Tor Vergata 2025. Tor Vergata 2025.  (@Vatican Media)

Mnamo Mei 14,Papa atafanya ziara katika Chuo Kikuu cha La Sapienza,Roma

Ratiba iliyotangazwa Aprili 25, na Ofisi ya Habari ya Vatican,inajumuisha ziara katika Kikanisa cha chuo kikuu,ikifuatiwa na mkutano wa faragha na Mkuu hicho,Antonella Polimeni.Ratiba ya asubuhi pia inajumuisha ziara ya maonyesho ya"Sapienza na Upapa"na mkutano na maprofesa na wanafunzi katika Ukumbi Mkuu ambapo Papa atatoa hotuba.

Vatican News.

Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kufanya ziara ya kichungaji katika Chuo Kikuu cha ‘La Sapienza’ cha Roma mnamo tarehe 14 Mei 2026. Ofisi ya Habari ya Vatican ilitangaza hilo  Jumamosi tarehe 25 Aprili 2026, ambao ni mpango wa ziara ya asubuhi ya Papa chuoni hapo, itakayoanza saa 4:20 asubuhi, katika kikanisa cha Chuo kikuu la "Divina Sapienza", ambapo Kardinali Baldo Reina, Makamu wa Askofu, Jimbo Kuu la Roma na Mkuu wa Chuo Kikuu Antonella Polimeni, na Padre Padre Gabriele Vecchione watamkaribisha.

Papa Leo XIV atakaa ndani ya Kikanisa kwa muda mfupi wa sala ya kimya kimya na kuwasalimia kundi la wanafunzi, kisha kusafiri kwa gari hadi uwanja wa kati, ambapo atawasalimia wanafunzi akiwa katika ngazi kubwa. Mkutano wa faragha na mkuu wa Chuo utafanyika saa 4:45 asubuhi katika Jumba la Mkuu wa Shule, ukifuatiwa na kusainiwa kwa Kitabu cha Heshima. Saa 5:00 asubuhi, bamba la kuadhimisha siku hiyo litazinduliwa kwenye Korido nje ya Ofisi ya Utawala, ikifuatiwa na salamu kwa wajumbe wa Seneti ya Taaluma na wafanyakazi wa Chuo Kikuu.

Papa Katika Mazungumzo na wanaotazama wakati ujao/mstakabali

Saa 5:15 asubuhi, Papa Leo XIV atatembelea maonyesho ya: "Sapienza na Upapa", yaliyowekwa katika uwanja wa Chuo kikuu. Dakika kumi na tano baadaye, atahutubia wahadhiri na wanafunzi katika Ukumbi Mkuu. Baada ya sherehe hiyo, zawadi zitabadilishwa na salamu itatolewa kwa ujumbe wa wanafunzi. Hatimaye, kabla ya kurudi Vatican, Papa atasimama kwenye ngazi kwa ajili ya kuwasalimia wanafunzi zaidi. Katika taarifa kutoka Vikariate ya Roma, Kardinali Reina alionesha furaha yake kwa ziara ya Papa katika Chuo Kikuu cha Roma.

"Papa Leo XIV daima alionesha kujali sana vijana na aliomba Jimbo Kuu lake  lisindikizane katika safari za ukuaji wa imani za vizazi vipya," alisisitiza Kardinali. Chuo Kikuu cha La Sapienza cha Roma ndicho Chuo kikuu kikubwa zaidi barani Ulaya. Kushiriki katika mazungumzo na wale wanaokabiliana na wakati ujao kupitia sayansi na utafiti mbalimbali ni muhimu sana. Tutasikiliza kwa makini kile ambacho Baba Mtakatifu atasema wakati wa ziara yake na tutakithamini kwa ajili ya huduma yetu ya Chuo kikuu na vijana."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

25 Aprili 2026, 16:30