake, akifufua kiini cha hati za Mtaguso wa Pili wa Vatican, lakini pia katika mikutano yake mbalimbali, na Katekesi  na miongozo, ambayo anatamani na hakutafuta kitu kingine chochote ila kuleta mioyoni mwa kila mmoja wetu msingi, msingi wa imani yetu na tumaini letu. Tunapoadhimisha mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwa Papa Leo kama mrithi wa Mtume Petro, tunaomba na kumwomba Mungu amwangazie, amtie moyo, na atusaidie kukuza zaidi ushirika na ushiriki katika maisha ya Kanisa kwa kuzingatia utume wake," anahitimisha

Askofu Farfán mrithi wa Papa Leo XIV jimbo la Chiclayo (Peru),

Askofu Edinson Edgardo Farfán Córdova, wa  Jimbo la Chiclayo, ambalo Papa Leo XIV alilihudumia kabla ya kuja Vatican, katika fursa ya kumbukizi hii muhimu aliandika katika tafakari iliyochapishwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Kipapa  cha Peru kuwa, “Kwa Jimbo langu pendwa la Chiclayo, ambalo limenipatia mengi" aliongeza “si usemi wa upendo tu, bali ni mchanganyiko wa kitaalimungu.  Unafichua uelewa wa kina wa Kanisa kama zawadi iliyopokelewa na kushirikishwa.

Papa alipokutana na wawakilishi wa Chiclay na Askofu wao
Papa alipokutana na wawakilishi wa Chiclay na Askofu wao

“Urithi wake unaweza kufupishwa katika neno ushirika"

Jimbo hili lilimfundisha kwa ajili ya utume wa ulimwengu wote." Kwa njia hiyo Jimbo Katoliki la Chiclayo, ambalo Askofu Robert Prevost (Papa Leo XIV) aliiongoza kati ya Novemba 2014 hadi  2022, kulingana na mrithi wake, alisisitiza kwamba "hapakuwa  mahali pa utume tu, bali jumuiya iliyomtajirisha mchungaji wake.” Upatanisho huu ndio msingi wa ushirika wa kikanisa: kutoa na kupokea, kufundisha na kujifunza, kuongoza na kushangazwa na tendo la Roho. Kwa hivyo, urithi wa Papa  Leo XIV "unaweza kufupishwa kwa neno moja: ushirika. Ushirika unaotafsiriwa katika kusikiliza, malezi, kujitolea kijamii, kuthamini kitamaduni, na uwazi wa sinodi.

Nchini Peru alijukana Askofu wa Ushirika

Katika Kanisa la Peru, alijulikana kama Askofu wa Ushirika; alituhimiza kuhamasisha utamaduni wa kukutana, mazungumzo, usawa, kusikiliza, utambuzi, na vitendo." Askofu  Farfán aidha anatafakari zaidi kuwa: "Ukaribu wake na maskini, wasio na ajira, na wahamiaji, hasa ndugu zake wa Venezuela, unaonesha Kanisa ambalo halijafungwa lenyewe.” “Katika nyakati ngumu, kama vile majanga ya asili au janga la Uviko-19, uongozi wake wa kinabii ulikuwa wa maamuzi. Miongoni mwa sifa muhimu zaidi za huduma yake, Askofu wa Chiclayo, anaendelea kuandika: "ni uwezo wake wa kusikiliza. Kipengele hiki hakiwezi kupunguzwa hadi sifa ya kibinadamu tu, lakini lazima kieleweke kama chaguo la kitaalimungu."

Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Papa Leo XIV
Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Papa Leo XIV   (@VATICAN MEDIA)

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio: Papa Leo XIV alitambua kuweka amani  kwana

Mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kwake, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaelezea, katika taarifa yake kuwa :“Huduma yake kwa umoja wa Kanisa umekuwa ya thamani. Akiwa amechaguliwa kuongoza Kanisa katika mojawapo ya nyakati ngumu zaidi katika historia ya sasa, alijua, kutokana na maneno yake ya kwanza, jinsi ya kuweka kipaumbele amani kama sharti muhimu kwa maisha na maendeleo ya watu na kwa ajili ya ulinzi wa walio hatarini zaidi na maskini, wahanga wa kwanza wa vita vingi vinavyoendelea. Tunamtakia kila la kheri kwa huduma yake muhimu kwa umoja wa Kanisa, kwa ajili ya mawasiliano ya Injili, na kwa ajili ya utume unaomsubiri duniani.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

08 Mei 2026, 13:00